Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Nimekuwa kipofu kwa bao la Mwaisa David Kaseke, nikitazama macho yananiambia mpira ulivuka mstari, nikifumba na kufumbua tena macho yananiambia yule beki alinyanyua mguu ukiwa sambamba na mstari wa goli. Kwa maana hiyo mpira haukuvuka wote mstari. Pale unahitaji bahati ya kipenga cha mwamuzi ikuokoe.

Penalti ya Pastory Atanas ilikuwa sahihi. Hakukuwa na utata sana dhidi ya Yassin Mustapha. Mpira ulipiga mkono kwasababu mkono haukuwa katika eneo lake halisi. Sijui kwanini 'reaction' ya wachezaji wa Yanga ilikuwa vile. Hapa si Macho yangu tena bali hakika yangu inaniambia ni penalty.

Tunaweza kumminia refa kila aina ya lawama. Tunaweza kuwatukana wasaidizi wake kila aina ya tusi, lakini tukumbuke kuwa uwanjani tukio linaonekana kwa mara moja. Sisi tunapata nafasi ya kurudia-rudia, ndiyo maana tunaweza kutoa tafsiri sahihi. Nazidi kuelewa kwanini wazungu wamekubali kuzidisha teknolojia viwanjani. Muda mwingine, marefa wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.

Wananchi niwaambie kitu?? Nilijua mmeamua kuleta magoli kwa kumsajili mshambuliaji wa kati, Fiston Abdulrazaq. Lakini nadhani Cedric Kaze anataka kutuaminisha tena kuwa, mlisajili winga na siyo mshambuliaji wa mwisho. Mbona anatumia muda mwingi kukimbia mbali na lango kiasi kile??

Wananchi mnaweza kumchukia Michael Saprong, wapinzani mnaweza kumtanania Michael Saprong. Lakini mkituliza kichwa kuna kitu cha ziada mnaweza kukikubali kwake, anajua kutunza mali, anajua vita ya nguvu, anachokosa ni kile kinachotafutwa kwa washambuliaji wote duniani, MABAO. Wananchi kama mtaamua kumfanya mpishi zaidi ya mlaji, mnaweza mkafaidi zaidi.

Pastory Atanas, NDIYO mzee. Mabeki wagumu kama 'rastaman' Mustapha Yassin, wanahitaji mawinga wasumbufu kama Pastory mwana Atanas. Alimkosa mtu mmoja tu, Kibu Denis. Labda Kibu angekuwepo Lamine na Bakari wasingekula bata kama vile.

Japo mnaweza mkanichukia lakini acheni Niwaambie ukweli mwingine wananchi, leo mmedondosha pointi mbili za muhimu sana kwasababu ya UBUTU mlionao kwenye safu yenu ya ushambuliaji. KUNRADHI, Pale mwisho hampo makini kabisa WANANCHI.
 
Sifa kubwa ya team kuwa bingwa ni kuchukua point kwenye teams ambazo yuko nazo kwenye mbio za ubingwa
Yanga vs Azam tiari 3
Yanga vs Simba tiari 1
Total 4
Simba vs Azam 1
Simba vs Yanga 1
Total 2
Huwez kuwa bingwa Kama huwezi wa piga unaoshindana nao
Azam yuko kwenye ubingwa upi we utopolo
 
Sifa kubwa ya team kuwa bingwa ni kuchukua point kwenye teams ambazo yuko nazo kwenye mbio za ubingwa
Yanga vs Azam tiari 3
Yanga vs Simba tiari 1
Total 4
Simba vs Azam 1
Simba vs Yanga 1
Total 2
Huwez kuwa bingwa Kama huwezi wa piga unaoshindana nao
Msimu ulioisha ulichukua point 4 kwa simba , ulibeba ubingwa wa wapi ? Kidimbwi ?
 
Nasema ukweli Yanga kwa mwendo huu hawezi kuchukua ubingwa tulikuwa na nafasi nzuri maana mtani wetu tulimwacha mbali nadhani viongozi wa simba wana mbinu kuliko viongozi wa Yanga vinginevyo kocha asiachiwe peke yake kusajili timu unajua wenzetu simba kocha hasajili timu bali viongozi kama kuna haja ya kumshirikisha kocha wanafanya hivyo alisema Hanspoppe kama wiki mbili zimepita hawa wachezaji aliosajili Kaze sidhani kama wataisaidia Yanga kama Yanga anataka ubingwa abadilike
 
Ila vitu vingine vinashangaza Mikia mnang'ang'ania Yanga hawezi kuwa bingwa mpaka sasa mumempita Points ngapi kwa huo ubora wenu mulio nao.

Mana kama mngekuwa bora mlipaswa mtuache mbali sana, sasa ikiwa mpaka viporo vyenu mlivyo navyo mufanikiwe kuvila ndio tunakuwa points sawa, sasa huu ujasiri wa kwamba Yanga haezi kuwa bingwa mnautoa wapi.

Haya maneno wanapaswa ziongee zile timu ambazo unakuta ziko mechi sawa na wenzake lakini anaongoza points hata 10 au zaidi na ligi ndo inaelekea ukingoni sasa wewe uko points sawa na yule mwenye kikosi kibovu halafu unasema hastahili kuwa bingwa niseme tu haya ni matumizi mabaya ya akili. Lol.

Mkisema Yanga atapoteza sijui atapata sare nyie hamuwezi kupoteza na kupata sare?

#Amkeni usingizini acheni kupumbazwa na kauli za yule Roporopo wenu.
 
Halafu wao ndio wa kwanza kusema tuna ndoto za alinacha na wakati wanashindwa kufikiria logic kama hii.
 
Halafu wao ndio wa kwanza kusema tuna ndoto za alinacha na wakati wanashindwa kufikiria logic kama hii.
Kiukweli tu mpaka sasa wakisema kwamba ubingwa Yanga haezi kuchukua ni sawa wanajidanganya tu sababu mpaka sasa hamna kinachowapa 100% kwamba wao watakuwa mabingwa wakati kuna mechi kibao mpaka ligi imalizike.

Kuwa makundi Champions League sio tiketi ya kuwa mabingwa wa VPL hili inapaswa walijue pia.
 
Hawa jamaa akili zao wengi ni fyatu. Wameshinda dhidi ya Vita wanapata mawenge wanaona wanaweza kushinda kila mechi EPL.

Wanasahau kuna baba yao Yanga, kuna mdogo wao Azam ambaye kawatoa kamasi juzi kati hapo na pia wapo mpaka vilembwekeza na wanasumbua sana. Sijui wao wanajikuta nani!!
 
Inabidi wajitafakari aisee.

Upo muda wa kutamba tena hapo wanatakiwa wawe na asilimia kubwa ya Ubingwa ila sio sasa ambapo mpaka sasa ni 50 kwa 50.
 
Inabidi wajitafakari aisee.

Upo muda wa kutamba tena wakiwa na asilimia kubwa ya Ubingwa ila sio sasa ambapo mpaka sasa ni 50 kwa 50.
Kweli kabisa. Upo wakati sahihi kuanza kujivuna na kupiga vijembe kwa wapinzani lakini siyo sasa wakati league ikiwa bado mbichi na kuna za ya mechi 15 bado hazijacheZwa.

Simba foolish kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…