Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Yanga siwapendi kwa sababu moja tu, CCM.
 
Last edited by a moderator:

Kaka, wengi tuko Yanga lakini hatuipendi CCM kabisa.....tuko wengi tu!

Halikadhalika kule CCM wako wengi wanaoipenda "mishikaki ya msimbazi" (Sitta, Kapuya, Makamba snr, Sarungi - wengi tu!).

Haya mambo ya mpira tuyaache hukohuko kwenye mpira kaka!
 
Last edited by a moderator:
Yanga siwapendi kwa sababu moja tu, CCM.

Nkwingwa.....Rangi zisikuchanganye bana.....

Yanga imeanzishwa hata kabla ya TANU na CCM tangu mwaka 1935 na tangu wakati huo inatumia rangi ya njano na kijani.....Hao CCM wenyewe wameiba tu rangi za Yanga.......Wapende tu bana, usiwachukie....
 
Last edited by a moderator:
Bala (Nkwingwa) na M-mbabe,

Nafahamu sana na nilikuwa nataka kumchanganya Mchungaji kidogo. Nakumbuka hadi leo tukiwa chini ya mwembe Sikonge na enzi hizo bado kidogoo, nilishuhudia bendera ya TANU ikishuka na CCM ikipanda.

Kwa wale waliokula chumvi nyingi, wanakumbuka hadi UGALI WA YANGA. Huu ugali na mchele fulani hivi sijui uliitwaje? Nimesahau, nilikuwa na hamu sana navyo nile maana kila sehemu waliongelea juu yake ila Marehemu Mzee alikuwa anafanya juu chini tuwe na chakula karibu cha kutosha miaka miwili ijayo. Hivyo, njaa iliposhuka na Serikali kuleta Unga wa YANGA, sisi tuliusikia tu na huo mchele wa Bulga sijui?

Naona ule unga uliwafurahisha wengi na wakaamua kuipa CCM hiyo rangi 🙂

4.JPG
 
Hivi huyu Magamba hakugundua hizo kadi zilikuwa mpya zote?

Yanga Oyeeeeeeeeeeeeeee
 
kafie mbele

Mnalo kesho....

Chama letu litakuwa hivi hiyo kesho....

1. Yaw Berko
2. Shadrack Nsajigwa 'Fuso'
3. Oscar Joshua
4. Chacha Marwa 'Muraa'
5. Nadir Haroub 'Cannavaro'
6. Juma Seif 'Kijiko'
7. Godfrey Taita
8. Nurudin Bakari
9. Davies Mwape
10. Jerry Tegete
11. Kigi Makassy
 
Ila kweli yanga hizo jezi zinazofanana na CCM waziache sasa zinatuaibisha sana. Watafute uzi mwinine

Yanga siwapendi kwa sababu moja tu, CCM.

Last edited by a moderator:
Ila kweli yanga hizo jezi zinazofanana na CCM waziache sasa zinatuaibisha sana. Watafute uzi mwinine
Hizo ndizo rangi za klabu mkuu tangu mwaka 1935.......

Ni ngumu sana kuzibadilisha kwa sababu tu za kisiasa......

Ni sawa na kusema bendera ya Tanzania ibadilishwe kisa ina rangi za kijani na njano,rangi za CCM

Yanga Imara,Yanga Daima......

Daima mbele,Nyuma mwiko
 
Mnalo kesho....

Chama letu litakuwa hivi hiyo kesho....

1. Yaw Berko
2. Shadrack Nsajigwa 'Fuso'
3. Oscar Joshua
4. Chacha Marwa 'Muraa'
5. Nadir Haroub 'Cannavaro'
6. Juma Seif 'Kijiko'
7. Godfrey Taita
8. Nurudin Bakari
9. Davies Mwape
10. Jerry Tegete
11. Kigi Makassy

Mkuu I salute you

Mimi hapo nawajua Cannavaro, Makassy, Tegete, Nsajigwa, na Bakar wengine Neeeeeeeeeeeeeey
 
Hahaaaaaaa........Ngoja nikujuze

1.Yaw Berko- Huyu ni kipa mghana ambaye tulikuwa naye tangu msimu uliopita,ndiye kipa bora wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu uliopita,
tulimsajili kutoka timu ya Liberty Proffesional ya Ghana.Akiwa golini mashabiki tunakuwa hatuna shaka naye kabisa,ila tatizo lake ni kwenye
penati,si mzuri sana kwenye penati kama Juma Kaseja....Tutegemee mazuri kutoka kwake hiyo kesho.

