Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Chura Churani fc, Utopolo FC, Yeboyebo fc timu inayoshikilia rekodi ya kuruhusu(kufungwa) magoli mengi zaidi katika hatua ya makundi ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika goli 19.
Source Mpangumbe.
 
MORRISON AHAIDI RAHA YANGA SC:-

Bernard Morrison ni moja ya wachezaji ambao walisajiliwa katika dirisha dogo kwenye kikosi cha Yanga akiwa mchezaji huru tangu alipoachana na DC Motema Pembe ya DR Congo.

Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa mkao wa kula kwani anajipanga kuwa na kiwango bora zaidi ya kile alichokionyesha katika mechi chache alizoichezea ambacho hajaridhika nacho. Akizungumza na Mwanaspoti Morrison alisema kuwa mechi aliyofunga bao pekee la ushindi dhidi ya Simba ndio alikuwa anaanza kuwa katika makali yake.

"unajua hata wakati nacheza mechi na Simba nilikuwa na maumivu ya mguu ndio maana baada ya kuifanya kazi ambayo niliagizwa na kocha wangu nilitolewa.

Kwa muda mchache niliokuwa hapa Tanzania nadhani bado sijacheza kwa kiwango ambacho natamani kukiona kwanza nilikuwa sijazoea mambo mengi lakini kwa sasa naona vitu vingi vipo sawa," alisema.

"Nikirudi katika ligi nitakuwa nimeimarika zaidi kwa maana hiyo nadhani kuna vitu vingi ambavyo nitavifanya uwanjani katika kila mechi ili kuona timu yangu inaweza kupata ushindi.

Nadhani nikifanya mambo mengi mazuri kwa timu yangu nitaweza kuisaidia kupata matokeo ambayo inahitaji lakini kufikia malengo yake wakati huo huo nitakuwa najitangaza mwenyewe," alisema Morrison.
Mume halali wa mikia amesema sisi ni akina nani hata tumpinge!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga kura kwa klabu yako ya Yanga ukifika bonyeza kwenye nembo ya yanga tu itabadilika na kukuonyesha asilimia utakua umeshapiga kura fuata link hii [emoji116]

Mwananchi Piga kura ili timu yako iingie kwenye list ya timu za Pro Evolution Soccer 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MABOSI:- MKWASA KUKABIDHIWA TIMU

Mabosi wa Klabu ya Yanga wamechungulia mbali na kuona ligi inaweza kurejea hivi karibuni lakini bila ya kuwa na makocha wao wawili, Kocha Mkuu Luc Eymael na yule wa viungo, Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini. Sasa kwa ajili ya kuweka mipango sawa bila ya kutetereka, mabosi hao wa Yanga wameamua kumuachia mikoba kocha msaidizi, Charles Mkwasa kuwa ndiye awe msimamizi mkuu wa timu hiyo wakati ambao Eymael atachelewa kurejea nchini endapo tangazo la ligi kuendelea litakapotangazwa. 

Mabosi hao wamefikia muafaka huo baada ya kuona Eymael ni ngumu kurejea Bongo kwa sasa kutokana na kwao, Ubelgiji kufunga uwanja wa ndege kutokana na janga la Corona ambapo pia akirejea atatakiwa kubakia karantini kwa siku 14.

Habari ambazo Championi limezipata ni kwamba timu hiyo itakuwa chini ya Mkwasa ambaye wamejiridhisha kuwa kutokana na uzoefu wake, ataweza kuibeba timu hiyo kwenye mechi zilizobaki.

Kabla ya kuja Eymael, Mkwasa aliachiwa timu hiyo baada ya kocha mkuu Mwinyi Zahera kuvunjiwa mkataba wake. “Inaonekana labda kocha Eymael anaweza kuchelewa kurejea Bongo kama ligi itaanza hivi karibuni, lakini hilo tayari limeshafanyiwa utaratibu wa kuweza kulikamilisha na kuwa vizuri.

“Kitakachofanyika ni kuwa Mkwasa ndiye atapewa timu aiendeshe kwa wakati huo kwa sababu wengi wamemuamini kutokana na kile alichokifanya wakati alipopewa timu baada ya Zahera kuvunjiwa mkataba,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wake, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema mipango hiyo wanaendelea nayo kuhakikisha hawapati tatizo lolote hata kama kocha huyo atachelewa kurudi na ligi ikianza.
 
