NYAMAZENI HAMNA CHA KUWAELEZA WANANCHI
Anaandika @exaud_msaka_habari
Kuizungumzia Yanga inahitaji uwe na akili sana maana unaweza kusema kitu hata usieleweke. Unatamani uisifie kiwango chake kuna roho inakuambia nyamaza, unatamani uwakosoe kuna roho inakuambia nyamaza wewe
Huna cha kuwaambia wananchi, huna cha kuwaeleza wakuelewe wakati wameshinda Goli Mbili Kirumba, Kama unasubiri Biriani endelea kuisubiri ila Wananchi wameshinda.
Unataka kuwaambia wananchi bado hawaeleweni? Watakulaani, wanakupiga mawe Yanga imeshinda Mbili Kirumba.
Unataka kuwaambia bado umiliki wa Mpira kwao sio wa kiwango mnachotarajia? Watakuelewa? Yanga ameshinda Mbili Kirumba.
Unataka kuwaambia Yanga Sarpong Bado sio mfungaji wa kutegemewa, watakuambia asipofunga yeye atafunga Waziri Jr. Asipofunga Sarpong atafunga hata Mukoko. Wananchi wanayo majibu sahihi ya kukujibu.
Kiwango cha Kisinda usiwaeleze kabisa wananchi watakuambia kafunga leo, Wananchi wameshinda.
Wananchi wapo juu ya Simba na wanamsogelea Azam huna cha kuwaambia wananchi, ukiwaambia kitu utakuwa unajisumbua tu.
ALL IN ALL USIWAAMBIE WANANCHI KUHUSU ILE PENAT YAO