Mmh!! We unaefuatilia hayo mambo yaani uache kabisa kuleta huu umbea huku jf. [emoji1787][emoji1787]
Au umeshawahi hata kugusia hii kitu humu.
Mwaka 2010, Azam FC ilimtaka Mrisho Ngassa, kipenzi cha Yanga na mashabiki wao.
Zikatumwa barua mfululizo za kuulizia bei na kuomba vikao vya majadiliano na viongozi wa Yanga.
Mwenyekiti alikuwa mwanasheria nguli, Imani Madega. Akasema kama mnataka kuongea na sisi, basi kikao kifanyike Serena Hotel. Akaambiwa panga siku na muda.
Siku ikafika na Madega hakutaka majadiliano marefu, akasema kama mnamtaka Ngassa toeni dola 40,000. Wakati huo uhamisho wa wachezaji ulikuwa hauzidi dola 5000!
Hapo hapo akatumwa mtu aende kuchukua hizo hela. Kumbe watu walijindaa kweli kweli...walikuja na dola laki 5 kwenye gari, zikabaki nje zinapumua tu...dola 40,000 kitu gani?
Madega kusikia hivyo akasema hapana jamani, msizilete...Yanga wataniua, ngojeni kwanza nikaongee na wenzangu.
Kumbe wao walipanga kutaja hela nyingi ili kukatisha tamaa, na walijiandaa kukataa kuombana heri.
Siku mbili baadaye, Ngassa akatua Chamazi.
KWANINI HAIENDELEI?
Moja ya sababu ya Azam kuacha ubabe wa usajili kwa Simba na Yanga ni kauli ya Zakaria Hans Pope (RIP) aliyoitoa pale Millennium Tower Basement baada ya Azam kupita na Ramadhan Singano mwaka 2015.
'Tunanunua bidhaa za Azam, wanapata pesa halafu wanatuchukulia wachezaji wetu. Kuanzia sasa nawaagiza mashabiki wa Simba wasinunue bidhaa yoyote ya Azam'.
Hii haikuwa kauli ya kiushindani wa mpira bali ya makasiriko na hasira zikizotokana na kukata tamaa.
Mwaka 2014, ubabe mwingine ulifanyika kwa usajili wa Frank Domayo, tena akiwa kambi ya timu ya taifa, Tukuyu Mbeya.
Hili suala liliwatingisha Yanga hadi mamlaka za soka nchini na Rais Malinzi akaunda tume ya kuchunguza usajili huo.
Ilikuwa kawaida kwa Simba na Yanga kusajili wachezaji wakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa, na hata Yanga walifanya hivyo kwa Domayo...lakini kwa Azam ikawa tabu, hadi mamlaka zinaingilia.
Ikaonekana kuendelea kushindana na watu wa aina hii kwenye usajili, siyo uungwana. Bora kuhangaika na usajili kutoka sehemu nyingine kabisa.
Kama ni kutoka Simba au Yanga basi kwa wachezaji ambao wenyewe hawana mipango nao.
Lakini kwa hizi kauli zako bwana mdogo @alikamwe, watu watajifikiria upya.
Azam maana yake ni KUBWA KULIKO ZOTE...tusije kulaumiana!
Naitwa Zaka!