Yoweri Museveni awapa makavu wadau wa maendeleo katika mkutano wa IDA mjini Nairobi

5 April 2024

MH. JUMANNE KISHIMBA (MBUNGE NA MFANYABIASHARA MKUBWA) KATIKA MAONGEZI : UCHUMI NI MATUMIZI PART 2


View: https://m.youtube.com/watch?v=oiiHH-pgamEMfuatilie Mheshimiwa Mbunge Jumanne Kishimba akieleza umuhimu wa matumizi ambayo yanaweza kuufanya Uchumi uwepo, usimame au usiwepo na ufe.

Shida ya vijana kukosa ajira nini tufanye kama nchi ? Ni vyuo vikuu kukosa kuunganisha masomo na mahitaji ya mazingira nje ya chuo hivyo ni muhimu vyuo na wizara ya uwekezaji kufanya kazi hiyo.

Miaka inakwenda wanafunzi waanzie wapi? Sisi tuna mitaji ya mamilioni tunapeleka mamia ya ngombe zetu tunalala ktk vitanda vya double decker lakini mwanafunzi wa chuo kikuu hajui kubana matumizi kutokana na ubongo wake kuchakachuliwa na ustaarabu kuwa hawapaswi tena kulala ktk kitanda cha double decker.

Waliomaliza elimu ya vyuo vikuu wanapoanza maisha kutokana na mshahara hivyo hawataweze ku 'save' wawekeze ktk biashara inayoleta mapato endelevu badala ya kukabiliana kununua usingizi kwa mikopo ya nyumba au mkopo wa gari ili aishi ilivyopandikizwa chuoni kuwa wao ni watu special..

Wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu hawarudi nyumbani au vijijini hivyo miji ya wazee wao ambayo ni mitaji kama mashamba na mifugo inakufa hivyo familia zinakosa muendelezo wa maendeleo ya kiuchumi yaliyoanzishwa miaka mingi.. mfano jamii yetu ya kihindi hawakati mnyororo ulioanzishwa na wazazi wao tofauti nasi wamatumbi ambao tunaukata mnyororo wa utajiri walioanzisha mababu zetu ktk mashamba, mifugo, uvuvi n.k

Kombinashe nyingi ikiwemo masomo ya dini, kichina na mitaala mipya isiyo endana na mazingira yetu n.k mbunge Jumanne Kishimba anasema imesahaulika dini kubwa za kienyeji ambazo zina watu wengi kuliko ukristo au uislamu.

Kwanini imani hii ya kienyeji yenye mambo mazuri zimepuuzwa ktk ngazi za shule za sekondari na elimu ya juu na kubwa mila za wenyeji ambazo zinasisitiza utaratibu wa maisha kama tabia njema, kutoa ahadi za kuaminika, kutekeleza ahadi, kujaliana n.k

Tunakopi sana mambo ya wageni na kusababisha gharama kubwa za ustaarabu wa kigeni na kupelekea maisha kuwa magumu, pesa kutohifadhika kwa kuwa hatuna mipango ya matumizi na kukua uchumi kwa kiasi kikubwa ni kudhibiti matumizi ...

Hakuna ukomo wa uwekezaji hivyo kila mmoja asiwekeze ktk usingizi yaani nyumba ya anasa ya gharama kubwa au gari bali katika mtaji wa biashara ya kuingiza mapato anasisitiza mbunge Jumanne Kishimba ... na hii elimu ya vyuoni na shuleni ni elimu ya zamani sana na haiendi na kasi ya mabadiliko ya ulimwengu tulionao...

Rasilimali, teknolojia na wingi wa watu ...

Source : sociology tanzania
 
Bagamoyo, hututendei haki,
Nafahamu una uwezo mkubwa sana wa kutupasha ambacho Musukuma na Kishimba wameongea , kwa njia ya maandishi kama ulivyotuwekea kwa Museveni,

Sasa kutuwekea Video na uwezo wetu mdogo wa bando, naona sio sahihi.

Naomba ufikilie hilo sana.
 
