Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
LUC EYMAEL AMENIONGEZEA KUJIAMINI - MAKAPU
Mlinzi wa kati wa Yanga, Said Juma Makapu amesema mkufunzi wa timu hiyo Luc Eymael amekuwa akimpatia mbinu zinazomfanya kucheza michezo mingi ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila presha ikiwa ni tofauti na makocha waliopita huko nyuma.
Tangu kocha Eymael amejiunga na mabingwa hao wa kihistoria katikati ya msimu huu, amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza na kutengeneza muunganiko mzuri sehemu ya ulinzi pamoja na Lamine Moro, huku akimuweka benchi beki mkongwe Kelvin Yondani.
Akizungumza Dar es Salaam Makapu alisema amefundishwa na makocha wengi ndani ya kikosi hicho tangu alipojiunga akitokea Shangani FC ya Zanzibar lakini Eymael ndiye mwalimu anayempatia uhuru wa kucheza na kujiamini kabisa.
Makapu amemsifia Yondani kuwa ni beki bora na amekuwa akijifunza mbinu tofauti namna ya kukabiliana na washambuliaji wakali na kwamba kitendo cha kukaa kwake benchi sio kwamba kiwango chake kimeshuka. "Pamoja na kupewa nafasi ya kuanza bado Yondani ana kiwango kikubwa kuliko mimi kutokana na uzoefu wake wa kucheza michezo tofauti ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa Afrika," alisema Makapu.
Makapu alisema wakati anajiunga na kikosi hicho alianza kufundishwa na kocha Marcio Maximo na baadaye makocha kama Hans Van der Pluijm, George Lwandamina na Mwinyi Zahera lakini wote hao walikuwa wanamuweka zaidi benchi.
Ndani ya kikosi cha Yanga Makapu ni miongoni mwa wachezaji watatu waandamizi pamoja na Yondani na Juma Abdul baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kuwashinda nyota wengine waliopo.