Half London
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 261
- 112
Habari wana Jamiiforums?
Leo nimeisikia ile nyimbo ya kipindi cha Watoto Show Radio One, nikamkumbuka yule mtoto aliyeiimba.
Wanaojua yuko wapi na anafanya nini kwa sasa atujuze. Ni hayo tu!
"Watotoo wasafi moyoni ni nyota za macho za wazazi, sisi ni maua tulioopendwa na Mungu mwenyezi"
======
Semboko said;
Utashangaa kwamba aliyeimba rekodi "Watoto (1986)" ni binti wa kihindi anaitwa Nipa alikuwa na miaka 6 wakati huo.Varda Arts ni wasanii wa kihindi ambao waliishi mkoani na kuhamia Dar baadaye.Kazi yao kubwa ilikuwa ni kupiga picha na baadaye wakageuzia muziki.Walitoa rekodi kama "Tazama Tanzania (1986"),"Maridadi Sana (1984)" na "Mwl Nyerere (1984)".Walikuwa wasanii wa kwanza kwanza kutoa swahili movie iitwayo "Maridadi".Waliwahi kushirikishwa kwenye All Stars Orchestra iliyotengenezwa na BASATA wakati huo kuimba katika charity balls mbali mbali Tanzania aidha za CCM au Serikali wakisindikizwa na wanamuziki wengine wazalendo.Kwa hesabu za haraka haraka Nipa atakuwa mtu mzima sana sasa!
Aliyeimba "Tanzania eeh" song anaitwa Martina Chambiri na hii ilikuwa katika tamasha la kimataifa la watoto huko Italy maarufu kama Zecchino d'Oro.Watanzania wengi hawakufahamu nyimbo ile mpaka presenters maarufu wa Radio One (Master T na Mike Mhagama) wakati ule walipomleta studio na kuzungumza naye na toka hapo wimbo ukawa maarufu sana.Binti sasa yuko chuo kikuu na anafanya vizuri sana,ila bahati mbaya baba yake mzazi alifariki dunia akiwa bado sekondari.