Yuko wapi producer Ambangile Mbwanji maarufu kama Producer Amba?

Yuko wapi producer Ambangile Mbwanji maarufu kama Producer Amba?

Ngushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Posts
9,065
Reaction score
18,358
Wakuu yuko wapi huyu producer amba ambaye kipindi cha nyuma kidogo alikua maarufu sana iringa baadae akaja kuhamia daresalam!
Alitengeneza ngoma za wasanii wengi mfano Album nzima ya Rama D iliyokuwa ina nyimbo kama Kikao cha familia,usihofie, Sara, nk..... Ambao mlibahatika kusikiliza hii album nadhani mtakua mnafahamu vizuri ngoma zilizomo humo ndani japo ilisemakana Rama D hakumlipa hata mia baada ya mauzo ya album(dhamana ilikua uaminifu) na baada ya hapo Rama D hakuwahi kurudi kwenye nafasi yake tena!

Pia alitengeneza ngoma ya Mh. Temba_Maneno nawafunza ukisikiliza hutatilia shaka uwezo wake!
Roho saba-nakupenda hip hop, Man kichefu(huyu nasikia ni mjeda kwasasa)_utanikumbuka....
Na nyingine nyingi za wasanii mbali mbali ambazo wadau mnaomfahamu mnaweza kuongea!

Nafikiri ndie aliyemtengeneza producer Tuddy Thomas ndani ya AB records enzi hizo (ingawa hili sina uhakika nalo sana) ila wamefanya kazi pamoja kipindi hicho Tuddy hajahamia dar....

Karibuni wadau!
Tahadhari:
Wale kizazi cha kina Eyooooo laizzer kaeni mbali na huu uzi
 
Yuko Mwanza bado?
Lini alihamia mwanza? Ninachojua jamaa baba yake alikua mchungaji huko Iringa na mama yake alikua anaenda enda huko ughaibuni na mara ya mwisho nilisikia kama jamaa yupo nje!
Au wewe unachanganya mafaili
 
Subiri usiwe na haraka.
 
Dah huyu bwana alikua fundi sanaaa ukisikiliza zile ngoma mbili za roho saba- Nakupenda Hip hop na Waite Polisi utaona ufundi wa huyu jamaa,

By the way nilikua nawasikia wawili tu Iringa Amba na Tuddy enzi hizo Radio Ebony ndo imeanza anza madogo underground kibao walikua wanatoa ngoma zao hapo nadhani ilikua bure tu
 
Daaa umenikumbusha Waite polisi hili jiwe hatari sana halafu ukisikiliza kwenye earphones Kuna mdundo flani unagonga kwenye sikio moja halafu unaunganisha masikio yote😂😂😂😂 hii ilikua ni pure talent!

Watakaobisha hili la mziki kugonga earphone ya sikio moja halafu unaunganisha masikio yote wasikilize wimbo wa Addo novemba - utabaki kuwa Mungu alitengeneza huyu mwamba!
 
Mtoto wa mchungaji mbwanji..
Yupo iringa anaendeleza mradi wa mama yake wa kufuga kuku akishirikiana yeye mama yake na mdogo wake joshua,
pale nnje kwao kuna duka la mahitaji ya nyumbani yeye kaweka mitungi ya gas,mpesa na tgo pesa..
Kwa sasa bado anajenga nyumba yake sehemu inaitwa changalawe ni umbali wa km 1 kutoka na nyumbani kwao
Gari anayotembelea ni IST number c nyeusi imechoka choka.

Ile nyumba ilipokuwa studio miaka ya zamani ni nyumba ya marehemu mchungaji ngede bado ipo kwa matumizi ya familia..
Ile nyumba imetoa vipaji kama kenani kihongosi alikua mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa iringa nafikiri amaeachia ngazi mwaka huu kwa sada yupo kwenye mbio za mwenge.

Una swali jingine niingie chimbo?
 
Na pia anamiliki bakery yenye kuzalisha mikate yenye chapa ya "Best Bakery"... zamani bakery yake ilikuwa njia ya kuelekea Mkimbizi.. maeneo fulani hivi ndani ndani kidogo.. ila kwa sasa amehamisha bakery yake.

Back
Top Bottom