sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Binafsi sioni tatizo lolote, ni aina ya uwekezaji ambao akifanya mzungu inaonekana sawa ila akifanya mtanzania mwenzetu anaonekana anapitia shortcut, 😂😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa kwa kutunga yuko vyema, anaweza watungia story za South Africa watu wakaamini alikuwa huko kumbe fix, Jamaa kipaji cha kutubga story nampa 100Sielewi vijana huwa wanadanganywa Nini? Baada ya kudondosha kilio humu kaenda kafungua kampuni nyingine kwa mbwembwe seems like capital 360 I think then vijana wakajaa Tena kaacha kilio Hadi post zake na any info kafuta mitandaoni..now kaanza kupost kitu kingine vijana Moto wanajazana .Mimi nadhani Kuna shida kubwa hasa ya saikolojia kwa vijana .huyu bwana kila siku kupost anaishi maisha luxury inawadanganya vijana wengi Sana..
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kuibiwa ni ujinga kwa sababu Forex ni real shida watu ni wavivu sana kutafuta elimu ya ForexAmeshapiga za Forex, deal done mission complete.
chizcom,
Nimekusoma mwanzo hadi mwisho na nimejiridhisha wala huna uelewa wa kutosha kwenye hii mada. Ngoja nikupe mawili matatu. Kwanza ni kweli watu aina ya Ontario walikuwa wanamwaga darasa kwa sababu kuu 2. Sababu ya kwanza wapate watu watakaojiunga na classes zao, na sababu ya pili hao watu wawaunganishe kwa brokers ili hatimae wapate kamisheni!! Na mara nyingi kama sio zote, hawa brokers wanakuwa brokers uchwara ambao hawajaji-establish.
Tukija kwenye crypto, kwanza ni mjinga tu ndie atalipa kusoma crypto class! Forex ina mambo mengi ya kujifunza kulinganisha na crypto. Kikubwa unachotakiwa kufahamu kwenye crypto ni legit exchange markets na jinsi ya ku-point hizi crypto. Na kama ni mgeni kwenye game, kikubwa unaweza tu uka-focus kwenye well established crypto ambazo hazipo kwenye risk ya kutoweka ingawaje kwa wenye mitaji midogo crypto kama hizi zitaishia kukupa hela ya kula tu, lakini kama unahitaji kutusua basi unatakiwa kulenga new crypto ambazo ni very risk kwa sababu, kimsingi crypto haina tofauti na biashara zingine tunazofanya kila leo!! Kama ambavyo watu 100 wanaweza kuanzisha biashara mpya na kwa mara ya kwanza leo, lakini baada ya mwaka 1, huku ni 10 tu kati yao ndio wali-survive, na 90 wote walikata mtaji. Hivyo ndivyo huwa kwa new cryptos. Nyingi huwa zinaingia sokoni lakini ni chache ndizo zina-survive! Sasa kama huku-point sawasawa, unaweza kujikuta vidola vyako 200 uli-invest kwenye new crypto ambayo inakuja kupotea baada ya muda!
It's business. Lakini $200 hiyo hiyo kama uli-invest muda muafaka, na crypto husika ika-survive, amini usiamini pesa ambayo unaweza kuingiza unaweza hata kuona aibu kuichukua. Ngoja nikupe mfanmo wa Shiba Inu
View attachment 2095289
Unaona hapo juu, August 13, 2020 coin moja ilikuwa inauzwa $0.000000000157. Sasa jiulize kwabei ndogo kama hiyo, na kama ungewekeza $200 ungepata coins ngapi? Kwa hesabu za haraka haraka, ungepata at least coins 1 Trillion. Baada ya Shib kwenda kwa slow motion kwa miezi kadhaa baadae baadae bei ya Shib ikapanda kwa kasi ya roket, ndo hapo nilipoweka box. Siku hizi bei ya Shib imeporomoka (hii ndo tabia kuu ya crypto) lakini pamoja na kuporomoka huko, bei yake kwa sasa ni $0.0000212. Sasa piga hesabu mwenyewe. Assume ndo uliwekeza zile $200, ukapata coins Trilioni 1, na leo ndo unaamua kuuza kwa $0.0000212 kwa coin. Hivi ulishajiuliza ungechukua dola ngapi hapo?! Hivi usingeona aibu kuchukua pesa yote hiyo wakati uliwekeza $200?
NInachokueleza hapo ni kwamba, Crypto sio utapeli. Utatapeliwa endapo umeingia kichwa kichwa bila kupata right information kutoka kwa right people. Tatizo lingine ndo hilo la ku-point, na upoint wakati gani. Kwa mfano, hivi sasa Shib bei yake ndo hiyo $0.0000212. Ukiona hayo mazero zero unaweza kujipa matumaini kwamba ni very cheap! In a long run, unaweza kuita ni cheap, lakini in a short run, tayari hapo bei yake imeshangamka!
