Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread


SIRI YA KIATU CHA MORRISON

Kwenye Mechi ya Watani wa Jadi Mshambuliaji Benard Morrison alicheza kwa dakika takribani 56 tu katika mchezo dhidi ya Simba ambao aliifungia Yanga bao muhimu lililowafanya watoke kifua mbele ka ushindi wa bao 1-0

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael baada ya mchezo alibainisha kuwa Morrison aliumia mazoezini siku mbili kabla ya mchezo na ndio maana alimtoa mapema tu kwenye kipindi cha pili kwani hakuwa fiti

Lakini siri moja kubwa ni kuwa mapema wiki iliyopita Morrison alitembelewa nchini na mkewe akiwa pamoja na mtoto wake.

Walimletea zawadi ya viatu ambavyo alivitumia kwenye mchezo wa jana.

Bao lake alilofunga kwenye mchezo huo tena akiwa na viatu hivyo alivyozawadiwa na 'wife', lilipeleka furaha sio tu kwa Wanayanga bali hata kwa familia yake.

Morrison amebainisha kuwa viatu hivyo atavitumia katika mechi maalum tu "Vilikuwa viatu Maalum kwa kazi maalum Namshukuru Mungu nimeimaliza kazi salama".
Shadeeya ukishasikia "viatu maalum kwa kazi maalum" ujue ndie aliyekabidhiwa mikoba ya ndumba, na kweli ilifanya kazi
 
20200311_085249.jpg
@YangaSc
 
TFF TENDENI HAKI LINDENI WACHEZAJI WENU WA TAIFA STARS

Mbunge wa Chalinze ambaye ni Mwanachama wa klabu ya Yanga Ridhiwani Kikwete amelitaka shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulinda wachezaji kwa kutenda haki na kuhakikisha sheria 17 za mpira wa miguu zinazingatiwa.

Ridhiwani ametoa maoni yake kufuatia tukio la Clatous Chama wa Simba kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Yanga Feisal Salum kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ameitaka TFF ichukue hatua bila ya kusubiri malalamiko kutoka kwa klabu ya Yanga.

Ikumbukwe tukio kama hilo lilifanywa na beki wa Simba Paschal Wawa dhidi ya Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

Hata hivyo TFF haikumchukulia hatua yoyote Wawa licha ya kuonekana dhahiri akimkayaga Nchimbi kwa makusudi "Na hili nalo ⁦‪TFF mnataka ⁦‪Yanga waje kulalamika? Lindeni Wachezaji wa timu ya taifa. Ninyi ndiyo wasimamizi wa mpira Tanzania. Tendeni haki kama kauli mbiu inavyosema ' Our Game Is Fairplay', Be fair," aliandika Ridhiwani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Juzi Chama aliomba radhi kwa tukio hilo lisilo la kiungwana alilomfanyia Fei Toto.
20200311_091541.jpg

Wadau wamempongeza Chama kwa kuwa muungwana lakini bado TFF ina nafasi yake ya kuchukua hatua ili kuhakikisha matukio haya hayaendelei kujitokeza.

@Yangadaima
 
Back
Top Bottom