EPISODE 2
Baada ya Prince Chibonge kunikurupua nilienda kwa step maza kuitikia wito.Nilimkuta yuko jikoni akipika chapati za maji na chai ya maziwa ikichemka kwenye jiko la pembeni huku mwanae wa mwisho ambae ni rika langu aitwae Tide akiwa kakaa kwenye kigoda pembeni ya mama yake akila chapati.Nyuma yangu alikua Prince chibonge.Alipoingia tu pale jikoni na kuona Tide anakula chapati na yeye akaomba akapewa moja akaikunja kisha yote akaitia mdomoni halafu akanyoosha mkono kuomba nyingine lkn mama yake akamwambia"Hebu toka hapa wewe nikikuendekeza utakula zote na bado hutashiba" lkn Prince chibonge akaendelea kunyoosha mkono huku akimuangalia mama yake kwa macho ya huzuni na mama yake kwa vile hapendi kuona wanae wakihuzunika akachukua chapati nyingine akampa na kumwambia nyingine asubirie mezani.
Na mimi nikamuangalia step maza kwa macho ya huruma nikiamin muujiza utatokea na mim nionjoshwe japo kipande lkn I was wrong kwani baada ya kumalizana na Prince Chibonge step maza akanigeukia na kuniambia"Nenda kule bafuni kuna nguo nimeziloweka ukafue",Nikaondoka kinyonge huku harufu nzuri ya chapati za step maza ikinisindikiza.Na mnyonge mnyongeni ila step maza wangu anajua kupika bana,sema tu sijui alikua ananikomoaga maana alikua akipika atahakikisha amechafua vyombo vyote.
Basi bana siku yangu ikaanza rasmi,baada ya udobi kuna kufagia uwanja,kuosha vyombo,kusafisha ndani,kuwekea bata maji na pumba,bado kuna kutumwa na katika yote hayo hakuna hata moja nililofanya akaridhika nalo,so shukran ilikua kama sio kwezi basi sitakosa japo tusi.
Nadhan mnakumbuka kuwa jana yake mzee Kipipa alimpa step maza mshiko wa maana eeh?Basi bwana lunch alopikiwa mzee Kipipa siku hiyo lilikua sio ya mchezo.Mama wa kisambaa alitulia jikon akapika vikapikika na vilivyoiva kama kawa nikaambiwa nimpelekee mjomba Kipipa chakula lkn kusikia tu hivyo nikaanza kutetemeka ghafla na nikakimbilia chumbani kulala nikajifunika gubigubi kwani nafsi yangu haikua radhi kumuona tena yule mzee lkn haikuchukua round step maza akaja kunifunua na kusema"Haya ndo mauzauza gan tena unayoniletea?Nikamwambia mama mim naumwa sitaweza kwenda lkn alinichomoa pale kitandani na kunivuta mpaka nje liliko kapu lenye msosi wa mzee Kipipa na kunishikisha kwa nguvu kisha bila kusema kitu akaweka sura ya subutu kukataa kwenda uone.Kinyonge sana nikaanza kutembea kupeleka chakula huku machozi yakinitoka na nilipokutana na watu njian nalijifuta machozi na kuficha uso mpaka nikafika site.Mzee Kipipa Alivyoniona tu kwa tabasamu la furaha akasema "Hujambo malkia wangu Clepatina" nikataka kujibu sijambo shikamoo mjomba lkn nikashindwa.Machozi yakaanza kunilenga lenga lakin nilipomuangalia niliona ananiangalia kwa macho ya kunitisha,nikawa najizuia kulia lkn nikaona mpaka nitoe mahot pot na sahani na vijiko ili nirud na kapu kama ninavyofanyaga machoz yatanizid nguvu mambo yawe mengi hivyo nikaacha kapu na kila kitu ndan yake kisha bila kuaga nikageuka na kukimbia nyumbani.
Wakati nakimbia niliwasikia baadhi ya mafundi pale site wakiulizana "kamepatwa na nin haka leo?"
