Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mtani umesababisha nicheke kwa sauti aisee.

Kwa hiyo mkipanda basi la timu na kucheza ni kazi yenu itakuwa!
Hahahaaa. Aliongeaga hivyo yule jamaa wa Utopolo ujue sio mimi.

Mi mwenyewe nikabaki nacheka tu yaani hapo alimaanisha wachezaji nao waone vile mashabiki wanapata tabu timu inapofanya vibaya.
 
Wacha waende CAS ndo pcha litakua tamu zaidi. Ndo watajua hawajui
Acheni kututisha na tarabu zenu za Manara, kwanza hakuna mtu muongo kama Manara. Issue ya kushushwa daraja ni kutokana na upangaji wa matokeo. Issue za usajili kama hizi timu haiwezi kushushwa daraja hua inafungiwa kusajili, mfano mzuri kuna team ya Ethiopia huko imemzingua yule aliyekua kipa wenu wa zamani na wamefungiwa miaka mitatu kusajili na sio kushushwa daraja.

Japo sina uhakika kama Yanga wataenda huko ila vitisho vyenu vya kiboya kama hivi havitushtuwi hata kidogo.
 
Viongozi wa Yanga waache ujanja ujanja kwanini wasingekaa na mchezaji wakasaini mkataba tu bila shida yoyote badala ya kufanya forgery?

Au kwasababu wao hawakumsajili Morisson hivyo hawakuwa concerned na contract yake ina muda gani ?

So sad.
Kutokana na maelezo ya kamati wanadai mkataba haujafojiwa ila una mapungufu.. Hayo mapungufu yametokana tu utamaduni wa klabu nyingi tu kusajili kienyeji enyeji bila kuangalia mbeleni kua kuna mambo kama haya yanaweza kutokea huko mbele.
Na tatizo kubwa Yanga na GSM hakuna connection nzuri hapa katikati, wanafanya vitu bila kuzingatia protocol,, kifupi vitu vingi havipo professional kwenye timu yetu.
 
Hela ya kumpa sureboy hamna, mtakuwa nayo ya kumpa Bwalya[emoji196][emoji196][emoji196]


Vichekesho
 
Hela ya kumpa sureboy hamna, mtakuwa nayo ya kumpa Bwalya[emoji196][emoji196][emoji196]


Vichekesho
Yanga walipeleka ofa ya 35M kwa sure boy Azam wametaka si chini ya 70M, halafu wakati huo mchezaji amebakiza mkataba wa mwaka 1. Hata kama mtu una ela za kuchezea huwezi kufanya biachara kichaa kama hii.
 
Kamati ilitoa hoja dhaifu sana.

Kama mkataba ulikuwa na mapungufu hayo mapungufu ni kwa kiasi gani yameathiri validity ya mkataba.?

Je TFF waliweza vipi kupokea na kuendorse usajili wa Morisson wakati mkataba una mapungufu?

Kamati either imewaonea Yanga au imewabeba Yanga.
 
Kimsingi watashushwa daraja na kuwadiscredit sana tff
Kweli kabisa mkuu. Yale mapungufu ya kwenye ule mkataba sio madogo. Actually kuna jinai pale na ni tusi la moja kwa moja(direct insult) kwenye familia ya mpira Tanzania, kuanzia kwa wachezaji, vilabu, mashabiki na hata kwa shirikisho la mpira lenyewe
 
Wakithubutu kwenda huko ndio wanajimaliza kabisaaa. Makaburi yote yaliyofunikwa kwa kutumia busara za tiefuefu yatafukuliwa!

Kama hawaogopi kushuka daraja basi waende huko CAS
Tff kwann walipitisha huo mkataba?? Kama walipitisha basi wa kwanza kupigwa chini ni tff maana wao ndo washauri na watendaji wakuu katika kuendesha timu, na mashabiki tunaamini kuwa wao ndo jicho la mpira wa kibongo.
 
Tff kwann walipitisha huo mkataba?? Kama walipitisha basi wa kwanza kupigwa chini ni tff maana wao ndo washauri na watendaji wakuu katika kuendesha timu, na mashabiki tunaamini kuwa wao ndo jicho la mpira wa kibongo.
Definitely kutakua na consequences hata kwa viongozi wa Shirikisho letu la soka, lakini Yanga ndio culprits kwenye hii issue na ndio wataathirika zaidi
 
Definitely kutakua na consequences hata kwa viongozi wa Shirikisho letu la soka, lakini Yanga ndio culprits kwenye hii issue na ndio wataathirika zaidi

Yote hii namlaumu Manara na Morrison wake kwani kama sio wao kulisuka jambo hili leo tusingekuwa tunapigishana kelele hapa
 
Kwa timu yenu hiyo mkifungiwa kusajili itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…