Yuko wapi msanii "Mtunis"?

Yuko wapi msanii "Mtunis"?

nakumbuka alihojiwa kipindi cha nyuma akaulizwa kuhusu maisha akasema ana nyumba kali anajenga lakini pia ni baba wa watoto wawili na ana supermarket mjini dsm hapa.

sema rafudhi yake ilikuwa kama ya watoto wanaosomea IST[emoji23][emoji23][emoji23].
Mzinguaji tu huyo hana nyumba yoyote amerudisha mpira kwa kipa amerudi kwao, kwao ni mbagala charambe magengeni,kutwa nzima anashinda kibarazani anapiga guitar.
 
Huyu msanii jina lake halisi silijui ila alikuwa na heka heka sana enzi hizo. Mara ya mwisho alikuwa anaishi Sinza kwa jimama moja kama marioo na alimfukuza kwake baada ya kufilisi duka alilomuachia.

Huyu msanii alikuwa muongo sana na mjivuni kuna interview yake moja pale Channel Ten alidai yeye alisomea masuala ya utengenezaji wa ndege kule South Africa.

Je huyu msanii yuko wapi kwa sasa au amerudia kazi yake ya uganga wa kienyeji.
Ubishoo wote ule kumbe mganga
 
kuna mmoja pia alikuwa msanii wa bongo muvi mweupe hivi kakaa kiupole sana..
naskia alikuwa anabadili demu kwa siku mara 3 km dozi ya asprini (sorry mzee asprin).
hadi mwenyekiti wa mtaa na balozi waliitwa na mwenyenyumba waje kumuonya!!simkumbuki jina ila uzi wake uko humu niliusoma.

na yule jamaa mwingine jina lake la kitajiri kila guest huko daslam walikuwa hawataki kumkodishia room sbb alikuwa anazichafua kwa majitaka ya mtaroni.
Copy huo uzi then uupaste hapa tuusome [emoji23]
 
Back
Top Bottom