Kwahiyo utake usitake, dunia ndo inaenda huko hivi sasa. Badala ya kujitisha na kuwatisha wenzako, chukua muda ujifunze! Huna haja ya kumlipa mtu kujifunza crypto. Lakini kama unaona kuwekeza pesa hapana, basi pitia hii post hii hapa. Hapo nimeelezea crypto inayoitwa Pi ( π) Coin. Hii haijaingia sokoni, kwahiyo hulipii hata senti 5 isipokuwa through mining. Of course, ingawaje Developer wa hii coin hawajaweka wazi lakini technique wanayotumia ndo kama hiyo uliyoita pyramid scheme. Hata hivyo, huyo haiwezi kuwa pyramid scheme kama unavyoweza kudhani. Kwanza, Founders wa hiyo project ni United States Citizens ,a ni graduates wa Stanford na ni PhD Holders. There's no way wanaweza kuanzisha pyramid scheme wakati pyramid scheme ni illegal ndani ya US. Na taarifa za hao founders zipo public, na kwahiyo kama wangelenga kuanzisha pyramid schemes, basi wasingeweka taarifa zao public. Hata hivyo, wanatumia hiyo model ambayo kwa haraka haraka unaweza kuamini ni pyramid scheme kwa sababu nguvu ya kwanza ya crypto coin yoyote ni kuwa na users wengi. Ikishakuwa na users wengi, itasajiliwa kirahisi tu kwenye legit exchange markets. Na pili, users wengi ni tafsiri ya kuwa na holders wengi waliosambaa sehemu mbalimbali duniani. Kuna biashara nyingi tu siku hizi zinapokea crypto kama medium of exchange. Sasa crypto inapokuwa na users wengi, inakuwa pia rahisi kutumuka na baadhi ya merchants kama medium of exchange. Kadri coin husika inavyozidi kukubalika, ndivyo bei yake inavyozidi kupanda kwa sababu demand inaongezeka!
Kutokana na hilo, unakosea sana unaposema "wanataka wafuasi wa ku-boost coin yao" huku ukiamini ni coin ya developers. Ingia twitter na utakuta coins nyingi zina akaunti kama hizi hapa chini
View attachment 2095322
Unaona hizo ni Army Accounts ambazo members/coin holders wanazianzisha wenyewe bila kutumwa na yeyote ili kui-promote coin. Wakati wewe unaamini ni "coin yao" kwa maana ya coins za developers, hawa armies wanaamini ni "coin yetu" kwa sababu bei ikitusua, na wenyewe wanatusua.
Chifu, usikubali kujifungia kwenye box la mbao, jifunze!! Hayo uliyoandika hapo juu ni kituko ambacho kinaonesha moja kwa moja hii industry bado kabisa huifahamu! Na pia ushauri wangu ni ule ule, kama hutaki kutumia pesa, bofya hapa kwa ajili ya uzi utakaokuwezesha kupata coins bila kulipa hata senti 5!
Naogopa post itakuwa ndefu lakini ningeonesha jinsi ambavyo nilipata zaidi ya Dogelon zaidi ya 100M bila kulipa hata senti 5. Of course, kama ilivyokwa crypto zingine, hivi sasa bei yake imeshuka sana lakini nikisema niziuze leo, sikosi $100 lakini nikivumilia na kuziacha zikae tu, usishangae baada ya muda zikafikia hata $10K
Mkuu watakuja kama mwewe..Ukiona unaitwa kwenye fursa na nguvu kubwa sana inatumika ujue kabisa wewe ndio fursa
WAJINGA NDIO WALIWAO, na ukienda kichwa kichwa wanakubamiza kweli
Mungu ameagiza tule kwa jasho nyie mmebadilisha mnakula kwa M B za mtandaoni, mnadownload pesa tu shchwaaaaaaa
FURSA YENYEWE NDIO HIYO UKIWAULIZA IMEPATA VIBALI HAPA TANZANIA NA KUSAJILIWA WANAKUWA MKALI MTAGOMBANA SIKU NZIMA
Ukipigwa au kutapeliwa kule ndio imekula kwako kwa kuwa huna sehemu ya kuwashtaki na uthibitisho rasmi sanasana utaishia kupoteza hela kufatilia kesi za hawa SCAMMERS
Najua mtakuja kunisema sijui chochote kuhusu haya mambo ya kuvuna coin, mara sijui wallet ila ndio hivyo mwenzako akinyolewa zako tia maji
Aisee, machawa wa blockchain na crypto msije kunivamia hapa ni mtazamo tu😎
😆
Maelezo yangu yametokana na hoja ya mtoa mada na ndo maana hayana maelezo kuhusu hoja yako.Halafu unamaanisha nini unaposema wanauziana cc zenyewe na kuzitunza kwenye kabati? Ukiangalia njia inayotumika kwenye biashara ya cryptocurrencies wala haina tofauti na biashara zingine zinazoangalia mwenendo wa soko.Mkuu umeandika maelezo marefu ila bado hayajibu swali la msingi kuhusu hizi cryptocurrencies; bado 99% ya watu wanaotengeneza pesa kwenye CC ni kwa kuuziana CC zenyewe kisha wanazitunza kama vyombo kabatini tu, bado haina applicable use on a daily basis for the most part.