MABADILIKO MAKUBWA NA JAMII
Mabadiliko katika Jamii na vichocheo kwanini mbadiliko yanatokea na jinsi ya kujitayarisha kukabiliana nayo. Na hivyo mwana sociolojia ndiyo kazi yake kutafsiri hayo na kuisaidia jamii iweze kujinasua.

Kutoka ujima hadi uchumi wa kilimo na kisha mapinduzi ya kiviwanda, na kutoka vijijini kukimbilia mijini ..... na suala la bidhaa bandia aliloliona Karl Polanyi kuwa ardhi, kazi na fedha siyo vitu halisi bali ni mazingaombwe hivyo utajiri halisi ni ..... na ukitazama listi ya watu tajiri zaidi duniani kuanzia namba 1 hadi 3 kwa mfano mdogo rahisi hutaona ardhi, ajira ya cheo kikubwa au pesa ndiyo imewafanya kuwa matajiri bali information / habari-mawasiliano Microsoft n.k

Sasa basi kadri nchi za kiAfrika zinavyokurupuka bila kutafakari kutoka hatua ya ujima kukimbilia usasa ndivyo tunajichongea kujiweka ktk hatua hatarishi anasema Ulrich Beck mwana sociolijia mjerumani, hivyo inatupasa kufikiri zaidi ktk maamuzi ..... mfano ukosevu wa mkubwa wa ajira Afrika ni kutokana na nchi zetu kukurupuka katika zama hizi za mabadiliko makubwa tusiyoyajua vizuri ....mchambuzi na mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii mwana sociolojia Bw. Bituro Paschal Kazeri anatufafanulia tulipo.

4 January 2024

THE GREAT TRANSFORMATIONS AND SOCIOLOGY

View: https://m.youtube.com/watch?v=umKH8iypKeoSociology rose out of the effects of the GREAT transformations which took place in the 18th and 19th centuries. Early and subsequent sociologists attempted to to understand and explain social phenomena which emerged due to the transformations. The transformation nature of the society is ongoing meaning sociologists should match with it ..

Source : Sociology Tanzania
 
Hayo yapo wazi ila je, wazawa wenyewe ni wagunduzi? Kma wasomi ni kutoa maoni mbona wao hawana hizo startups?

Haya madude yuto ni trash hayana msingi , hao wasomi wameajiriwa nje kuongea tu na kjipa vyeo ambavyo havina maana.. Maprofessors wote hawana mitazamo ya ubunifu kazi kukalia vyeo tu.
 
Hayo yapo wazi ila je, wazawa wenyewe ni wagunduzi?

Tatizo tumekuwa taifa la kupenda njia za mkato nchi imejaa wachuuzi, machinga, maafisa usafiri hatuzalishi chochote nchini kuongeza thamani tunaagiza bajaj, pikipiki, mafuta ya kula, nguo n.k huku hakuna viwanda vya kuongeza thamani kwa bidhaa tunazozalisha nchini tunawapelekea nje bidhaa ghafi mfano pamba kisha tunatumia dola fedha za kigeni kununua mitumba ya marehemu toka ulaya na Canada...
 
BENKI KUU YA TANZANIA, TUNA AKIBA KUBWA YA KUTOSHA KUAGIZA BIDHAA NA HUDUMA TOKA NJE

Aug 22, 2023
Jumanne, Agosti 22, 2023

Benki kuu ya Tanzania BoT imesema akiba ya fedha za Kigeni hadi jana ilikuwa Dola za Marekani bilioni 5.41 ambacho kinatosha kuagiza bidhaa za nje kwa miezi minne na siku 27.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema akiba ya fedha za Kigeni hadi jana ilikuwa Dola za Marekani bilioni 5.41; kiasi ambacho kinatosha kuagiza bidhaa za nje kwa miezi minne na siku 27.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 22, 2023; Mkurugenzi Utafiti na Sera wa benki hiyo, Suleiman Misango, amesema upungufu uliopo sasa wa fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.

