Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Hii biashara kufilisika ni dk 0 tu!
Ndomana sumry alingia kwenye
Kilimo

Ova
Na wengi wanaonunua mabasi ni sababu ya mapenzi tu na kuvutiwa na hayo mabasi lakini vision hawana kabisa ndio maana wanapukutika kila leo.....
 
Uzi ttajir Sana huu, heshima kwa wakongwe wote hapa mmeonyesha kwa kina sana kumbukumbu mlizo nazo za enzi hizo hasa Yohanne mbatizaji mimi sikuwa najua bwana Mbowe ana nyota nyingi hivyo kwakweli
Sasa tuleteeni uzi wa mbabe wa kaskazini enzi hizo
Heshima yenu!!
Wababe wa kaskazini wapo wengi
Ngorika
Buffalo
Chakito
Meridian
 
Huyu bwana anaendesha Gari kwa mdogo wa KT Abri waarabu wa iringa, kuna mtu kasema hapo alisababisha ajali ni kweli yeye na marehemu ally kilaweni alikuwa anaendesha basi la Zainabs VOLVO B7, ndio waliisababishia basi ya Shabby ilikuwa inaendeshwa na marehem ROSHI ilipata ajali baada ya mashindano makali pale kona za kukutamisha mkoa wa ruvuma na wilaya ya Njombe, wakati huo sisi Scandanavia tulikuwa tunakuja nyuma pole pole na hiyo ruti nilikuwa nimempokea mzee Okala mzee wa mliyayoyo. Giriki ni halfkast wa kigiriki na kingoni, alipigwa marufuku kabisa kuendesha mabasi na liseni yake alifungiwa miaka 2 na kutangazwa ktk Gazeti la serekali.
Mdau ina maana ulikuta iyo ajali ikiwa ya moto kabisaaa
 
Wababe wa kaskazini wapo wengi
Ngorika
Buffalo
Chakito
Meridian
Kanda hiyo haikuwa na nguli kama Giriki mkuu?
Kwa wakati huo, au ni huyu picha imetumwa juu huko mwenye kidevu cheupe au yule anaita madereva derere 😂
 
dah kweli kitambo... sie tulikuwa madogo kiasi so tulikuwa sana sana tunashabikia.. maana mpira ule zaman wa kihuni sana... yaani mpira kuisha mtu kapasuliwa kitu cha kawaida...

mechi zetu za chandimu tunachezea msisiri uwanja wa msufini karibu na kwa fundikira

enzi hizo watoto wa kina fundikira waliotoka ulaya wazungu wa meli .. wanakuja na wachumba wa kizungu pale mtaani
Daaa umenikumbusha msisiri jioni uwanja wa mpira usiku mama ntilie wanauza msosi
 
Daaa umenikumbusha msisiri jioni uwanja wa mpira usiku mama ntilie wanauza msosi

halafu asubuh tulikuwa tunawahi kuokoteza chenji zilizokuwa zimeanguka usiku na hazikuonekana.. hadi kule kwa chonya na duka la mpemba
 
halafu asubuh tulikuwa tunawahi kuokoteza chenji zilizokuwa zimeanguka usiku na hazikuonekana.. hadi kule kwa chonya na duka la mpemba
Chonya ndo alikuwa diwani wetu enzi hizo nakumbuka kipind cha uchaguzi unakuta ananunua jezi kwa team ya mtaa pale ili ajihakikishie ushindi
 
Giriki yupo anaendesha maroli ya mwarabu mmoja wa mlandizi anaitwa Ahmed motor says safari zake nyingi na za Rwanda Dar
 
Giriki huyu hapa
8817066b5f20a1bbcba4c33c82982ef1.jpg
 
Mara ya mwisho nilipanda basi la Tawaqal nikitokea mkoani Ruvuma lakini kwa sasa ni muda mrefu Tawaqal zimeachana na route hiyo.

Nauliza Wahenga wale wa " Watu wa safari" huyu nguli wa barabarani dereva Giriki yuko wapi siku hizi?

Kazi Iendelee

cc: Bujibuji
Yupo anaendesha tenki siku hizi. Pia niliwahi kusikia ana mwanae anaendesha New Force almaarufu kwa jina la Mwarabu, nae ni mtu wa mwendo kama baba yake
 
Wababe wa kaskazini wapo wengi
Ngorika
Buffalo
Chakito
Meridian
Pia kulikuwa na : Rombo Investment,Kamwanga Line, Loliondo Bus, Dar Express, Salama Star, Fresh ya Shamba,Osaka,Hood,Njuweni(Ya Mzee Mfinanga wa Kibaha), Imamu Express , Machame, Wakongwe wengine wataongeza.
 
Mara ya mwisho nilipanda basi la Tawaqal nikitokea mkoani Ruvuma lakini kwa sasa ni muda mrefu Tawaqal zimeachana na route hiyo.

Nauliza Wahenga wale wa "Watu wa safari" huyu nguli wa barabarani dereva Giriki yuko wapi siku hizi?

Kazi Iendelee

cc: Bujibuji
Mabasi ya Fresh ya shamba yalifia wapi?
 
Hahaha mitaa yangu hiyo
Mzee songambele mzee wangu sana
Haipiti wiki bila kunigusa hewani!
Ila mimi kwangu ni nyuma ya mango,ila nlihama huko nmewachia ----wakae huko[emoji23]
Ila mitaa hiyo ya songambele wazee wengi hapo nlikuwa naelewana nao sana
Kina mzee kumwembe (rip) etc
Huko nkipitaga ni wanted[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Mzee Songambele yule alikuwa mkuu wa mkoa enzi za Nyerere yupo hai? Nilimuona kama miaka 3 iliyopita na niliongea nae ila alikuwa dhaifu kiasi na umri nao Si haba!

Sent from my S20 Ultra using JamiiForums mobile app
 
Nilishawai toka dar saa 12 asubuhi saa 11 jioni nipooo songea yule mwamba alikuwa anaijua njia ya dar to songea balaaaa
 
Back
Top Bottom