Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

tetesi za chini chini timu ya yanga leo hawajafanya mazoezi kisa ni ukwasi wa pesa uliopo kambini kiasi cha kuomba mechi ya hisani na timu ya mawenzi market ya Morogoro
ingawa mechi hiyo ipo katika mpango wa mkutano wa dini (dhehebu mojawapo hapo Morogoro ambao wanakawaida ya kufanya tamasha kila mwaka
 
Kubwa kuliko Imeisha? [emoji23][emoji23][emoji23]
tetesi za chini chini timu ya yanga leo hawajafanya mazoezi kisa ni ukwasi wa pesa uliopo kambini kiasi cha kuomba mechi ya hisani na timu ya mawenzi market ya Morogoro
ingawa mechi hiyo ipo katika mpango wa mkutano wa dini (dhehebu mojawapo hapo Morogoro ambao wanakawaida ya kufanya tamasha kila mwaka
 
Sawa kumbe na wewe una msimamo wako... ndio maana
Nakukumbusha kuwa simba alienda robo fainal na Vita club alirudi nyumbani.. (bisha tena)

Mnatuchafulia Uzi wa Yanga, habari za mikia mkajadili kwenye Uzi wenu
 
AHSANTENI SANA GSM, KWA DHAMIRA YA DHATI KUELEKEA WIKI YA WANANCHI.

Gari hili maalumu lenye screen kubwa pande zote likiwa katika hatua za mwisho 'branding' ili kuanza amsha amsha kuelekea wiki ya Mwananchi.

Wakazi wa Pwani, Morogoro na Dar kaeni tayari kupokea matangazo haya, mtawashuhudia wasanii mbalimbali na watu maarufu wakileta hamasa huku mkiangalia matukio ya kukonga moyo yahusuyo Yanga yetu katika screen hizo kubwa. .

Usipange kukosa

NDIO MAAANA TUNASEMA. . FUNGA KAZI KUSANYA KIJIJI.
FB_IMG_1564090131940.jpg
FB_IMG_1564090118215.jpg
 
kesho YANGA na mawenzi market uwanja wa jamuhuri Morogoro saa kumi jioni kiingilio bure
 
RATIBA RASMI YA KUSANYA KIJIJI*

1. *Jumatatu *29/07/2019*
Viwanja vya Ikulu Bagamoyo Mjini Mkabala na Nyumbani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Msafara utapokelewa na Wanachama wa Bagamoyo eneo la Mapinga saa tatu asubuhi kwa maandamano kuelekea Bagamoyo.

2. *Jumanne 30/07/2019*
*Viwanja vya Sabasaba (Kiwanja cha Ndege) Morogoro Mjini*
Mapokezi yatakuwa saa tatu asubuhi kupitia njia ya Old Dar es Salaam Road hadi njia panda ya Bigwa kuelekea Kilakala na kuingia njia ya Kichangani hadi Mji Mpya kuelekea Nunge kupitia daraja la Mwere hadi round about ya Posta na Round about ya Stand ya daladala. Msafara utaelekea Msamvu kuelekea Chamwino hadi Mafiga na kutokea Sua Road hadi round about ya Sua na kumalizia kukusanya Kijiji katika katika Kiwanja cha ndege - Sabasaba.

3. *Jumatano*
*31/07/2019*
Chalinze Mjini Nyuma ya Polisi.
Mapokezi yataanzia Mdaula saa tatu asubuhi kwa msafara hadi Chalinze viwanja vilivyopo nyuma ya Kituo cha Polisi Chalinze.

4. *Alhamis 01/08/2019*
Mlandizi mjini
Msafara utapokelewa Ruvu Darajani hadi viwanja vya wazi Mlandizi.

5. *Ijumaa*
*02/08/2019*
Kibaha Maili Moja
Msafara utapokelewa kwa Kibaha kwa Mathias kupitia Picha ya Ndege hadi Stand ya Mabasi Kibaha Maili moja (Kibaha Container)

6. *Jumamosi*
*03/08/2019*
Kigamboni Uwanja wa Swala Tuamoyo.

Msafara utapoelewa Darajani Kurasini kuelekea Viwanja vya Swala Tuamoyo. *UTARATIBU WA KUIPOKEA TIMU KWA MAANDAMANO IKIWA INATOKEA MOROGORO UMEANDALIWA KWA KUSINDINDIKIZWA NA WANAYANGA WA MOROGORO NA KUPOKELEWA KWA WATU WA MKOA WA PWANI KABLA YA TIMU KUKABIDHIWA KWA WANADARES SALAAM KWA MAANDAMANO AMBAYO YAMEANDALIWA KIUNADHIFU NA KISASA KABISA* *DEO MUTTA*
*KATIBU WA HAMASA*
 
Back
Top Bottom