Tangu vita vya Ukraine (Machi 2022 hadi Agosti 21, 2023), BoT imeuza Dola 5.18.5 milioni katika soko la fedha na kuanzia Julai Mosi hadi jana BoT ilikuwa imeuza zaidi ya Dola milioni 100 ikiwa ni ongezeko kubwa kuliko zaidi ya Dola milioni 62 zilizouzwa Julai hadi Septemba 2022.

Juni 8, 2023; Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba alinukuliwa akisema hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa zinaifanya Tanzania kuwa salama dhidi ya changamoto ya upungufu wa sarafu za kigeni ulioathiri nchi nyingi.

Miongoni mwa mataifa yaliyoathirika na upungufu wa dola ni Ghana, Misri, Zimbabwe, Nigeria na Kenya, ambayo baadhi yanafikiria kuweka kando matumizi ya dola katika biashara zake.

Hivi karibuni wakati wa mdahalo wa wadau wa sekta binafsi barani Afrika uliofanyika jijini Nairobi, Rais wa Kenya, William Ruto alitoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwa na mfumo wao wa malipo na kuweka kando matumizi ya dola.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Tutuba alisema licha ya akiba ya fedha za kigeni kupungua nchini, hakuna changamoto hadi sasa.

Alisema Tanzania kila siku inauza hadi wastani wa dola milioni mbili, kiwango ambacho hakifikiwi na nchi yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Hadi Mei, mwaka huu, Tanzania ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni ya Dola bilioni 4.88 zinazotosha kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi minne na nusu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita
 
Julius Nyerere katika hotuba yake kuhusu kanisa na Theolojia ya Ukombozi katika Amerika ya Kusini akiwa nchini Managua, Nicaragua. Hotuba yake hii ya mwaka 1988 inaigusa Tanzania ya 2023 kuhusu masuala yanayoendelea ya maeneo ya ardhi ambayo viongozi watawala wachache wameamua kwa siri kupewa milele kwa wageni.


JULIUS NYERERE Former President of Tanzania Speech in Nicaragua in 1988


 
Raisi wetu na February na Yule Waziri wetu wa 1st grade digiri ya uchumi walipata Shule ya kutokukimbilia kutoa kazi zetu Kwa watu wa nje ??? Na Zana Za Kilimo Yule jamaaa wa Kigoma mwenye kurandana nao.

Kwa maana nyingine M7 Sera zake zimepita kulekule alikopita Yule kiongozi aliyeongoza Tz Kwa Awamu 1
 

Nimeona nyuso za tahayari na uwoga kutoka kwa February na waziri 1st Class ya Uchumi waliposikia mtiririko wa nondo za M7 kuhusu kuwakumbatia wadau wa maendeleo wasiotaka kuona nchi ikiendelea kwa sera zisizo za mashiko maendeleo kuweza kupatika na kujitegemea.
 
By Engineer Noel K. Ngowi : HOW THE QUEST FOR INDUSTRIALISATION CAN BE ACHIEVED IN AFRICA

2019 4 January
TECHNOLOGIES ARE THE ARTS - Is a book written for the purpose of changing the Mindset of African intellectuals to be practical oriented rather than to major in narrations OUR MOTTO IS : SCIENCE IS ABOUT KNOWING BUT TECHNOLOGIES ARE ABOUT DOING.


View: https://m.youtube.com/watch?v=NfuM3gq0zjs
 

Friday, May 21, 2021​

WAZIRI WA KILIMO AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA JUU YA “KUTUMIA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA KILIMO KULETA MAENDELEO SHIRIKISHI TANZANIA”​



Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza umuhimu wa kuongeza tija ya Kilimo wakati akifungua warsha ya kitaifa iliyofanyika Jijini Dodoma juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 21 Mei 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)


