Yule mkongwe aliyeteka JF kuhusu Forex sasa kaingia kwenye Cryptocurrency, tusubiri vilio

Mimi saizi siwezi poteza muda kubishana na vilaza ambao hawajui crypto currency ....

Ni matumizi mabaya ya akili ,ninafanya mwenyewe na sipo tayari kupoteza nguvu zangu kumwelekeza mtu ambaye tayari ana negativity na hii issue ..

Hold coin , siku wakikuita freemason achana nao ,
 
Umebadili ID?
 
Jifunze kuchambua watu wa kuwapa elimu/mwanga. Sio kila mtu anafaa kupewa mwanga, wengine ni sawa na kupigia mbuzi gitaa. Mtu anaye attack mtu individual badala ya fact achana nae mkimbie maana ni mpuuzi mno. Kwenye Dunia ya Leo full of information kila mtu abaki na anachokiamini. Anayeamini kilimo kinalipa, let it be. Anayeamini currency and stock trading zinalipa let it be. Mjinga mmoja haamini kama Kuna watu wanatengeneza pesa wakiwa wamekaa City pub au KFC au Pizza Hut achana nae. Anakaza forex ni kamali, sa akielezwa ya drop shipping ataelewa Nini! Au money movers kama Stock brokers Wana mashamba??
Tumieni smartphone zenu kujielimisha nyie watoto.
 
Upo sahihi kabisa! Ni bahati mbaya sana hadi 2022 watu wanatumia smartphone kama chombo cha mawisiliano tu na cha kuingilia kwenye social network bila kujua wanatembea Digital Universities mifukoni mwao!!!
 
Forex crypto vyote ni utapeli tu bora nikaajiriwe kwa muhindi nilipww buku saba zangu, hakika nakuapia hutoboi ng'ooo,
 
Kwan kuishi kwa forex sio kula kwa jasho?
 
Forex crypto vyote ni utapeli tu bora nikaajiriwe kwa muhindi nilipww buku saba zangu, hakika nakuapia hutoboi ng'ooo,
Mkuu umeelewa vibaya au aliekuelewesha kakuelewesha vibaya , forex sio utapel Ila ni taaluma . Kwahiyo wengi wanadhani kupata pesa kwenye forex ni lahisi kwahiyo ndio hapo inakuja kuonekana Kama utapel
 
Mkuu watakuja kama mwewe..
Kuna rafiki yangu kila siku namtoa beer ajabu hiyo forex na coin anazicheza kabla mimi sijapata job.
Lakini wapi daily yupo msoto
Forex ni kuchelewa kupata maisha tu, utakuta kijana wa miaka 25-30 anakomaa na forex tangu amalize shule lakini maisha yake ni apeche alolo.

Nina uhakika kuwa hâta hawa wanaoitetea humu hawana chochote walichopata huko isipokuwa ni imani tu ya kwamba siku moja watapata, kwakua akili zao zimelemazwa na hakuna namna wanaweza fanya kupata pesa.

Watu wa aina hii huwa ninawaona kama kuku wa kizungu (broilers)
 
Hawa vijana huwa wanaimani kubwa sana, wajinga kabisa.
 
Akitoka crypto ni nft, mwendo wa kula pesa za wapenda kitonga
 
Mkuu watakuja kama mwewe..
Kuna rafiki yangu kila siku namtoa beer ajabu hiyo forex na coin anazicheza kabla mimi sijapata job.
Lakini wapi daily yupo msoto
Hapa chawa Pro max wa forex na crypto hawakuelewi yaani nakwambia🤣
 
Mpaka umeandika gazeti leo,kweli umechafukwa....pole yao ngoja wamtajirishe mkulima tajiri,yajayo yawafurahishe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…