Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Atakuwa kishakuwa mtu mzima sanaumetisha daa huyo mdosi sijui yuko wapi sasa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Atakuwa kishakuwa mtu mzima sanaumetisha daa huyo mdosi sijui yuko wapi sasa.
Mwenye video ya Pain in Me by Emmanuel Nkulila yupo beach na mrembo aiweke hapa link yake.
aliyeimba mbuga za wanyama nadhani anaitwa martina chambili, ni giza sio muhindi
nenda u tube andika hilo jina na jina la wimbo ni tanzania-e
Atoke UK akufuate wewe na kijinsi chako kisa album? Kwa akili yako albam imewahi kumtoa nani bongo hii tangu imeZaliwa! Acha kumchuria binti wa watu wewe
Utashangaa kwamba aliyeimba rekodi "Watoto (1986)" ni binti wa kihindi anaitwa Nipa alikuwa na miaka 6 wakati huo.Varda Arts ni wasanii wa kihindi ambao waliishi mkoani na kuhamia Dar baadaye.Kazi yao kubwa ilikuwa ni kupiga picha na baadaye wakageuzia muziki.Walitoa rekodi kama "Tazama Tanzania (1986"),"Maridadi Sana (1984)" na "Mwl Nyerere (1984)".Walikuwa wasanii wa kwanza kwanza kutoa swahili movie iitwayo "Maridadi".Waliwahi kushirikishwa kwenye All Stars Orchestra iliyotengenezwa na BASATA wakati huo kuimba katika charity balls mbali mbali Tanzania aidha za CCM au Serikali wakisindikizwa na wanamuziki wengine wazalendo.Kwa hesabu za haraka haraka Nipa atakuwa mtu mzima sana sasa!
Aliyeimba "Tanzania eeh" song anaitwa Martina Chambiri na hii ilikuwa katika tamasha la kimataifa la watoto huko Italy maarufu kama Zecchino d'Oro.Watanzania wengi hawakufahamu nyimbo ile mpaka presenters maarufu wa Radio One (Master T na Mike Mhagama) wakati ule walipomleta studio na kuzungumza naye na toka hapo wimbo ukawa maarufu sana.Binti sasa yuko chuo kikuu na anafanya vizuri sana,ila bahati mbaya baba yake mzazi alifariki dunia akiwa bado sekondari.
nakumbuka enzi hizo jumamosi ikifika bila kwenda itv/redio one ilikuwa ni shida nyumbani.
Kuna siku tumetoka studio, nikatumia nauli yote ikabidi tutembee kwa miguu hadi home.
Utoto jamani, nikiahidiwa kwenda studio basi ntakuwa a good girl wiki nzima
Kichuna,Amina Chifupa alianza hivyo hivyo,mwisho "akafundishwa" utangazaji na akina Mike Mhagama na Deo Mshigeni,baadaye akaupata ubunge.Mungu amrehemu alikuwa mbunge matata sana na shukrani ziwaendee waliomfanya awe maarufu.Kutembea kwako kwa miguu basi wewe ulikuwa unakaa Mlimani,Mwenge,Kijitoonyama au Sinza maana ni sehemu hizo tu ni karibu na Mikocheni,lol.
"Watotoo wasafi moyoni ni nyota za macho za wazazi, sisi ni maua tulioopendwa na Mungu mwenyezi"
(niekee beat kwanza)
Yap mi ndo mdosi...hujambo lkn shemNdo wewe ulieimba nini??
Yap mi ndo mdosi...hujambo lkn shem
Sijambo, mambo niaje??
Yule alikuwa mtoto wa Kihindi, sijui hata alipotelea wapi.
"Watotoo wasafi moyoni ni nyota za macho za wazazi, sisi ni maua tulioopendwa na Mungu mwenyezi"
(niekee beat kwanza)