Sehemu ya Washiriki wa warsha ya kitaifa iliyofanyika Jijini Dodoma juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda wakati wa ufunguzi, tarehe 21 Mei 2021.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam/Taaluma Prof Bonaventure Rutinwa akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda kwa ajili ya ufunguzi wa warsha ya kitaifa iliyofanyika Jijini Dodoma juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 21 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza umuhimu wa kuongeza tija ya Kilimo wakati akifungua warsha ya kitaifa iliyofanyika Jijini Dodoma juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 21 Mei 2021.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es salam Dkt Ronald Ndesanjo akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa iliyofanyika Jijini Dodoma juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 21 Mei 2021.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Tanzania inatambua umuhimu wa wakulima wote nchini – yaani wakulima wadogo, wa saizi ya kati na wakubwa - katika mageuzi ya kilimo na kuendeleza mbinu za kisasa na kilimo cha kibiashara chenye tija zaidi na faida kubwa kwao.

Mkakati wa Sekta ya Kilimo (ASDS I na ASDS II) na Programu ya kuendeleza Kilimo (ASDP I na ASDP II) imelenga kukuza kilimo kwa ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi ili kuleta matumizi endelevu ya ardhi na maji, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, huduma za utafiti na ughani, upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo, masoko na uchakataji wa mazao ili kuongeza thamani za mauzo ya nje (value addition).

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma tarehe 21 Mei 2021 wakati akifungua warsha ya kitaifa juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kulingana na sera zetu za kilimo wawekezaji wakubwa wanategemewa sio tu kuzingatia haya katika kilimo chao wenyewe bali pia kusaidia wakulima wadogo – outgrowers na wakulima wengine - kwa kuwakopesha mbegu bora na pembejeo, kutoa elimu, ushauri na huduma za ughani kwa ujumla na kuingia mikataba mizuri ya kununua mazao yao” Amekaririwa Mhe Mkenda

Amesema kuwa Wakulima wakubwa wanategemewa pia kuchangia katika kuongeza thamani ya mazao na uboreshaji wa mnyororo wa thamani, na hivyo kuongeza bei za bidhaa za kilimo tunazouza nje ya nchi.

Amesema kuwa kunapokuwa na wawekezaji wakubwa na wa saizi ya kati ambao wengi wao huchukua maeneo makubwa ya ardhi, mojawapo ya majukumu ya serikali ni kulinda haki za raia na kuhakikisha ardhi yao na maji haviporwi, na pia wanalipwa fidia stahiki na bei nzuri kwa mazao yao.

Waziri Mkenda amesema kuwa Zaidi ya asilimia sabini (70%) ya watanzania wanaishi vijijini ambako wanajishughulisha na kilimo, kilimo huchangia 26% hivi ya pato la taifa na asili mia thelathini (30%) ya mauzo ya nje (exports). “Lakini kwa miaka mingi tumejitahidi kuinua ubora wa kilimo kwa mafanikio japo si makubwa sana, kutokana na ujuzi mdogo wa wakulima wetu na matumizi hafifu ya sayansi na teknolojia ya kilimo, na hivyo tumeendelea kuwa na tija ndogo sana (low agricultural productivity) na upotevu wa mavuno” Amesema

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam/Taaluma Prof Bonaventure Rutinwa amesema kuwa Warsha hiyo ni kilele cha Utafiti wa mwaka mmoja uliofanywa na taasisi ya taaluma za maendeleo ya Chuo Kikuu cha dar es salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya Bill&Melinda Gates ikiwa na lengo la namna ya kutumia fursa za uwekezaji mkubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo Dkt Ronald Ndesanjo amesema kuwa radi huo wa utafiti ni sehemu ya majukumu ya taasisi hiyo ambapo ulikuwa na malengo makubwa mawili ikiwa ni pamoja na kufahamu kiwango cha ujumuishi katika ngazi ya miradi ya Uwekezaji wa kilimo chini ya Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Pia amesema lengo la pili ilikuwa ni kubuni namna bora ya kubadilisha mabadiliko jumuishi ya kilimo katika ngazi za uwekezaji pamoja na ngazi ya sera.

