Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Hivi Shaban Ramadhani yuko wapi? Namkubuka kuna siku tuliwafunga Simba alikuwa amevaa fulana imeandikwa NATO
 
yanga jogoo la bongo lakini likitoka nje tu huwa kuku jike
 
Kawaida wanachama wa yanga wanakuwaga natabia za ubishi sana.
Bishana mpaka ufe.....ndio motto ya yanga.
 
Yanga mabingwa wa Tusker

December 28, 2009

Wachezaji wa Timu ya Yanga wakisherehekea Ushindi baada ya kunyakua Kombe la Tusker katika mchezo wa Fainali ambapo waliwalaza wapinzani wao Sofa Paka ya Kenya 2-1. Picha na Michuzi
TIMU ya Yanga imefunga mwaka kwa 2009 kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Tusker kwa kuichapa Sofapaka kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga walilazika kusubili hadi dakika tano za mwisho kuanza kusherekea ubingwa wao kwa mabao yaliyofungwa na Mrisho Ngassa (90 dk), na Boniface Ambani (85dk).

Mabingwa hao wa Tanzania wamefanikiwa kujinyakulia shilingi milioni 40, huku ndugu zao Simba wakijinyakulia nafasi ya tatu Mil 10 na Wakenya hao Sofapaka washindi wa pili walijinyakulia Mil 20.

Mshambuliaji Jerryson Tegete alikabidhiwa zawadi yake ya ufungaji bora Mil 2 baada ya kufunga jumla ya mabao 6 kwenye michuano hiyo, huku Mafunzo ya Zanzibar imepata tuzo ya timu yenye nidhamu.

VITUKO
Wachezaji wa Sofapaka waliwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kubadilishia nguo uwanjani badala ya kwenye vyumba vya kubadilishia kabla ya kuanza kwa mchezo huu.

Baada ya filimbi ya mwisho wachezaji wa Sofapaka wakiongozwa na kipa wao Obungu walimvamia mwamuzi Denis Batte kutoka Uganda wakitaka kumpiga, lakini kikosi cha kutuliza ghasia 'FFU' waliwahi kuzima jaribio hilo.

Yanga:Obren Cuckovic, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Bakari Mohamed,Nadir Haroub, Athuman Idd, Nurdin Bakari, Abdi Kassim, Jerry Tegete, Mrisho Ngasa, Kigi Makasi.
Sofapaka: Wilson Obungu, Kamadi Michael, James Situma, Tumba Kilonzo, Edger Ochieng, Nicolaus Muyoti, Humphrey Ochieng, Kimani Antony, Wanyama Thomas, Bob Mugaliya, John Onami.
 
Wakati wa mashindano ya Kombe la Kagame pamoja na yale ya Tusker Challenge Cup wenzetu wa toka Kenya na Uganda walikuwa na majina ambayo yalinikumbusha enzi zile nikiwa nafanya kazi ya geshi na hivyo kufanikiwa kufahamu maana ya majina hasa yale yenye asili ya kijaluo. Nilipoyasikia tena safari hii yalinikumbusha mbali sana miaka ile ya 1970.

Baadhi ya majina hayo na maana yake ni hii:

Obungu = kichaka
Otieno = usiku
Onyango = adhuhuri
Oluoch = mawingu
Okeyo = kuvuna
Oludo = kusia mbegu
Odipo = zizi
Ochieng' = jua/mchana
Okoth = mvua
Ondiek = fisi
Oliech = tembo
Ogwang' = mnyama

* Mwanaume jina lake huanzia na herufi 'O' wakati mwanamke huanza na 'A'

Nilikumbuka mbali sana.
 
Ambani katupia goli tatu juzi....yanga daima mbele...nyuma mwiko
 
 
Ligi Kuu ya VODACOM-YANGA 1 JKT RUVU 0-MRISHO NGASA
 
Kipofu kaona mwezi....Timu ya kwenye bonde la mpunga!

Bonde la mpunga lakini lakwetu.
Nyie Simba mbona mnashindwa hata kupaka rangi jengo lenu?

Hv wachezaji wenu wanajisikiaje wakipita ktk Villa letu huku kila chumba kikiwa na AC?
 
nadhani habari zote za Yanga yetu zikiingia hapa itapendeza zaidi maana kuna mithread ya kizungu tu. wadau wa soka la bongo hasa Yanga tupeni raha kuanzia hapa na kuendelea
 
.......wewe Mziwanda tuondolee kandambili zako hapa bana!!..teheehehe!

Yeboyebo mwenzio alishaiweka hapa siku nyingi sana....itafute huko huko kwenye michezo!
 
dah! mbona imepotezwa sasa? nao MODS basi wasiache habari za timu yetu tukufu kuzagaa ovyo tu. waziweke pamoja jamani
 
why washabiki wengi wa yanga ni iliterate?????????????????????
 
why washabiki wengi wa yanga ni iliterate?????????????????????

kwa vigezo vipi, mkuu? si bora mashabiki kuwa hivyo kuliko huyo broker wenu? ashukuru Mungu kaepushiwa kikombe cha shahada. nina hofu na wewe pia
 
why washabiki wengi wa yanga ni iliterate?????????????????????
.....kwi!kwikwikwikwiwiwwwww.....teheteheheeeeee....u made my dei Boss! unatumia kinywaji gani? waiter please....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…