Yuko Wapi Said Maulid-SMG?

Yuko Wapi Said Maulid-SMG?

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
48,474
Reaction score
125,866
Huyu mchezaji sijamsikia kwa muda mrefu sasa.

Aling'ara sana kipindi cha nyuma kwenye ngazi ya vilabu hapa nchini na hadi kwenye timu yetu ya Taifa(Taifa Stars)

Nakumbuka Taifa Stars iliwahi kucheza na Senegal ikiwa inawania kufuzu mashindano ya Barani Afrika ambapo Taifa Stars ililazwa bao 4-0(endapo nimekosea mnisahihishe) huko ugenini nchini Senegal chini ya Kocha Mbrazil-Macio Maximo.

Said Maulid(SMG) alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi hicho.

Kwa sasa yuko wapi? Bado anasakata kabumbu au kashatundiga ndaluga?

Mwenye habari zake tushare hapa tuweze kujikumbusha umahiri wake japo kidogo.
 
Said Maulid a.k.a SMG alishastaafu soka.

Nafikiri anajiandaa kuwa mchambuzi kama mwenzie Ali Mayai.
 
Said Maulid a.k.a SMG alishastaafu soka.

Nafikiri anajiandaa kuwa mchambuzi kama mwenzie Ali Mayai.
Aisee.

Kitambo sana sijamsikia kumbe kashatundiga ndaluga.

Ila akiwa hata kocha msaidizi kwa kilabu hizi za nyumbani nayo sio haba
 
Mara ya mwisho alisajiriwa na timu ya Ashant United wakati wao ligi kuu nafikiri ilikuwa 2014
 
Eeeee!! baba tena, dah mkuu umenikumbusha mbali sana,

Baba yangu alifariki nikiwa katikati ya mtihani wa NECTA tena ilikuwa soma la GEO (RIP mzee wangu)

asante.
Na ulifeli sio?
 
Kuna kipindi alikuwa anacheza soka Angola sijajua kama amerudi bongo ama kabaki kulekule after maisha ya soka.
 
Back
Top Bottom