Yuko wapi aliyeimba wimbo wa Watoto Wasafi moyoni show?

..'Huukasirishwa na wenzao, mara hutembea na hao hao, wakigoombana na wenzao muda si muda huzungumza nao, la la laa..'

Kipindi hicho nasoma mafundisho ya kipaimara. Nimeikumbuka nyimbo ya "Machozi" ya Lady Jay Dee.
 
Habari wana Jamiiforums? Leo nimeisikia ile nyimbo ya kipindi cha Watoto Show Radio One, nikamkumbuka yule mtoto aliyeiimba. Wanaojua yuko wapi na anafanya nini kwa sasa atujuze. Ni hayo tu!

Wanaitwa VARDA Arts walikuwa wana band yao walikuwa wanakaa mitaa ya msasani ukishapita shule ya msasani kama unakwenda slipway, ni wahindi wa mwanzo mwanzo kuishi msasani, pia ndio watu wa kwanza kwanza Kuuza UROJO aka Mix
 

Umechambua vizuri sana! Siku hizi vijana maridadi sana maridadi sana,kuna m-bongo aliyekuwa kwenye hiyo movie ya maridadi alikuwa anahojiwa na Star TV msanii wetu.
 
Last edited by a moderator:
Habari wana Jamiiforums? Leo nimeisikia ile nyimbo ya kipindi cha Watoto Show Radio One, nikamkumbuka yule mtoto aliyeiimba. Wanaojua yuko wapi na anafanya nini kwa sasa atujuze. Ni hayo tu!
Mkuu yupo ni mkubwa sasa anaitwa Melody Mbasa anawimbo mzuri sana unaitwa Nikoleze, anaimba huyo Bella anakaa pembeni.
 
Nadhani ndiye aliyeimba nyimbo ya mbuga za wanyama. Ni nyimbo ya mda mrefu sana,ikitoka kupigwa hiyo nyimbo inapigwa ya Emmanuel Nkulila.

Hahaha ikitoka ya Emmanuel Nkulila inaingia ya Sama Mapangala dunia tunapita kila kitu kitabakia, halafu kisa cha mpemba Twangapepeta kina luiza mbutu wanakata mauno wameshika nyungo
 
Kuna ile pia ya kabinti kanaimba "Tanzania eeh,jela mia,jela mia,sijui na nini,karibu mumuone"

Kuna kabinti keusi kanaimba huku nyuma kuna kwaya ikimsapoti,na mbele kuna kwaya masta akiongoza.

Ilikuwa inapigwa pia wakati wa kipindi cha watoto cha itv.
 
Semboko,Hivi Mike Mhagama sio ndio Marehemu Deo Filikunjombe?
 
Mwny ule wimbo auweke humu tujikumbushe kipindi kile mambo ya kwenda studio radio one
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…