Young Bilionea wa Madini wa Arusha Afariki Dunia

Young Bilionea wa Madini wa Arusha Afariki Dunia

Ndo mtambue kuwa kifo huwa kipo, wote wale unaofanya nao chochote kile kila mtu anakufa kivyake
 
Ngoja ni-google kama huyu marehemu alishawahi kufahamiana na Lulu
 
Like seriusly tajiri mkubwa eti lemutuz duh,hizi blogu kweli uchwara
 

Attachments

  • 1434913064356.jpg
    1434913064356.jpg
    66.1 KB · Views: 582
Si hydary huyo. .marehemu mwanae hydary kavira wa mwananyamala hao na marehemu mitkasi yao kuwasafisha makorongwee wa kilami na madini feki. ..hydary kasimama kipakee ila Jimmy haikuwa kivile kipesa kawaida sana,instagramically alikuwa tajiri wa picha mnato alizokuwa anaweka. .. sema alikuwa mtu smart na pesa ya kulipia bills. .
Umejitaidi kuelekea kwenye ukweli bwana mdogo lakini umeboronga mwishoni,..ngoja nikupe siri, No research, No Right to speak... Bado naendelea kuwackiliza bdae nitamaliza mjadala huu kwa kuwapa ukweli wa mambo, maana wengi wenu mnaonekana hamuwafahamu hawa wa2 vizuri
 

Umejitaidi kuelekea kwenye ukweli bwana mdogo lakini umeboronga mwishoni,..ngoja nikupe siri, No research, No Right to speak... Bado naendelea kuwackiliza bdae nitamaliza mjadala huu kwa kuwapa ukweli wa mambo, maana wengi wenu mnaonekana hamuwafahamu hawa wa2 vizuri
Mzee unakuwa kama huijui jamii forums. Humu wamejaa wapuuzi tu ambao anaanza kumuelezea mtu ambaye hajawahi kumuona au kumsikia maishani mwake. Kuna vichwa vimejaa wadudu humu balaa
 
Hii ni mahususi kwa wale wote ambao walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumjua 'Jimmy Mcmelle' ni mtu wa aina gani, maana nimepitia Comment nyingi za watu huku wengi wao wanaonekana wanafuata mkumbo na kuckia habari za chini ya Carpet.

Jimmy Mcmelle ni kijana wa pekee katika familia ya Mzee Mcmelle aliyefariki miaka mingi iliyopita, Kwa ufupi malezi yake ameyapata kutoka kwa mama yake anayeitwa 'Jane Mcmelle' ambaye nae ni mjasiriamali na mpambanaji hapa mjini.

Jimmy pamoja na Hydery wamejuana kipindi wanasoma shule japokuwa Hydery Kavira alikuwa yupo kidato cha mbele zaidi ya huyu mwenzake.

Baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2009 katika shule ya sekondari ya Green Acre, Akaanza kujihusisha na biashara za madini kama alizokuwa akifanya baba yake enzi za uhai wake, ndipo hapo ukaribu wake na Hydery ulipoanza kushika kasi japokuwa kipindi hicho Hydery alikuwa amekwisha anza kuivaa katika hayo mambo.

Siwezi kusema kwa asilimia zote kwamba biashara zao za madini walizokuwa wakifanya zilikuwa ni halali au sio lakini nachofahamu walikuwa wanapiga hizo ishu(Ya Ngoswe muachie Ngoswe).

Kwa ufupi hali ya kimaisha ya kwa kina Jimmy haikuwa mbaya, tunaweza kusema hela ya kubadilisha mboga ilikuwa haiwapigi chenga, hasa ni kutokana na baba yake kuiacha familia yake katika hali nzuri. Kipindi hicho baba yake alikuwa anamiliki MaVx na magari ya thamani ya juu kbs.

Basi katika harakati za kupambana, Upepo wa pesa ukaanza kumvumia Jimmy ambapo nakumbuka baadhi ya gari yake ya mwanzo kuanza kumiliki kabla ya hizi Foreign Cars ni pamoja na Verossa moja nyeusi.

