Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

sio kweli kuwa yanga ni timu ya magamba. ila magamba ndo wanataka kuitumia kama ngazi ya kujirudishia umaarufu uliotoweka.

cha msingi ni wanayanga wote kusimama kidete na kuwakatalia wanamagamba kuitumia chama yao kama njia ya kujipa umaarufu wa kisasa.

yanga wakiliachia hili liendelee watapoteza umaarufu wao kama magamba walivyopoteza umaarufu wao
 
kweli timu yangu ni yanga na ni ukweli usiopingika kwamba yanga ilianzishwa na taa+tanu=ccm miaka hiyo ili kurahisisha mchakato wa kupata uhuru.

mimi naichukia ccm ya sasa kuliko na ikizingatia kuwa ccm ilihodhi mali zote zilizokuwa chini yao kabla ya vyama vingi ilihali wameshidwa kuwahodhio wanachama wote waliokuwa nao.
my take nitaipenda yanga daima nitaendelea kuivaa jezi ya yanga,south africa na brazil bila kujali kwamba inafanana na magamba.

na katika kitu kitawawia vigumu ccm ni kujidanganya kwamba wanaweza kuidibiti yanga kwa miaka hii wakidhani hii ni yanga ya kina kitwana kondo.
 
Hata mimi nilifatilia historia ya yanga ilitokana na chama cha magamba TAA-TANU-CCM....wakati wa harakati za uhuru Tanu waliitumia sana Yanga kuhamasisha mshikamano na umoja ndio maana Rangi asili za Yanga zilifanana na Bendera ya Tanu .i.e

ZAMANI Yanga ilitumia rangi Tatu rangi ya kwanza njano,ya pili Kijani na tatu Nyeusi...kama ilivyokuwa Bendera ya Tanganyika enzi hizo! Rangi blue kwenye bendera ilikuja baada ya kuzaliwa Tanzania.

Hivyo rangi za Tanganyika/Yanga ni Njano=Madini na maliasili, Kijani=Mimea na misitu,Nyeusi=Watanganyika! hii ndio historia ya kweli ya Yanga Kijani na Njano zilikuja kutumika sana ilipokuja Sunderland=Simba!

Kumalizia ni kwamba Yanga ilitumika hivyo tu zamani hizo na si kwamba wana yanga wote ni Magamba! NDIO MAANA Yule fisadi PAPA mmoja jiitu ni Simba na wala si Magamba!
 
Hata mimi nilifatilia historia ya yanga ilitokana na chama cha magamba TAA-TANU-CCM....wakati wa harakati za uhuru Tanu waliitumia sana Yanga kuhamasisha mshikamano na umoja ndio maana Rangi asili za Yanga zilifanana na Bendera ya Tanu .i.e

ZAMANI Yanga ilitumia rangi Tatu rangi ya kwanza njano,ya pili Kijani na tatu Nyeusi...kama ilivyokuwa Bendera ya Tanganyika enzi hizo! Rangi blue kwenye bendera ilikuja baada ya kuzaliwa Tanzania.

Hivyo rangi za Tanganyika/Yanga ni Njano=Madini na maliasili, Kijani=Mimea na misitu, Nyeusi=Watanganyika! hii ndio historia ya kweli ya Yanga Kijani na Njano zilikuja kutumika sana ilipokuja Sunderland=Simba.

Kumalizia ni kwamba Yanga ilitumika hivyo tu zamani hizo na si kwamba wana yanga wote ni Magamba! NDIO MAANA Yule fisadi PAPA mmoja jiitu ni Simba na bado ni Magamba.
 
Nimekuwa shabiki wa yanga tangu nikiwa mtoto, enzi hizo za redio ya kijiji, mkulima.
Nimeanza kuichukia tangu nilipogundua kuwa ni timu ya MAGAMBA. Hili halina ubishi.

Niko tayari kupambana na mpenda Yanga yeyote bila kujali ni nani

Wewe acha kuficha hisia zako wewe ni Simba damu
 
Nenda kashangilie simba timu ya warabu.

Ushangiliaji wa YANGA.....Hongereni!!

264656_131090303642985_100002260494106_233629_8120326_s.jpg
 
[h=3][/h]

Jana ilikuwa raha sana wanazi wa Simba kimyaaaaaaaaaa
 
Yani aibu sana...sijui lini tutapata viongozi wa wajibikaji......masihara masihara kila sector....hata michezo hatuna mipango madhubuti.Si shangai kwa lililotokea......
 
