Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

MCHEZO DHIDI YA KMC FC .

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba juzi, siku ya Alhamisi, March 12 kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Taifa kumenyana na KMC katika mchezo ambao KMC watakuwa wenyeji.

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi jioni badala ya saa moja iliyopangwa awali kwa kile kinachoelezwa marekebisho ya hitilafu ya umeme uwanja wa Taifa.

Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Lindi kuifuata Namungo Fc tayari kwa mchezo ambao utapigwa March 15 katika uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa.
 
Naaam sportlady

Sent using Jamii Forums mobile app
 

SIRI YA KIATU CHA MORRISON

Kwenye Mechi ya Watani wa Jadi Mshambuliaji Benard Morrison alicheza kwa dakika takribani 56 tu katika mchezo dhidi ya Simba ambao aliifungia Yanga bao muhimu lililowafanya watoke kifua mbele ka ushindi wa bao 1-0

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael baada ya mchezo alibainisha kuwa Morrison aliumia mazoezini siku mbili kabla ya mchezo na ndio maana alimtoa mapema tu kwenye kipindi cha pili kwani hakuwa fiti

Lakini siri moja kubwa ni kuwa mapema wiki iliyopita Morrison alitembelewa nchini na mkewe akiwa pamoja na mtoto wake.

Walimletea zawadi ya viatu ambavyo alivitumia kwenye mchezo wa jana.

Bao lake alilofunga kwenye mchezo huo tena akiwa na viatu hivyo alivyozawadiwa na 'wife', lilipeleka furaha sio tu kwa Wanayanga bali hata kwa familia yake.

Morrison amebainisha kuwa viatu hivyo atavitumia katika mechi maalum tu "Vilikuwa viatu Maalum kwa kazi maalum Namshukuru Mungu nimeimaliza kazi salama".
 
sasa Simba imefikaje fikaje hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa update!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…