2. Oscar Joshua- Huyu ni mgeni,tumemsajili kwa ajili ya msimu ujao akitokea Ruvu Shooting Stars ya Pwani.Ni beki mzuri kweli na ameweza
kuliziba vema pengo la Stephano Mwasika ambaye ni majeruhi anayesubiri kufanyiwa upasuaji wa goti..Aanacheza vizuri sana na anapanda
mbele na kupiga krosi.Kaonesha kiwango kizuri na kuizoea timu kwa muda mfupi sana....

3. Chacha Marwa 'Muraa'- Huyu ni beki ambaye huwa hacheki uwanjani na ameweza kuelewana vizuri na Nadir Haroub na kuziba mapengo
yaliyoachwa na mmalawi Wisdom Ndhlovu na mghana Isack Boakye....Hataki utani huyu dogo na kwa umri mdogo alio nao nachelea
kusema kwamba hii ni hazina ya taifa huko mbeleni...

4. Juma Seif 'Kijiko'- Huyu kabatizwa jina la Jack Wilshire...Kwa kiwango alichoonesha mechi ya jana na St.George na hata mechi ya mwisho
ya Simba na Yanga dogo alidhihirisha kwamba ni kweli ana kipaji.Ana akili sana na anacheza mpira wa kisasa na nanchelea kusema ndiye
liyeibadilisha Yanga jana na kuifanya icheze mchezo wa kuvutia.Alielewana vizuri sana na Nurudin Bakari pale kati...Huyu tulimsajili mwaka
jana kutoka JKT Ruvu ya Pwani...

5. Godfrey Taita-Huyu naye ni beki wa kulia ambaye tumemsajili kwa ajili ya msimu ujao,tumemsajili akitokea Kagera Sugar.Anafanana sana
(kwa sura na umbo) na Shadrack Nsajigwa kiasi cha watu kuanza kuwaita mapacha.Kocha Sam Timbe anawachezesha pamoja yeye na
Nsajigwa na mara nyingi Taita anacheza kama namba 7 na wakati mwingine anarudi Nsajigwa anapanda.Dogo ana kasi na anapiga krosi za
kufa mtu.Yeye ndiye alipiga krosi zilizozaa magoli yote mawili wakati wa mechi ya Yanga na Bunamwaya....Tutegemee mazuri kutoka kwake
hiyo kesho.

6. Davies Mwape- Hili ni jembe kama Niklas Bendtner wa Arsenal,hana control ya mpira,anachojua yeye ni kutupia magoli wavuni tu,tulimsajili
wakati wa dirisha dogo la msimu uliopita akiwa mchezaji huru na kwa muda mfupi aliweza kuibuka na kuwa tishio katika ufungaji kwenye ligi
kuu ya VodaCom msimu uliomalizika.Ndiye aliyefunga goli la Video siku lilitupeleka robo fainali siku tulipocheza na Bunamwaya..
 
Muraa tutakuona kesho li Mwakingwe litakavyokuwa linakupiga matobo ya kufa mtu, huku li Boban likitoa mapasi ya kuua viuno na nyonga, sijalisahau lile tulilolitoa Azam, kumbe na li Chuji litachesa, li Banka kama kawaida, Cholo piga mashuti ya mbali
 
July 19, 1977 : Simba 6 Yanga 0. WAFUNGAJI: Abdallah Kibadeni (3) dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' (3) dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20. Kumbukeni hii mechi inachezwa July pia
 
natamani niwe karibu na batalanda kesho pale taifa..
 
July 19, 1977 : Simba 6 Yanga 0. WAFUNGAJI: Abdallah Kibadeni (3) dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' (3) dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20. Kumbukeni hii mechi inachezwa July pia
hahahhhahmkuu Balantanda umeiona hii?
 
July 19, 1977 : Simba 6 Yanga 0. WAFUNGAJI: Abdallah Kibadeni (3) dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' (3) dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20. Kumbukeni hii mechi inachezwa July pia
sometimes history will change ila sina maana hiyoo..
 
Back
Top Bottom