Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Huyu mchezaji sijamsikia kwa muda mrefu sasa.
Aling'ara sana kipindi cha nyuma kwenye ngazi ya vilabu hapa nchini na hadi kwenye timu yetu ya Taifa(Taifa Stars)
Nakumbuka Taifa Stars iliwahi kucheza na Senegal ikiwa inawania kufuzu mashindano ya Barani Afrika ambapo Taifa Stars ililazwa bao 4-0(endapo nimekosea mnisahihishe) huko ugenini nchini Senegal chini ya Kocha Mbrazil-Macio Maximo.
Said Maulid(SMG) alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi hicho.
Kwa sasa yuko wapi? Bado anasakata kabumbu au kashatundiga ndaluga?
Mwenye habari zake tushare hapa tuweze kujikumbusha umahiri wake japo kidogo.