changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Hakika Mkuu.
Pia mashabiki tulijitahidi kuwa wavumilivu mana Luc alikuja na gundu tukapoteza mechi mbili ile ya Azam na Kagera ambapo upande wa pili walianza kumbeza kumbe lilikuwa swala la muda tu.
Nina imani tutazidi kufanya vizuri zaidi huko mbeleni na pia yabidi nguvu zaidi tuzihamishie kwenye FA ili kuzidi kujihakikishua kucheza kimataifa mwakani.
Alibezwa hadi na washabiki wenyewe wa Yanga hasa baada ya kupoteza mechi ya pili dhidi ya Azam. Mashabiki wengi walianza kuulalamikia uongozi kwa kumleta huyu mzungu badala ya kumuacha Mkwasa. Kwenye mitandao ya kijamii watu waliandika kwa jazba kabisa kuwa mzungu arudishwe kwao hatumtaki.
Upande wangu niliiona yanga ikianza kucheza mpira unaoeleweka tokea mechi ya kagera ukiachana na swala la matokeo, maana matokeo yalisababishwa na makosa binafsi ya wachezaji.
Nina mashaka na huyu kocha kwenye upande mmoja tu, upande wa kukaa na timu kwa muda mrefu ndio shida ilipo. Huyu kocha angefaa sana kwenye kuijenga Yanga na kuwa moja ya timu iliyo ya ushindani na tishio kwa ukanda Africa, na kama inavyojulikana timu imara haiwezi jengwa kwa kipindi kifupi bali ni project ya zaidi ya msimu mmoja.
Sent using Jamii Forums mobile app