Mkuu I salute you
Mimi hapo nawajua Cannavaro, Makassy, Tegete, Nsajigwa, na Bakar wengine Neeeeeeeeeeeeeey
Hahaaaaaaa........Ngoja nikujuze
1.Yaw Berko- Huyu ni kipa mghana ambaye tulikuwa naye tangu msimu uliopita,ndiye kipa bora wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu uliopita,
tulimsajili kutoka timu ya Liberty Proffesional ya Ghana.Akiwa golini mashabiki tunakuwa hatuna shaka naye kabisa,ila tatizo lake ni kwenye
penati,si mzuri sana kwenye penati kama Juma Kaseja....Tutegemee mazuri kutoka kwake hiyo kesho.
2. Oscar Joshua- Huyu ni mgeni,tumemsajili kwa ajili ya msimu ujao akitokea Ruvu Shooting Stars ya Pwani.Ni beki mzuri kweli na ameweza
kuliziba vema pengo la Stephano Mwasika ambaye ni majeruhi anayesubiri kufanyiwa upasuaji wa goti..Aanacheza vizuri sana na anapanda
mbele na kupiga krosi.Kaonesha kiwango kizuri na kuizoea timu kwa muda mfupi sana....
3. Chacha Marwa 'Muraa'- Huyu ni beki ambaye huwa hacheki uwanjani na ameweza kuelewana vizuri na Nadir Haroub na kuziba mapengo
yaliyoachwa na mmalawi Wisdom Ndhlovu na mghana Isack Boakye....Hataki utani huyu dogo na kwa umri mdogo alio nao nachelea
kusema kwamba hii ni hazina ya taifa huko mbeleni...
4. Juma Seif 'Kijiko'- Huyu kabatizwa jina la Jack Wilshire...Kwa kiwango alichoonesha mechi ya jana na St.George na hata mechi ya mwisho
ya Simba na Yanga dogo alidhihirisha kwamba ni kweli ana kipaji.Ana akili sana na anacheza mpira wa kisasa na nanchelea kusema ndiye
liyeibadilisha Yanga jana na kuifanya icheze mchezo wa kuvutia.Alielewana vizuri sana na Nurudin Bakari pale kati...Huyu tulimsajili mwaka
jana kutoka JKT Ruvu ya Pwani...
5. Godfrey Taita-Huyu naye ni beki wa kulia ambaye tumemsajili kwa ajili ya msimu ujao,tumemsajili akitokea Kagera Sugar.Anafanana sana
(kwa sura na umbo) na Shadrack Nsajigwa kiasi cha watu kuanza kuwaita mapacha.Kocha Sam Timbe anawachezesha pamoja yeye na
Nsajigwa na mara nyingi Taita anacheza kama namba 7 na wakati mwingine anarudi Nsajigwa anapanda.Dogo ana kasi na anapiga krosi za
kufa mtu.Yeye ndiye alipiga krosi zilizozaa magoli yote mawili wakati wa mechi ya Yanga na Bunamwaya....Tutegemee mazuri kutoka kwake
hiyo kesho.
6. Davies Mwape- Hili ni jembe kama Niklas Bendtner wa Arsenal,hana control ya mpira,anachojua yeye ni kutupia magoli wavuni tu,tulimsajili
wakati wa dirisha dogo la msimu uliopita akiwa mchezaji huru na kwa muda mfupi aliweza kuibuka na kuwa tishio katika ufungaji kwenye ligi
kuu ya VodaCom msimu uliomalizika.Ndiye aliyefunga goli la Video siku lilitupeleka robo fainali siku tulipocheza na Bunamwaya..