Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mnalo la kujiuliza hapo mtani, maana Mkienda kwenye yale mashamba yenye visiki vya miwa, utamuelewa huyo kalinyo wenu kwa nn alikimbizwa kwao
Juzi mlisema tukitoka nje ya Taifa hatuna chetu leo mnasema tukienda kwenye mashamba ya visiki. lol.

Huko nako tutafanya wonders sijui mtasingizia nini Mtani.
 
Mechi ijayo na mtibwa Yanga waanze na Waziri junio kwenye 433, sarpong hana movement nzuri, pale mbepe panatakiwa striker mwenye mikimbio mizuri ili kufungua chance za viungo kupiga pasi za mwisho, Sarpong anakimbia kimbia tu kama kuku mwenye kideri.
 
Hongereni Ntan.. ila nadhan maneno yangu hujayasahau, tatizo lenu la kufumania nyavu bado halijapona, tegemea suluhu nyingi sana
Ahsante Mtani. 🤝

Sijayasahau Mtani na hapa inabidi lifanyiwe kazi hasaa kwani Sarpong naye ana mechi na mechi sababu kama hii ya leo utadhania hakuwepo vile, Yule Yacouba naye bado tia maji tia maji, Tuisila Pupa nyingi basi tabu tupu.

Kazi ipo kwa kweli Mtani hasa kwa Kocha.
 
Naona kocha baro anatafuta kikosi cha kwanza ila mabadiliko yameonekana walipoingia Niyonzima, Kaseke na Carlinho.

Viva Young Africans [emoji617]

Sent using Jamii Forums mobile app
Yambidi achangamke kupata first eleven kwani kadri tunavyosonga ndo na ligi inachanganya.

Na zile sub zimesaidia sana aisee kwani walau kukawa na uchangamfu wa timu.

"DaimaMbeleNyumaMwiko"
 
Mechi yenu leo ni kama haikua na plan kabisa, yani kuonyesha tu kwamba hii timu kuna kitu inatafuta hakuna, kuna kazi kubwa sana ya kufanya

mna kazi ya kujenga kikosi, sisi tuna kocha kiaz [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Yambidi achangamke kupata first eleven kwani kadri tunavyosonga ndo na ligi inachanganya.

Na zile sub zimesaidia sana aisee kwani kukawa na uchangamfu wa timu.

"DaimaMbeleNyumaMwiko"
Sijui ni macho yangu tu .. ila nadhani Tuisila anafaa kutumika kama "Mpango Maalumu" ukiacha upuuz wake wa hapa na pale yule jamaa ana pace moja hatari sana, probably kuliko full back yeyote yule atakae kutana nae..na ana uwezo mkubwa tu wa kugeuka na kuingia ndani, anafaa kutumika kama njia ya kupitisha mashambuli, ila awe na maelekezo, kupiga kross na V pass ziwe amuzi lake la kwanza, kufunga mwenyewe liwe amuz la mwsho, mtamfurahia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…