Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mazungumzo ya mkataba mpya baina ya uongozi wa Yanga SC na wachezaji wakongwe Juma Abdul na Kelvin Yondani yanaelekea kukwama na huenda pande zote wakapeana mkono wa kwa heri.

Wachezaji hao kila mmoja kwa wakati wake alikuwa tayari kusaini mkataba wa kusalia Jangwani lakini kikwazo kilikuwa hakuna hela ya usajili 'Signing Fee' ambapo mhusika atalipwa mshahara tu jambo hawajaafiki wachezaji hao.

Na Yanga SC wameshaanza mikakati ya kutafuta wabadala wa nyota hao!
 
Mnaojua kuhusu hiyo Signing fee imekaaje eti kwa wachezaji wasainiwa wapya na wale wenyeji? 🤔🤔🤔
 
Ni mpambanaji sana

Ni dalili ya kuachana na Yondani
Aendage tu huyo kama anataka kwenda sababu hapa mwisho mwisho alikuwa anachezea sana benchi na Uwanjani mambo kwa Timu ya Wananchi yalikuwa yanaenda.
 
TETESI ZA KOCHA MPYA YANGA

Hatima ya kocha kujulikana Jumatatu

Mpka kufikia Jumatatu ya tarehe 10 kuna uwezekano mkubwa Klabu ya Yanga itakuwa imesha tangaza kocha mpya anae kuja kukinoa kikosi cha Mabingwa wa kihistoria Tanzania.

Wachezaji wote wa ndani wanatarajia kuanza mazoezi siku ya Jumatatu (10/08/2020) kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara na mashindano mengine. Kwa wachezaji wa nje ya nchi ambao watarudi kuitumikia Klabu yetu mwisho wa kuripoti ni tarehe 13.

Kocha anaetajwa kuwa katika nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Luc ni Ettiene Ndayiragije ambae ni kocha wa Taifa Stars kwa Sasa.
 
Mnaojua kuhusu hiyo Signing fee imekaaje eti kwa wachezaji wapya ma wale wenyeji? [emoji848][emoji848][emoji848]
Signing fee maana yake ni pesa anayopewa mchezaji ili asaini mkataba mpya au ku renew mkataba wake. Nje ya mshahara pamoja na bonus atakazokua anapata kila mwezi au week kwa timu nyingi za ulaya.

Mfano Yondani anaweza akasema ili ni saini mkataba mpya nipeni milioni 10, (nje ya mshahara atakaokua analipwa kutokana na mkataba anaousaini)
 
Ooooh!! Sasa imekuwaje hao viongozi washindwe kuwapa hao kina Yondani na kutaka kuwasainisha bure bure?
 
kuna tetesi yanga wanataka kumsajili Lusajo wa namungo, kwa maoni yangu yule hana tofauti na tariq seif, ni mchezaji wa kawaida sana na si level za yanga.
 
Angekuwa wa ndani nisingekuwa na shida

Ila kwa mchezaji wa nje, inabidi awe mkali kweli kweli

Yaani mchezaji wa nje inabidi awe piga ua ana uwezo wa kucheza first 11, labda kocha kwa sababu zake aamue kutomwanzisha

huyu ni wa ndani lakini style yake ya uchezaji haina tofauti na Tariq, sema Tariq pressure ya timu kubwa imempa changamoto.

Hata yule Blaise wa kawaida sana, kama Yanga inataka kuchukua ubingwa si aina ya wachezaji wa kwenda pale.
 
Ni mtanzania kumbe Blaise Bigirimana, hata kiswahili chake ni majirani zetu
huyu ni wa ndani lakini style yake ya uchezaji haina tofauti na Tariq, sema Tariq pressure ya timu kubwa imempa changamoto.

Hata yule Blaise wa kawaida sana, kama Yanga inataka kuchukua ubingwa si aina ya wachezaji wa kwenda pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…