Yule mkongwe aliyeteka JF kuhusu Forex sasa kaingia kwenye Cryptocurrency, tusubiri vilio

Yule mkongwe aliyeteka JF kuhusu Forex sasa kaingia kwenye Cryptocurrency, tusubiri vilio

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
kiwa na bahati ya kuhandika na maandiko yako yakawakamata vizuri watu basi utawachota kweli kweli.

Huyu bwana hapa JF aliwakamata watu sana kipindi cha Forex na mpaka wengine hata umweleweshe vipi kukubali kuwa alikuwa akili yake aina 50 zake ilikuwa ngumu.

Hapa JF watu wameweza kueleza Forex ni kama kubeti au kudownload pesa ambayo kuna mawili kama kamali upate au usipate.

Sipigilii nyundo, forex inatumia nguvu kubwa kimatangazo na watu kama mmoja alikuwa hapa JF sasa kakimbilia Twitter kwenye kichwa cha habari. Usipokuwa makini unaweza kusema pesa inakuja haraka kumbe sio kabisa.

Sasa tuje kwenye huyu jamaa kiukweli!.baada ya kuona Forex hana jipya tena kahamia kwenye cryptocurrency.

Cryptocurrency kipindi cha miaka ya juzi imeanza kushika kasi kwa kuwavutia watu sana kwa kuona mafanikio makubwa ya sarafu kama kusikia biticoin 1 sawa usd 0.6 imeweza kufikia usd 36000.kipindi cha miaka michache huko nyuma.

Hapa watanzania ndio tunapokuja kupigwa na tamaa na kuchotwa na hawa vijana.

Sasa hawa vijana baada ya kukosa wafuasi nyanja ya forex wamekimbilia kwenye cryptocurrency .

Siri iliyopo wanayofanya:
Vijana wanachofanya kwenye cryptocurrency ni mtindo ambao yeye ataweza kukueleza mafanikio ya haraka huku akitafuta chain ambayo mtakuwa mkilipa yeye kupata kamishine kutoka kwenye hizo sarafu.

Kamishine zinatoka wapi?

Kuna kampuni nyingi ambazo zinataka wafuasi wa kuboost coin zao au tuseme pyramid system.
Kinachofuata ukiingia na ukilipa yeye anakula pesa yako bila kujua.

Lingine ni kwamba mfumo huu cryptocurrency hata mkidhulumiana au kutuma pesa au kukudhulumu hakuna pa kumshitaki kama hata chukua pesa zenu kwa mtindo cryptocurrency, kwa sababu huwezi kutrace na wala huwezi kujua atapeleka benki gani.
 
mbinu myingine inayotumiwa na watu wa forex/cryptocurrency ni kufanya creative visualisation. wanatumia social media kuonyesha lifestyle yao.

watakuonyesha magari ya gharama wanayoendesha, nguo za gharama wanazovaa, migahawa maarufu wanayoenda kupata lunch/breakfast, prominent figures wanaokutanao nk.

hii yote ni katika namna ya kuwavuta vijana wengine waingie huko na kutepeliwa.
 
Ukiona unaitwa kwenye fursa na nguvu kubwa sana inatumika ujue kabisa wewe ndio fursa

WAJINGA NDIO WALIWAO, na ukienda kichwa kichwa wanakubamiza kweli

Mungu ameagiza tule kwa jasho nyie mmebadilisha mnakula kwa M B za mtandaoni, mnadownload pesa tu shchwaaaaaaa

FURSA YENYEWE NDIO HIYO UKIWAULIZA IMEPATA VIBALI HAPA TANZANIA NA KUSAJILIWA WANAKUWA MKALI MTAGOMBANA SIKU NZIMA

Ukipigwa au kutapeliwa kule ndio imekula kwako kwa kuwa huna sehemu ya kuwashtaki na uthibitisho rasmi sanasana utaishia kupoteza hela kufatilia kesi za hawa SCAMMERS

Najua mtakuja kunisema sijui chochote kuhusu haya mambo ya kuvuna coin, mara sijui wallet ila ndio hivyo mwenzako akinyolewa zako tia maji

Aisee, machawa wa blockchain na crypto msije kunivamia hapa ni mtazamo tu😎

😆
 
Vijana kuna fursa kubwa katika cryptocurrency na kama hujui chochote chukua fursa zilizopo kujifunza ili uone kama itakufaa ama la. Duniani ni kwenda na trend tu. Ukiweka juhudi za kutosha jumlisha na bahati kidogo inawezekana hii ndio ikawa fursa yako ya kutoka.
 
Ukiona unaitwa kwenye fursa na nguvu kubwa sana inatumika ujue kabisa wewe ndio fursa

WAJINGA NDIO WALIWAO, na ukienda kichwa kichwa wanakubamiza kweli

Mungu ameagiza tule kwa jasho nyie mmebadilisha mnakula kwa M B za mtandaoni, mnadownload pesa tu shchwaaaaaaa

FURSA YENYEWE NDIO HIYO UKIWAULIZA IMEPATA VIBALI HAPA TANZANIA NA KUSAJILIWA WANAKUWA MKALI MTAGOMBANA SIKU NZIMA

Ukipigwa au kutapeliwa kule ndio imekula kwako kwa kuwa huna sehemu ya kuwashtaki na uthibitisho rasmi sanasana utaishia kupoteza hela kufatilia kesi za hawa SCAMMERS

Najua mtakuja kunisema sijui chochote kuhusu haya mambo ya kuvuna coin, mara sijui wallet ila ndio hivyo mwenzako akinyolewa zako tia maji

Aisee, machawa wa blockchain na crypto msije kunivamia hapa ni mtazamo tu😎

[emoji38]
maadam umekili hujui chchote endelea kubwata
 
Back
Top Bottom