Mkuu muanzisha post, sipendi kukuita muongo, wala mkatisha tamaa naomba nikuite mtu usie na taarifa sahihi kuhusu YouTube.
Najiuliza hiyo miaka 10 ulikua unafanyia YouTube gani.kama ni kweli umefanya miaka 10 ukiwa na elimu kubwa ambayo si sahihi kama hii ulioandika hapa nakubaliana nawe kua YouTube 'HAIKULIPI'
1.Youtube haiangalii lugha unayotumia ili kukulipa,chanzo kikubwa cha mapato ni matangazo, na yotube wanapokea matagazo ya lugha zote hata kiswahili,hivyo content cretor ukiwa unapata watazamaji wa kiswahili, youtube wataweka matangazo ya aina hiyo na utaingiza hela vema kabisa.
Ishu ya lugha inazingatiwa kutokana na kwamba CPM za mataifa yanayoongea kiingereza ni kubwa, kwani content zao huangaliwa dunia nzima, hivyo YouTube wanaweka tangazo kubwa kwenye video ya Youtuber wakijua litaangaliwa na watu wa mataifa mbalimbali, hivyo na creator anapata hela nzuri.
Tanzania ukipata watazamaji 1000 walioona tangazo unalipwa kuanzia $0.80 mpaka $1
Wakati marekani ukipata watazamaji 1000 unaweza pata dola 8 mpaka 15. Na hizi CPM huwa zinabadilika deile, leo inapanda kesho inashuka.
Unaweza kuwa na content ya kiswahili alafu ukapata watazamaji waliopo marekani (mfano diaspora wanaotoka kenya,Tz na nchi zinazoelewa kiswahili) unapiga hela nzuri tu
Ndio maana sasa hivi marekani wanatukata kodi, kwenye hela uliyoingiza kupitia watazamaji walio ndani ya marekani, bila kujali wewe ni youtuber ulie nje ya marekani.
NB:sio kila mtazamaji ataona tangazo,hivyo video inaweza kuwa na watazamaji laki moja alafu wakaona tangazo elfu 30 mpaka 50
Nimefanya Youtube kwa miaka mitano na ninaingiza hela nzuri tu kwa mwezi, ambayo hata sina mpango wa kuajiriwa.
Elimu ya youtube ipo mtandaoni, pitia soma, kama kuna eneo nimedanganya niambie nikupe proof.
YOUTUBE INALIPA NA BADO KUNA FURSA NZURI KWA WATU KUJIAJIRI.
ASANTE
Yeah nakubaliana na wewe hata mimi nilikua namiliki channel YouTube kwa kupindi flani lakini kwa sasa nimeacha ila nina uelewa wa mambo mengi ,jamaa kuna vitu anachanganya eti ukitumia kiswahili unalipwa hela ndogo hapana sio kweli
Haijalishi unatumia lugha gani,what matters is the audience wanaotazama video zako
Nchi kama Marekani na bara la ulaya audience yake ina thamani kuliko audience ya Africa na sababu kubwa ni kwamba makampuni ya Ulaya yanalipa pesa nyingi kwa Google kwa ajili ya matangazo yao tofauti na Kampuni za Africa
Ngoja nifafanue kidogo kwa wasio elewa,iko hivi yale matangazo unayoyaona YouTube ni ya makampuni tofauti duniani kwa mfano Coca-Cola,Apple,Pesi,Mcdonalds na nyinginezo sasa hayo makampuni ndo yanawalipa Google pesa ili watangaze
Kwahyo Google wanachokifanya ni baadhi ya matangazo wanayapeleka YouTube na hao wanaomiliki YouTube ndo wanaweka yale matangazo kwenye channel tofauti za watu ambazo zimekidhi vigezo.
Ndo maana ukifungua video ya millard ayo unaweza ukakutana na tangazo la Cocacola ambalo limewekwa na YouTube kutokea Google.
So kwa njia rahisi ni Cocacola wamelipa pesa ya matangazo kwa Google na Google watalipeleka YouTube,likifika YouTube linapelekwa kwenye channel ya millard ayo
Kwahiyo hapo kila mmoja anapata mgao wake.
Na kama nilivyosema hapo awali makampuni ya Ulaya yanalipa pesa nzuri ya matangazo tofauti na Kampuni za Africa kwahyo watazamaji walioko ulaya wana thamani kuliko Africa na ninaposema thamani namaanisha mchango wao kwa view
Hivyo basi YouTube hela ipo lakini ukitaka kupata pesa nyingi zaidi inabidi uwe na audience ya ulaya na ili uipate inabidi uwe na content ambazo hata mtu wa ulaya anaweza kuangalia
Nitatoa mifano miwili
Mfano wa kwanza mtu mwenye channel ya mpira anayepost habari za michezo,na highlights za ligi kuu za ulaya kama Epl,la liga,Uefa,europa nk atapata international audience yani watu kutoka kila pembe ya dunia wataangalia videos zake na hivyo atapiga hela
Mfano wa pili ni mtu mwenye channel ya mpira anayepost ligi kuu ya bongo tu,huyu atapata local audience tu yani watu wanaofatilia channel yake ni watanzania tu tena wachache,Mtu wa ulaya hawezi kuhangaika na ligi ya bongo tena aangalie Timu kama namungo[emoji23](jokes)
Kwahyo mtu anayepost vitu international atapata audience kubwa na hela nyingi pia
Ningeendelea ila dah nimechoka kutype