Nimekuwa shabiki wa yanga tangu nikiwa mtoto, enzi hizo za redio ya kijiji, mkulima.
Nimeanza kuichukia tangu nilipogundua kuwa ni timu ya MAGAMBA. Hili halina ubishi.

Niko tayari kupambana na mpenda Yanga yeyote bila kujali ni nani

Wewe ni mwanachama? Kadi namba...... So unahamia timu gani sasa? Mtibwa.... Azam au maji maji? Kuwa wazi otherwise umetumwa weye tena waonekana mnazi wa timu ya waarabu AKA Wapakatwaji
 
Pengine kama si huduma ya kwanza jana ingekuwa kichekesho kikubwa
wakati mabingwa wa kombe la kagame wakifika kupokea kombe wah wa tanesco walikata umeme wao
na baada ya hapo zilitokea busara za gari l a ambulance la huduma ya kwanza kuwasha taa ili kombe lisiibiwe namashabiki wa simba ambao baada ya umeme kukatika wengine walisogelea kama vile wanasikilizia kinachoendelea huku wakila timing
polen watani wangu ila aibu kubwa kwa serikali yetu rais akiwa na umati wa watu huk sudan na perdiem za nguvu watanzania wanaumia kukosa umeme

Florian kaijage walimuwajibisha kwa kudai alikuwa mzembe wakati wa mechi ya stars na morocco , sasa mechi ya jana ndio imekuwa aibu kubwa kwa tanzania maana watu wengi wa mataifa mbalimbali waliangalia sasa atafutwe mzembe aliesababisha aibu ile awajibishwe,tunajua tanesco imeshakufa bado kuzikwa kama anavyosema mzee Renatus mkinga pale wa kulaumiwa ni TFF kwa kushindwa kuwa na generator ya ziada(backup) wakijua umeme tanzania muda mwingi hukatikakatika mawazo yao wakiweka katika pesa ya viingilio

Ingawa hatujui tatizo la jana ni shida ya kawaida ya tanesco kama tulivyozoea au kulikuwa na watu wa simba ndani ya tanesco waliosababisha na kweli ilikuwa bado kidogo wakate kabla mpira haujamalizika ili warudie mechi baada ya kuona simba hawawezi kurudisha bao kwavile mkuu ni yanga ndio maana waliokuwa na njama wakaogopa!!
 
Hata kama ni timu ya chama,mimi naipenda yanga kama club,i dont wana knw what is behind,ukimchunguza sana kuku hutakula nyama yake..
 
Florian kaijage walimuwajibisha kwa kudai alikuwa mzembe wakati wa mechi ya stars na morocco , sasa mechi ya jana ndio imekuwa aibu kubwa kwa tanzania maana watu wengi wa mataifa mbalimbali waliangalia sasa atafutwe mzembe aliesababisha aibu ile awajibishwe,tunajua tanesco imeshakufa bado kuzikwa kama anavyosema mzee Renatus mkinga pale wa kulaumiwa ni TFF kwa kushindwa kuwa na generator ya ziada(backup) wakijua umeme tanzania muda mwingi hukatikakatika mawazo yao wakiweka katika pesa ya viingilio

Ingawa hatujui tatizo la jana ni shida ya kawaida ya tanesco kama tulivyozoea au kulikuwa na watu wa simba ndani ya tanesco waliosababisha na kweli ilikuwa bado kidogo wakate kabla mpira haujamalizika ili warudie mechi baada ya kuona simba hawawezi kurudisha bao kwavile mkuu ni yanga ndio maana waliokuwa na njama wakaogopa!!

Mpaka lini hizi aibu jamani!!!!, Haswa ikijulikana kuwa Super Sport ya Africa Kusini walikuwa wanatangaza Afrika na dunia nzima, Jamani mbona aibu, kama wewe ni mtanzania uko nje unashangilia mara Buuuup, Giza nene, nakwambia watamani kuingia chini ya Meza!!
 
Yanga siwapendi kwa sababu moja tu, CCM.

Si unajua ccm wanavyojua kuchakachua? Yanga ndio ilianza na rangi zake CCM kwa kujua Yanga inapendwa na wengu wakazichakachua!!!
Ila na nyie SImba mmezidi mno kujiregea khaa! kidogo tu chali!?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom