Yule mkongwe aliyeteka JF kuhusu Forex sasa kaingia kwenye Cryptocurrency, tusubiri vilio

Jamaa kwa kutunga yuko vyema, anaweza watungia story za South Africa watu wakaamini alikuwa huko kumbe fix, Jamaa kipaji cha kutubga story nampa 100
 


Mkuu umeandika maelezo marefu ila bado hayajibu swali la msingi kuhusu hizi cryptocurrencies; bado 99% ya watu wanaotengeneza pesa kwenye CC ni kwa kuuziana CC zenyewe kisha wanazitunza kama vyombo kabatini tu, bado haina applicable use on a daily basis for the most part.

Ili iwe widely acceptable inabidi iwe regulated kama currencies zingine which defeats the purpose of cryptocurrencies hence hitting the dead end.
 
Mkuu watakuja kama mwewe..
Kuna rafiki yangu kila siku namtoa beer ajabu hiyo forex na coin anazicheza kabla mimi sijapata job.
Lakini wapi daily yupo msoto
 
Maelezo yangu yametokana na hoja ya mtoa mada na ndo maana hayana maelezo kuhusu hoja yako.Halafu unamaanisha nini unaposema wanauziana cc zenyewe na kuzitunza kwenye kabati? Ukiangalia njia inayotumika kwenye biashara ya cryptocurrencies wala haina tofauti na biashara zingine zinazoangalia mwenendo wa soko.

Na kwa suala kwamba haina applicable use, usisahu kadri siku zinavyoenda, more and more companies zita adopt hizi currencies, na ni suala la muda tu kabla ya baadhi ya nchi kuzifanya ni legal tender kama walivyofanya El Salvador! Hata hizi fiat currency, wakati nchi zingine zinatumia fiat currencies, Afrika bado tulikuwa tunafanya barter trade! Ni suala la muda tu!

Kuhusu zikiwa regulated zitaharibu maana mzima ya crypto inategemea unazi-regulate kwa mapana yapi, na una-regulate nini! US wana-regulate crypto, na exchange markets ambazo hazi-conform with US Regulation zinapigwa ban kufanya biashara na US Citizens as well as PRs. Lakini pamoja na hayo bado crypto in US imebaki kuwa crypto.
 
Mkuu watakuja kama mwewe..
Kuna rafiki yangu kila siku namtoa beer ajabu hiyo forex na coin anazicheza kabla mimi sijapata job.
Lakini wapi daily yupo msoto
Mwambie aachane na Forex, na ajifunze zaidi mambo ya crypto! Crypto sio suala la kununua na kuuza peke yake, kabla hujanunua kuna mengi ya kuangalia. Akizingatia ushauri wangu wewe mwenyewe hapo baadae utakuwa ndo mnunuliwa crates za bei badala ya uto tubia tumoja moja! Nawe unaweza kutembelea huu uzi kupata machache kuhusu coins ambazo haziuzwi. Unaweza kuanzia huko ambako huna cha kupoteza.

Lakini kwa upande mwingine, unatakiwa kumfariji tu bcoz kwa sasa soko la crypto lime-collapse vibaya sana. Bitcoin kwa mfano, miezi michache tu iliyopita ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya $65K lakini leo hii inauzwa chini ya $40K. Hii ni fursa kwa wanaoingia kwenye game au wanaotafuta kuongeza stock lakini kwa akina sie wenye senti za kuchungulia, ambao ukilipa $1K unabaki hoe hae, hiki kwetu ni kipindi cha maumivu huku tukisali bei i-stablize, na ni suala la muda tu, ita-stablize. Huo ndo uzuri wa crypto over forex. Forex unaiona akaunti yako inavyopukutika lakini crypto kinachopukutika ni market value ya crypto zako lakini crypto kama crypto zinabaki vile vile. Kwahiyo bei ikipanda, market value inapanda!

Kama utamkejeli ni kumuona f'ala kwa kudhani anaweza ku-download pesa mtandaoni kama ambavyo huwa mnakejeli, am telling you, kuna siku utakuja kuona aibu hata ya kumwambia akuelekeze! Mark my word.
 
