Ndivyo walivyo mawakili,amechukua mpunga wake na kumetulia.
Suala la Amsterdam nalitizama kwa jicho jingine na naona kuna faida ilipatikana kwa kelele zake.Kwa chuki iliyokuwepo dhidi ya Lissu naamini waliokuwa na nia ovu walitishwa na kauli za Amsterdam na angalau wakawa na uoga. Uhusika wa Amsterdam ulionyesha kuwa dunia inafuatilia.
Katika chaguzi hizi za kwetu kuna funzo ambalo wote (washindi na washindwa) tunatakiwa tulijue na kulitilia maanani nalo ni kuwa nchi za magharibi hazina rafiki wa kudumu bali zina rafiki maslahi.
Kwa yaliyotokea Uganda na ukanyagaji wa demokrasia kwa kiwango kile usingetegemea hata balozi mmoja wa magharibi ahudhurie kuapishwa Museveni.Vyama vya upinzani viwekeze kwa wananchi wao na ushirika wao na Magharibi uwe ushirika wa mashaka.