MWISHO
 
Uchimbaji madini ya chuma na viwanda vyenye ujuzi wa ufuaji Tanzania vyatakiwa kupewa kipaumbele pamoja na miundo mbinu ya kuifikisha kwa wingi viwandani

09 MAY 2024
Kigamboni, Dar es Salaam
Tanzania

RAIS SAMIA HASSAN AAGIZA MADINI YA CHUMA CHA TANZANIA YATUMIKE KUUNDA VIPURI


View: https://m.youtube.com/watch?v=2inFOGsta5oWaziri wa Viwanda na Biashara ametakiwa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji katika Mradi wa Liganga na Mchuchuma ili nchi iweze kuzalisha chuma kitakachotumiwa kwenye viwanda na kutengeneza vipuri vya magari.

Maagizo hayo yametolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha magari makubwa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam chenye uwezo wa kuunganisha magari 270 kwa mwezi.

Tanzania : Newly Launched Dar Truck Assembly Plant to Generate Over 2,000 Jobs. President Samia Suluhu Hassan has launched the Saturn Corporation Limited Company's truck assembly plant in Dar es Salaam. The project is expected to generate about 2,050 job opportunities
 
Kwanini hawatumii kiswahili kama tulivyo kubaliana kipindi cha Magufuli??
 
16 MAY 2024
Nairobi, Kenya
MASHIRIKIANO BAINA YA NCHI JIRANI KATIKA BIASHARA KUNYANYUA CHUMI ZA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI


Ziara ya kiserikali ya rais Yoweri Kaguta Museveni nchini Kenya

View: https://m.youtube.com/watch?v=Yd4uxaaJkX0
Baada ya nchi za kiafrika kupata uhuru takribani miaka 60 iliyopita kuna kitu nchi za kiafrika hazikuzingatia ili nchi zao pamoja na raia kwa ujumla kupata kuneemeka kwani toka nchi za Afrika zipate uhuru tulidhani misaada ya wanaoitwa wadau wa maendeleo wangesaidia nchi zetu kuneemeka.

Kuanzia mwaka 1980 baada ya miaka 20 toka uhuru ndiyo kukabainika soko uhuru miongoni mwa nchi za kiafrika ndiyo moja ya nyenzo muhimu kuneemesha uchumi wa nchi zetu pamoja na raia kutajirika tofauti na hivi sasa kufanya biashara na nchi za nje ya bara la Afrika ambao wanatoa bei ndogo.

Mfano nchini Uganda kulikuwa na makelele mchele wa Tanzania upigwe marufuku kwa vile mbali wa mchele wa Tanzania ni mtamu na wa ubora mzuri kuliko wetu wa Uganda ambao ni bei ya juu pia hauna utamu na ubora kama wa Tanzania, hivyo mimi nikakataa kusiikiliza kelele za wakulima wa mpunga wavivu wa Uganda wasioweza kulima mpunga unaoweza kushindana na ule mzuri wa Tanzania.

Unaweza kuwa na nchi ikawa na uchumi mzuri lakini kiusalama ni petevu, mfano enzi za miaka ya 1930 -1945 nchi za Ubelgiji, Ufaransa zilikuwa na uchumi ulioneemeka lakini dhaifu kiusalama hivyo Ujerumani ya Hitler iliweza kuzivamia na kuzivuruga.

Hivyo kwa nchi za Afrika Mashariki mbali ya agenda ya kukuza uchumi pia uende sambamba na usalama wa nchi zetu za EAC ama sivyo uchumi wetu unaweza kuendelea lakini tukaangushwa na matatizo ya kiusalama kutoka nje ya bara letu....

Ziara hiyo ya siku tatu ya mheshimiwa rais Yoweri Museveni wa Uganda nchini Kenya imekuja siku moja baada ya kumalizika kwa Kikao cha Pili cha Tume ya Pamoja ya Mawaziri (JMC) kati ya Uganda na Kenya kilichomalizika jana jijini Kampala.

Wakati wa JMC, mataifa yote mawili yalijitolea kuhakikisha utekelezaji wa haraka na kamili wa maamuzi yaliyofikiwa wakati wa vikao vya mikutano mingine ya nchi mbili...
 