Kwani forex nayo ilikuwaje ?
Si alianza na story zake za kilimo
Katika hili la Cryptos namtetea sijawahi kushuhudia sehemu yoyote akisema alipwe pesa afundishe Cryptos au umpe pesa awejeze on your behalf.
 
Haya mambo ya kusema kuna siku itakuwa hivi au vile ni bora ununuwe shamba lako walau heka 5, upande mitiki baada ya miaka 10 mpaka 15 una uhakika wa kuwa tajiri kuliko hizo mambo zenu ambazo hakuna hata mtu mmoja wa kunionesha sample kwamba huyu haya ni mafanikio ya crypto currency, hakuna.
 
Hiyo sample unayoitaka wewe ni kutoka kwa Watanzania wasio hata na uwezo wa kuwekeza huko, au? Kwa Bongo inaweza kuwa ngumu kwako kuona kwa sababu haya mambo huku Afrika yametawaliwa sana na vijana kwa sababu wao ndio wanaofahamu haya mambo ya mitandao! Kwa bahati mbaya, hawa vijana wengi hawana uwezo, kwahiyo ni kumi kwa mmoja mwenye uwezo wa kuwekeza angalau $1000. Na tatizo lingine, wengi wao wana-focus kwenye Bitcoin kwa sababu ina guarantee ya kupanda hata kama itakuwa imeshuka kiasi gani! Sasa huwezi kuwekeza $1000 kwenye Bitcoin inayouzwa $40K halafu ukatarajia huyo aliyewekeza $1000 atapata cha maana. Hawezi kupata hasara lakini ataishia kupata pesa ya kawaida tu! Lakini kama unakuwa risk taker, na kuwekeza hiyo $1000 kwenye riskier coins, yaani zile zinazoingia sokoni, Chifu, nisiseme sana!
 
Kamwe sitajihushisha na hayo mambo vibiashara vyangu vya kueleweka visivyo na unasaba na kamari pamoja na tumshahara twangu vinanitosha sana.

Tafuta ndugu zako na watu wako wa karibu watajirike, au wote wao wameshatajirika?!
 
Kamwe sitajihushisha na hayo mambo vibiashara vyangu vya kueleweka visivyo na unasaba na kamari pamoja na tumshahara twangu vinanitosha sana.

Tafuta ndugu zako na watu wako wa karibu watajirike, au wote wao wameshatajirika?!
Siku utakavyoenda kinyume na hayo, rudi tena hapa!! Na kama ungesoma thread yangu wala usingesema masuala ya kutajirika kwa sababu hakuna popote nilipoahidi utajiri na hata crypto niliyoizungumzia wala haijaingia sokoni na bei yake ni $0, na nimesema wazi kwamba:-
Usijiwekee matarajio makubwa lakini kama umevuna za kutosha, na baada ya muda Pi (Ο€) Coin moja ikafikia angalau $5 tu, hapo ndipo utakapokuja kuuona umuhimu wa thread hii.
Kwahiyo acha jazba, na usidhani kila mtu hapa ni ONTARIO anayetafuta kuwakamua watu kwa kuwaahidi utajiri!! Thread yangu haina mapicha picha ya watu wakiwa mbele ya mijengo wala kuendesha ma-BM but I only wanted to share what I believe kinaweza kuwa na bright future, ambayo sio leo wala kesho!!
 
Mkuu huna ndugu n awatu wa karibu wao hawataki pesa?!
Mimi nimechagua kupata pesa kwa mfumo mwingine na sio huo
 
Mkuu huna ndugu n awatu wa karibu wao hawataki pesa?!
Mimi nimechagua kupata pesa kwa mfumo mwingine na sio huo
Chifu, umelazimishwa?! Na unajuaje kwamba hakuna ndugu yangu anayefanya haya mambo?! Don't take it personal. Posts za JF ni kwa kila mtu hata kama mtu atakuwa ameku-tag au kuku-quote wewe, kwahiyo haina haja ya league lakini nimekushauri tu huna sababu ya kuapiza kwamba kamwe huwezi kufanya crypto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…