Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

LUC EYMAEL AMENIONGEZEA KUJIAMINI - MAKAPU

Mlinzi wa kati wa Yanga, Said Juma Makapu amesema mkufunzi wa timu hiyo Luc Eymael amekuwa akimpatia mbinu zinazomfanya kucheza michezo mingi ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila presha ikiwa ni tofauti na makocha waliopita huko nyuma.

Tangu kocha Eymael amejiunga na mabingwa hao wa kihistoria katikati ya msimu huu, amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza na kutengeneza muunganiko mzuri sehemu ya ulinzi pamoja na Lamine Moro, huku akimuweka benchi beki mkongwe Kelvin Yondani.

Akizungumza Dar es Salaam Makapu alisema amefundishwa na makocha wengi ndani ya kikosi hicho tangu alipojiunga akitokea Shangani FC ya Zanzibar lakini Eymael ndiye mwalimu anayempatia uhuru wa kucheza na kujiamini kabisa.

Makapu amemsifia Yondani kuwa ni beki bora na amekuwa akijifunza mbinu tofauti namna ya kukabiliana na washambuliaji wakali na kwamba kitendo cha kukaa kwake benchi sio kwamba kiwango chake kimeshuka. "Pamoja na kupewa nafasi ya kuanza bado Yondani ana kiwango kikubwa kuliko mimi kutokana na uzoefu wake wa kucheza michezo tofauti ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa Afrika," alisema Makapu.

Makapu alisema wakati anajiunga na kikosi hicho alianza kufundishwa na kocha Marcio Maximo na baadaye makocha kama Hans Van der Pluijm, George Lwandamina na Mwinyi Zahera lakini wote hao walikuwa wanamuweka zaidi benchi.

Ndani ya kikosi cha Yanga Makapu ni miongoni mwa wachezaji watatu waandamizi pamoja na Yondani na Juma Abdul baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kuwashinda nyota wengine waliopo.
 
Kajitajihidi sana hizi dakika za mwisho hapa kabla ya korona kumsimamisha. Aendelee kujifunza kwa yondani atakuwa bora sana
 
wachezaji wana lalamika mishahara hawajalipwa.tangu corona ianze[emoji24][emoji24][emoji24]

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
HATMA YA CHIKUPE, NGASA KUAMULIWA NA EYMAEL

Kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa, beki Andrew Vicent pamoja na Deus Kaseke na Tariq Seif ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.

Wakati baadhi ya nyota wameanza kupewa mikataba mipya, inaelezwa Eymael aliondoka na majina ya baadhi ya wachezaji ambao aliomba akawafanyie tathmini kabla ya kuidhinisha wapewe mikataba.

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa maamuzi kuhusu baadhi ya wachezaji yanamsubiri Eymael mwenyewe "Kocha kabla ya kuondoka aliomba orodha ya wachezaji wanaomaliza mikataba kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini yake nani na nani anawahitaji kwa msimu ujao" "Alitarajia kuyatuma majina ya wale ambao anawataka wabaki Ijumaa iliyopita lakini hakufanya hivyo, lakini bado uongozi unaendelea kumsubiria kuona kitu gani atakisema kisha kwa wale ambao watapendekezwa kubaki tutamalizana nao mara moja," alidokeza Bumbuli.

Hata hivyo Bumbuli amesema masuala mengine kuhusu mustakabali wa baadhi ya wachezaji yatafahamika baada ya msimu kumalizika "Sasa hivi siwezi kukwambia ni mchezaji gani ataondoka na nani atabaki. Tuwe na subira, msimu ukimalizika nadhani kila kitu kitafahamika".

@Yangadaima
 
MCHAKATO WA MABADILIKO YANGA SC KUKAMILIKA MAY

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo utakamilishwa mwezi May.

Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kubwa kuona jambo hilo likitokea.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka Wanachama wa klabu hiyo wakae tayari kupokea mabadiliko hayo "Tumeunda Kamati ambayo inasimamia mchakato huo, tunashukuru kila kitu kinaenda sawa, " amesena "Tumekuwa tukipokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali. Muhimu zaidi tumepata nafasi ya kwenda kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa" "Lengo letu ni kuwa na mfumo ambayo utaifanya Yanga isimame na kuweka historia ya Mafanikio".

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo mwaka uliopita, Dk Mshindo Msolla alitangaza suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kuwa kipaumbele chake cha kwanza..

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kujaribu kubadili mfumo wake wa uendeshaji kuwa kampuni.Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 Yanga imejaribu mara kadhaa bila ya mafanikio, mivutano baina ya wanachama ikikwamisha zoezi hilo.

Lakini hitaji la mabadiliko wakati huu limekuwa kubwa miongoni mwa Wanachama wa klabu hiyo.

Kama mpango huo utafanikiwa, Dk Msolla ataingia kwenye historia ya klabu hiyo kwa kufanikiwa kumaliza mchakato huo ambao watangulizi wake hawakufanikiwa kuukamilisha.

@Yangadaima
 
Huyo kocha ni mtaalam wa jadi nini Shadeeya? Eti kaondoka na orodha majina ili aende akayafanyie mchakato huko aendako kisha ndio arudishe Tanzania ya wale ambao atawaacha! Naona anaenda kumuuliza "babu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…