Hotuba ya mheshimiwa rais Dr. William S. Ruto wa Jamhuri ya Kenya wakati wa ziara ya kiserikali ya rais Museveni nchini Kenya,


View: https://m.youtube.com/watch?v=AWHamXN0pLs

Rais William Ruto alisema Kikao cha 2 cha Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri(JMC) kilichofanyika kuanzia Mei 12 hadi 14 2024, Kampala, Uganda, kilifikia kilele kwa kutiwa saini kwa hati saba za mashirikiano.

Rais alisema Kenya na Uganda zimeunganishwa kithabiti na uhusiano uliokita mizizi katika historia ya pamoja, utamaduni, na matarajio ya amani na ustawi wa kikanda.


Nchi hizo mbili zilitia saini Mkataba wa Makubaliano ili kuimarisha ushirikiano katika taasisi za Huduma za Kigeni ambao unahakikisha kubadilishana maarifa na kuoanisha miundo na maudhui ya mafunzo ya kidiplomasia. Hii inahusu pia sasa kuhakikishiwa Uganda kuunga mkono nia ya Raila Odinga wa Kenya anayewania nafasi ya uongozi katika secretariati ya kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Rais alisema kuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usimamizi na Maendeleo ya Utumishi wa Umma utaimarisha utoaji wa huduma kati ya mataifa hayo mawili.

"Pamoja na hayo, Mkataba wa kuwezesha ushirikiano katika masuala ya vijana umetiwa saini, ambao unatuwezesha kuongeza uwezo wa kundi letu la vijana ambao ndiyo wengi katiks idadi ya watu kwa kuzilazimu nchi hizi mbili kutekeleza sera na programu Ubunifu za kitaifa zinazohusu vijana," alisema. .

Rais alisema JMC ilishuhudia utiaji saini Mkataba wa ushirikiano katika michezo unaoonyesha uzito wa nchi zote mbili katika kukuza na kuendeleza michezo na uhamasishaji wa uwekezaji unaofungua fursa ya sekta hiyo.

Alisema MoU imekuja wakati muafaka huku nchi hizo zikiweka msingi wa kuandaa kwa pamoja makala ya AFCON 2027 ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushirikiano wa utatu wa pamoja baina ya Kenya, Tanzania na Uganda.

Ruto alisema nchi hizo mbili zina chombo cha kuongoza ushirikiano wa kimkakati katika elimu, mafunzo, na utafiti wa kisayansi, pamoja na MOUs katika sekta ya biashara ndogo na za kati, na usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Alisema Mkataba wa tatu wa Uagizaji na Usafirishaji wa Bidhaa za Petroli zinazo safirishwa kupitia Kenya hadi Uganda unaiwezesha Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda kuagiza bidhaa za petroli iliyosafishwa moja kwa moja kutoka kwa chanzo cha mamlaka ya wazalishaji cha nje ya Afrika ya Mashariki.


Ruto alisema hatua hiyo iliyogusa sekta ya usafirishaji nishati ya mafuta inamaliza changamoto zinazokabili sekta hiyo Nchini Uganda. Pia bomba la mafuta kutoka Eldoret Kenya hadi Kampala Uganda litawezesha mafuta kusafirishwa moja kwa moja kupitia bomba la mafuta toka bandari ya Mombasa Kenya hadi Kampala Uganda.

"Tuna imani kwamba vyombo hivi vitaimarisha uhusiano wetu dhabiti na kuuweka kwenye mkondo wa kuleta mabadiliko. Kama viongozi, tumejitolea kutekeleza majukumu yetu yote ili kufaidika kikamilifu," alisema.

Rais alisema kuwa mawaziri wa biashara kutoka nchi zote mbili wameagizwa kukutana na kutatua vikwazo vyovyote vya kibiashara na masuala mengine yanayoathiri biashara.

Ruto alizungumza hayo leo jijini Nairobi alipokutana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye yupo katika ziara yake ya kiserikali nchini Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…