Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Asante kwa kunifumbua macho. Mimi nilijua ni kejeli na dharau tu au kwa kuwa kanda mbili zina dharaulika.
 
Aaaah nlikuwa nachukia kwel nkisikia neno kandambili, kumbe ndo hvo safi mkuu
Wala huna haja ya kuchukia, hilo jina linabeba historia nyingi ambazo hata hao wanaolitumia kuikashifu Yanga hawajui kwamba wanaitukuza kupitia kwalo: (1) Yanga ni timu ya Watanzania wote. Kwenye makundi yote hayo ya Kandambili na Raizoni kulikuwa na watu wa kila rika, kila tabaka, kila amali, kila fani na kila kabila. (2) Yanga si timu ya mchezo. Hapendwi mtu, awe kiongozi, mchezaji, mwanachama ama mshabiki, tajiri au masikini, mnyonge au mwenye nguvu. Kinachopendwa ni misingi iliyowekwa, ikiongozwa na 'Daima Mbele ..... ' Kama ingekuwa ni timu ya kunyenyekea wenye pesa, umaarufu au umahiri uwanjani, basi akina Mangara Tabu, Shiraz Sharif, Sunday Manara, Jella Mtagwa na wengineo walioanzisha Pan African wasingeondoka Yanga na kuwaachia watu ambao hata kutamka Young Africans hawakumuda vizuri; wakaita kwa urahisi wao tu wa kutamka :Yanga. Angalia wenzetu wanavyoendelea kuteseka hadi kufikia kuitwa 'mbumbumbu' na bado kiongozi aliyewaita hivyo anadumu mpaka anapokataa mwenyewe kuongoza. Au mchezaji anapokuwa mfalme mpaka anapanda ndege peke yake huku wenzake wakitapikiana kwenye boti. (3) Hakuna mkubwa kuliko Yanga ndani ya Yanga (4) Yanga ilikuwapo, ipo na itakuwapo. (4) Wanaosema Yanga hailei bali inaua vipaji hawaijui Yanga, hawajui historia ya mpira wa nchi hii na huenda hawajijui wao wenyewe. Kuibua vipaji siyo kunyakua wachezaji wanaojulikana tayari kwa uchezaji wao unaojulikana tayari kwenye madaraja yanayojulikana tayari, ili wacheze Uhai Cup. Asilimia kubwa ya wachezaji walioondoka na Yanga Raizoni walitokana na malezi ya kocha aliyemtangulia Tambwe, Mromania Profesa Victor Stansleascu. Huyu alichukua watoto wadogo aliyowaita Yanga Kids (kwa sababu walikuwa kweli ni kids) na kuwaendeleza hata kama hakukuwa na mashindano mahsusi kwa wachezaji wa rika hilo. Hiyo ndiyo hasa inayoweza kuitwa akademi. Baada ya miaka kadhaa ndio taratibu wakachukua nafasi za akina Muhiddin Fadhil na Elias Micheal golini, Hassan Gobos, Abdulrahman Juma (Mapafu ya Mbwa) na Kitwana Manara (Popat) ndani ya uwanja. Hao ndio akina Juma Mensah (ama Pondamali), Jaffar Abdulrahman, Mohammed Rishad (Adolf), Mohammed Yahya (Tostoa), Mohammed Mkweche nk ambao Taifa linawatumia hadi leo. Anayebisha anitajie kizazi gani cha wachezaji walioendelezwa tangu wadogo kinachofikia mafanikio haya. (5) Yanga haikuanza miaka hii kuchukua makocha mahiri kutoka nje. Huyo Prof. Victor ni Mromania, Tambwe Leya ni Mzaire (sasa DRC), nk. Ni baadaye sana ndio akina Nabi Kamara walikuja kuifundisha Simba kutoka Ghana. (6) Wanaosema Yanga imeshindwa kujenga uwanja miaka yote hiyo, hawajui Yanga ni ipi na Uwanja ni nini. Ni sawa na mtu aliye chini ya kivuli cha mwembe uliozeeka na kudai mwenye shamba hajawahi kupanda miti ya kudumu. Wakati unafunguliwa, Uwanja wa Kaunda ulikuwa unazidiwa na Taifa na Karume pekee kwa ubora hapo Dar. Ndio maana ukathubutu kupewa jina la kiongozi shupavu kama huyo. Wanafikiri ungekuwa uwanja uchwara, Mwalimu angekubali upewe jina la rafiki yake? Au hawazijui siasa za nchi hii zama zile? Huo ndio uwanja aliopenya Mzee Mangara alipokosewa bakora na Yanga Kandambili! Kwamba haujaendelezwa sikatai, ila hilo ni swala jengine. (7) ... Nitaendelea siku nyengine nikitakiwankufanya hivyo. Hayo yote yamefutikwa kwenye historia isiyoeleweka ya jina la Kandambili! Wasiojua watambue!
 
tofauti na matarajio ya mashabiki wengi wa nyau sc; dar es salaam young africans tunashinda mechi ya leo na kuwakata ngebe wamatopeni

"karibuni tena katika episode nyingine ya show ya kampa kampa tena"

hii ndo yanga.....daima mbele nyuma mwiko!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…