Ili iwe widely acceptable inabidi iwe regulated kama currencies zingine which defeats the purpose of cryptocurrencies hence hitting the dead end.
Mwambie aachane na Forex, na ajifunze zaidi mambo ya crypto! Crypto sio suala la kununua na kuuza peke yake, kabla hujanunua kuna mengi ya kuangalia. Akizingatia ushauri wangu wewe mwenyewe hapo baadae utakuwa ndo mnunuliwa crates za bei badala ya uto tubia tumoja moja! Nawe unaweza kutembelea huu uzi kupata machache kuhusu coins ambazo haziuzwi. Unaweza kuanzia huko ambako huna cha kupoteza.Mkuu watakuja kama mwewe..
Kuna rafiki yangu kila siku namtoa beer ajabu hiyo forex na coin anazicheza kabla mimi sijapata job.
Lakini wapi daily yupo msoto
Katika hili la Cryptos namtetea sijawahi kushuhudia sehemu yoyote akisema alipwe pesa afundishe Cryptos au umpe pesa awejeze on your behalf.
Haya mambo ya kusema kuna siku itakuwa hivi au vile ni bora ununuwe shamba lako walau heka 5, upande mitiki baada ya miaka 10 mpaka 15 una uhakika wa kuwa tajiri kuliko hizo mambo zenu ambazo hakuna hata mtu mmoja wa kunionesha sample kwamba huyu haya ni mafanikio ya crypto currency, hakuna.Mwambie aachane na Forex, na ajifunze zaidi mambo ya crypto! Crypto sio suala la kununua na kuuza peke yake, kabla hujanunua kuna mengi ya kuangalia. Akizingatia ushauri wangu wewe mwenyewe hapo baadae utakuwa ndo mnunuliwa crates za bei badala ya uto tubia tumoja moja! Nawe unaweza kutembelea huu uzi kupata machache kuhusu coins ambazo haziuzwi. Unaweza kuanzia huko ambako huna cha kupoteza.
Lakini kwa upande mwingine, unatakiwa kumfariji tu bcoz kwa sasa soko la crypto lime-collapse vibaya sana. Bitcoin kwa mfano, miezi michache tu iliyopita ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya $65K lakini leo hii inauzwa chini ya $40K. Hii ni fursa kwa wanaoingia kwenye game au wanaotafuta kuongeza stock lakini kwa akina sie wenye senti za kuchungulia, ambao ukilipa $1K unabaki hoe hae, hiki kwetu ni kipindi cha maumivu huku tukisali bei i-stablize, na ni suala la muda tu, ita-stablize. Huo ndo uzuri wa crypto over forex. Forex unaiona akaunti yako inavyopukutika lakini crypto kinachopukutika ni market value ya crypto zako lakini crypto kama crypto zinabaki vile vile. Kwahiyo bei ikipanda, market value inapanda!
Kama utamkejeli ni kumuona f'ala kwa kudhani anaweza ku-download pesa mtandaoni kama ambavyo huwa mnakejeli, am telling you, kuna siku utakuja kuona aibu hata ya kumwambia akuelekeze! Mark my word.
Hiyo sample unayoitaka wewe ni kutoka kwa Watanzania wasio hata na uwezo wa kuwekeza huko, au? Kwa Bongo inaweza kuwa ngumu kwako kuona kwa sababu haya mambo huku Afrika yametawaliwa sana na vijana kwa sababu wao ndio wanaofahamu haya mambo ya mitandao! Kwa bahati mbaya, hawa vijana wengi hawana uwezo, kwahiyo ni kumi kwa mmoja mwenye uwezo wa kuwekeza angalau $1000. Na tatizo lingine, wengi wao wana-focus kwenye Bitcoin kwa sababu ina guarantee ya kupanda hata kama itakuwa imeshuka kiasi gani! Sasa huwezi kuwekeza $1000 kwenye Bitcoin inayouzwa $40K halafu ukatarajia huyo aliyewekeza $1000 atapata cha maana. Hawezi kupata hasara lakini ataishia kupata pesa ya kawaida tu! Lakini kama unakuwa risk taker, na kuwekeza hiyo $1000 kwenye riskier coins, yaani zile zinazoingia sokoni, Chifu, nisiseme sana!Haya mambo ya kusema kuna siku itakuwa hivi au vile ni bora ununuwe shamba lako walau heka 5, upande mitiki baada ya miaka 10 mpaka 15 una uhakika wa kuwa tajiri kuliko hizo mambo zenu ambazo hakuna hata mtu mmoja wa kunionesha sample kwamba huyu haya ni mafanikio ya crypto currency, hakuna.