Unapoona mafanikio ya Marehemu Jimmy, nyuma yake kuna mtu amehusika kwa asilimia kubwa ambaye ni Hydery Kavira ambaye urafiki wao ulivuka mipaka mpk watu kujua ni ndugu wa damu, tofauti na watu wengine wanaosema Jimmy amerithi pesa za urithi.

Wanasema Mungu amtupi Mja wake. Katika kipindi chote cha mafanikio Jimmy alikuwa yupo bega kwa bega na mama yake, ambapo alifanikiwa kumnunulia Nissan Murano na yeye mwenyewe kuweza kununua BMW ya Blue na Mercedes Benz ambayo imemletea umauti.

Wasanii na watu wengi maarufu wamemjua Jimmy kupitia Hydery Kavira ambaye alikuwa anasifika kwa kula bata la kibabe na kutoka na totoz wazuri kama vile Mheshimiwa pamoja Penny sambamba na kutoa ofa za kibabe pindi anapokuwa kwenye kumbi za starehe.

Hapo ndipo Jina la Jimmy lilianza kusikika mjini plus mitandaoni kama vile Instagram ambapo alikuwa akipost picha akiwa amejiachia sehemu expensive akila bata na watu wake na hivyo kupelekea kushobokewa na totoz wanaopenda bata hapa mjini.

Miongoni mwa Totoz hizo ni pamoja na Diva wa Clouds Fm, Jokate,Wema, Lulu ambaye alifikia mpk hatua ya kucomment kwenye picha zake, Esha Buheti ndio usiseme na wengine kibao..Kwa ufupi this dude was living a life.

Chanzo cha kifo chake kimezungumziwa na watu wengi, lakini kwa uchunguzi mdogo niliofanya, mpendwa wetu Jimmy alipatwa na ajali katika eneo la Mbuyuni njia panda ya kwenda Kunduchi mishale ya saa 8 usiku ambapo inasemekana alikuwa ametoka kumrudisha rafiki yake huku wengi wao wakidai alikuwa yupo tungi.

Kwa jinsi navyoifahamu njia panda ya mbuyuni pale ni sawa na machinjioni, watu wengi wamekuwa wakipata ajali za kutatanisha huku watembea kwa miguu wakigongwa na kupoteza maisha. Kwa ufpi sio sehemu nzuri hata ya kucmama mwenyewe mchana. Ni Neema zake Mungu ndio zinazotuokoa

Inasemekana Lori lilokuwa likitokea Tegeta lilishuka na kumgonga kwa kishindo ambapo licha ya airbag kutoka kila upande lakini haikuweza kuokoa maisha ya mpendwa wetu Jimmy ambaye alikuwa yupo ndani ya gari lake la kifahari aina ya Mercedes Benz na kumpelekea kuumia maeneo ya tumboni.

Nakumbuka maneno ya mwisho aliyosema Jimmy ni kuwa, magari yake mawili aliyokuwa akimiliki ambayo ni Benz pamoja na BMW yanamtosha na hana mpango wa kununua gari lingine tena kwa sasa.

Binafsi kifo chake kimenigusa sana hasa ukizingatia ni kijana mwenzangu na ameondoka katika kipindi ambacho alikuwa anahitaji sana kwa namna moja ama nyingine.

Baadhi ya watu wanaweza wanafikiri huenda kifo chake kimesababishwa na Pombe, wengine mara ametolewa kafara na wengine ni kula majasho ya wa, lakini hakuna mwenye uhakika kuhusu hili, wakuhukumu ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kama mdau wa Jamii Forums sio mbaya ukachukua walau dakika moja kumuombea Ndugu yetu Jimmy Mcmelle huko alipo. Ningependa kuwaclisha uzi wangu huu, kama kuna sehemu utakuwa na mapungufu mtaniwia radhi.

Wale wataalam wakuCOPY na kuPASTE wote mnakaribishwa lakini msisahau kutaja ni wapi mlipotoa huu Uzi. Kwa Heri Ya Kuonana My Nigga Jimmy Mcmelle...tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi
 
Back
Top Bottom