Shadeeya unajua Mkwasa yeye plani zake kuifunga Simba tu basi anakua ameridhika, hana mipango ya kuiendeleza Yanga baada ya hapo!!!
 
DANTE ACHIMBA MKWARA YANGA .

Beki wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ amesema Ligi Kuu Bara itakaporejea anaamini kwamba atarejea katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa zamani. Katika msimu huu wakati unaanza, Dante alichelewa kujiunga na wenzake baada ya kuweka mgomo wa kutaka kulipwa pesa zake za usajili na ndipo akapoteza namba katika kikosi cha kwanza alipokuwa anacheza na Kelvin Yondani.

Akizungumza na Mwananchi, Dante alisema baada ya kutokea janga la corona anaamini kila kitu kimeanza upya, hivyo kurejea kikosi cha kwanza ni rahisi. “Unajua muda kama huu kila mtu hafanyi mazoezi ya timu, tukienda tunaenda kuanza wote kwa pamoja ndio maana nakuambia tunaenda kuanza upya, kwa hiyo nitatumia nafasi hii vizuri kurejea katika kikosi cha kwanza,” alisema.

“Mimi naamini kiwango changu kwamba suala la kucheza ni la muda na ndio maana siku zote siachi kufanya mazoezi, nitafanya mazoezi mchangani na nitacheza mpira, haya yote ni mazoezi.”

Akizungumzia upande wa programu walizoachiwa na kocha wao, Luc Eymae, alisema tayari zote alishazimaliza kikamilifu na kwamba, kwa sasa anaendelea kujifua ili aendelee kuwa fiti zaidi.

Dante ana wakati mgumu wa kutetea namba mbele ya beki Lamine Moro na Kelvin Yondani ambao wameonekana kuelewana zaidi, huku pia anapokosekana Lamine au Yondani, basi Said Makapu huwa anachukua nafasi hiyo, hivyo bado anatakiwa kupambana.
 
LUC EYMAEL AUKWEPA MTEGO WA ZAHERA .

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ameweka wazi kwamba katika kikosi chake cha msimu ujao atakachofanya ni kutosajili wachezaji wengi badala yake atafanya maboresho tu kidogo.

Eymael raia wa Ubelgiji, amefunguka kwamba hahitaji wachezaji wengi katika kikosi chake cha msimu ujao badala yake analenga kuchukua wachezaji wachache ambao watakuja kuongeza nguvu kwa waliopo sasa.

Eymael ameongeza kwamba hatafanya kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo kikosi hicho kilisajili zaidi ya wachezaji 11 kwenye dirisha kubwa la usajili wakati kocha mkuu akiwa Mwinyi Zahera raia wa DR Congo.

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa mipango yake kwa sasa ni kuongeza nguvu mpya za wachezaji wachache katika wale ambao wamebakia kwa ajili ya kuifanya timu hiyo kwa msimu ujao kuwa na nguvu ya kupambana. “Ripoti juu ya nani na nani wasajiliwe tayari niliiwasilisha kwa viongozi na kuweka wazi kwamba nahitaji nafasi hizi na hizi katika kikosi cha msimu ujao.

“Nitakachofanya ni kutokuwa na kundi kubwa la wachezaji kwa sababu kuna wengi ambao wapo kikosini kwa sasa nimewaona wanaweza kutusaidia, kwa hiyo ni kuwaongezea kiasi kidogo cha wachezaji kisha wafanye kazi.

“Nataka kujenga kikosi imara kwa hiyo sitaweza kusajili namba kubwa ya wachezaji badala yake nitawaboreshea kwenye maeneo kadhaa kisha tutakuwa tayari kupambana,” alimaliza Mbelgiji huyo.

Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu na kuachwa ni Juma Balinya, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo na Mustafa Seleman ambao walionekana kushindwa kufi kia malengo.
 
Bora iwe hivyo kwakweli
20200316_151541.jpg

CORONA IISHE AISEE. 😎😎
 
Back
Top Bottom