Kamwe sitajihushisha na hayo mambo vibiashara vyangu vya kueleweka visivyo na unasaba na kamari pamoja na tumshahara twangu vinanitosha sana.Mwambie aachane na Forex, na ajifunze zaidi mambo ya crypto! Crypto sio suala la kununua na kuuza peke yake, kabla hujanunua kuna mengi ya kuangalia. Akizingatia ushauri wangu wewe mwenyewe hapo baadae utakuwa ndo mnunuliwa crates za bei badala ya uto tubia tumoja moja! Nawe unaweza kutembelea huu uzi kupata machache kuhusu coins ambazo haziuzwi. Unaweza kuanzia huko ambako huna cha kupoteza.
Lakini kwa upande mwingine, unatakiwa kumfariji tu bcoz kwa sasa soko la crypto lime-collapse vibaya sana. Bitcoin kwa mfano, miezi michache tu iliyopita ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya $65K lakini leo hii inauzwa chini ya $40K. Hii ni fursa kwa wanaoingia kwenye game au wanaotafuta kuongeza stock lakini kwa akina sie wenye senti za kuchungulia, ambao ukilipa $1K unabaki hoe hae, hiki kwetu ni kipindi cha maumivu huku tukisali bei i-stablize, na ni suala la muda tu, ita-stablize. Huo ndo uzuri wa crypto over forex. Forex unaiona akaunti yako inavyopukutika lakini crypto kinachopukutika ni market value ya crypto zako lakini crypto kama crypto zinabaki vile vile. Kwahiyo bei ikipanda, market value inapanda!
Kama utamkejeli ni kumuona f'ala kwa kudhani anaweza ku-download pesa mtandaoni kama ambavyo huwa mnakejeli, am telling you, kuna siku utakuja kuona aibu hata ya kumwambia akuelekeze! Mark my word.
Siku utakavyoenda kinyume na hayo, rudi tena hapa!! Na kama ungesoma thread yangu wala usingesema masuala ya kutajirika kwa sababu hakuna popote nilipoahidi utajiri na hata crypto niliyoizungumzia wala haijaingia sokoni na bei yake ni $0, na nimesema wazi kwamba:-Kamwe sitajihushisha na hayo mambo vibiashara vyangu vya kueleweka visivyo na unasaba na kamari pamoja na tumshahara twangu vinanitosha sana.
Tafuta ndugu zako na watu wako wa karibu watajirike, au wote wao wameshatajirika?!
Kwahiyo acha jazba, na usidhani kila mtu hapa ni ONTARIO anayetafuta kuwakamua watu kwa kuwaahidi utajiri!! Thread yangu haina mapicha picha ya watu wakiwa mbele ya mijengo wala kuendesha ma-BM but I only wanted to share what I believe kinaweza kuwa na bright future, ambayo sio leo wala kesho!!Usijiwekee matarajio makubwa lakini kama umevuna za kutosha, na baada ya muda Pi (Ï€) Coin moja ikafikia angalau $5 tu, hapo ndipo utakapokuja kuuona umuhimu wa thread hii.
Mkuu huna ndugu n awatu wa karibu wao hawataki pesa?!Siku utakavyoenda kinyume na hayo, rudi tena hapa!! Na kama ungesoma thread yangu wala usingesema masuala ya kutajirika kwa sababu hakuna popote nilipoahidi utajiri na hata crypto niliyoizungumzia wala haijaingia sokonina bei yake ni $0, na nimesema wazi kwamba:-
Kwahiyo acha jazba, na usidhani kila mtu hapa ni ONTARIO anayetafuta kuwakamua watu kwa kuwaahidi utajiri!!
Chifu, umelazimishwa?! Na unajuaje kwamba hakuna ndugu yangu anayefanya haya mambo?! Don't take it personal. Posts za JF ni kwa kila mtu hata kama mtu atakuwa ameku-tag au kuku-quote wewe, kwahiyo haina haja ya league lakini nimekushauri tu huna sababu ya kuapiza kwamba kamwe huwezi kufanya crypto!Mkuu huna ndugu n awatu wa karibu wao hawataki pesa?!
Mimi nimechagua kupata pesa kwa mfumo mwingine na sio huo