Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190731_093538.jpg
 
20190731_094036.jpg


YANGA Tawi la nguvu ya Buku lenye makazi yake Mwananyamala leo wamekabidhi rasmi msaada wa ukarabati wa Wodi ya Wanaume no.5 waliokuwa wakifanya kwa takribani wiki moja kuelekea kilele cha siku ya Wananchi inatarajiwa kuadhimishwa na Klabu ya Yanga Jumapili ya Agosti 4,2019.

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya makabidhiano Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura aliwapongeza Wanayanga tawi la Nguvu ya Buku kwa fikra za msaada walioufikiria na fundisho tosha kwa wengine.

Alisema Wambura, msaada wa kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa Historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja.Leo mmefanya Tawi la Nguvu ya Buku tunaomba wajitokeze na wengine.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano Mwananyamala ambako Tawi hilo linapatikana aliwapongeza sana Tawi la Nguvu ya Buku kwa kitendo cha Kijamii walichokifanya na hakika yeye kama mpezi wa upande wa pili wamejifunza kitu ambacho kinastahili kuigwa na Mwananchi yeyote anayejitambua.

Nae Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha aliwapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano huohuo siku zote.

Mwisho Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Iyagala alisema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu. cc. @ikulu_mawasiliano @ummymwalimu
 
Tanga nako hawakuwa nyuma. Wiki ya Wananchi. Tawi la CHUMBAGENI hilo nao walifanya yao.


20190731_101714.jpg

20190731_101702.jpg



20190731_101614.jpg
 
Mashabiki wa Timu ya wananchi kila kona wako na furaha tu na Wiki yao ya Wananchi.

20190731_103307.jpg
20190731_103240.jpg



20190731_103253.jpg

20190731_103228.jpg


20190731_103217.jpg
 
hii gym ya hapa uwanja wa jamhuri Morogoro watapata tb hawa sio kwa vumbi hilo
 
Back
Top Bottom