Nilipokua njian nilipita sehemu kuna kichaka.Nikaingia humo nikajificha halafu nikaliaaa mpaka machoz yakawa hayatoki tena kisha nikasimama kwa lengo la kuondoka lkn nikasita baada ya kuona mti wenye vitunda fulani ambavyo nilisikiaga eti ukivila halafu ukilala unakufa huamki tena.Nikatabasamu kisha nikavichuma vingi vikajaa mikono yote miwili kisha nikakimbia kuelekea home.
Nilipofika karibu ya home nikaingia kwa kunyata ili mtu asinione.Maza nikamuona yuko nyuma ya nyumba na mashost zake wanasukana na kupiga umbea,Prince Chibonge na Tide sikujua wako wapi.Nikaingia kwa kujificha mpaka chumbani kwangu,nikafunga mlango kwa ndani na kutafuna vile vitunda vyote nikajifunika gubi gubi nikiamini usingizi ukinichukua tu ndo imetoka hiyo siamki tena na hakuna atakayeweza tena kunituma kwa mzee Kipipa.
Hata hivyo nilikuja kuamka saa mbili ya usiku ule.Kilichotokea ni kwamba mama alijua tokea nitumwe ule mchana kupeleka chakula kwa mzee Kipipa sikurudi tena kwa vile hakuna aliyeniona nikirudi.Masaa yakapita,prince Chibonge akatumwa akanitafute hakuniona na kwa majirani sikuwepo. Maza akamtuma Chibonge akatafute fimbo nzuri kubwa zinisubir nitakaporud lkn mpaka muda wa kupeleka chakula kwa mzee Kipipa ukafika hawakuwa na wazo la kutazama chumbani kwangu.Ikabidi Prince Chibonge ndio apeleke chakula siku hiyo.
Kufika kule mzee Kipipa akauliza kwanini leo umeleta wewe na sio Clepatina?Prince Chibonge akajibu"Shida yako ni chakula au Clepatina?"Mzee Kipipa akataka kumdaka Chibonge amchape ila Prince Chibonge akafanikiwa kukimbia.Prince Chibonge alitokea kumchukia mzee Kipipa tokea siku ya kwanza anafika nyumbani kwetu na shikamoo yake kwa mzee Kipipa ilikua inatoka kwa kulazimishwa.
Kufika saa moja na nusu hivi usiku, mmoja wa majirani aliyefika pale nyumban kusaidiana mawazo juu ya nini kifanyike kwa kupotea kwangu akiwa anelekea chooni kwetu ambako njia iko karibu na dirisha langu alisikia sauti ya kicheko kutoka chumbani kwangu.Akachungulia na kumulika na tochi zile za betri na hamadi ananiona nimelala fofofo nacheka usingizini.
Jirani yule akaahirisha safari ya kwenda chooni na kisha kwenda kumuuliza mama yangu wa kambo"Uliangalia chumban kwake?".
Hilo swali ndo likamkumbusha step maza kuwa wametafuta kijiji chote kasoro chumban kwangu.Basi yule jirani akawaambia alichokiona na kweli kufika pale dirishani wakanikuta nimelala fofofo sina habari nacheka zangu ndotoni.
Zoezi la kuniamsha likaanza lakini halikua rahisi maana waliita, walirusha magunzi,maji,vimawe lakini wapi.Kama sio kule kucheka ndotoni wangehisi nimekufa.Ilibidi mlango uvunjwe nitikiswe kwa nguvu ndio nikaamka.Kilichofanya nilale vile ni mlundikano wa usingizi wa siku nyingi na uchovu.Mara nyingi nilikua nachelewa kulala nawahi kuamka.Nikaulizwa kama niko sawa nikajibu niko sawa step maza akajifanya eti amefurahi hadi akalia kwa furaha eti maana alidhani eti mwanae kipenzi nimepotea au nimepatwa na kitu kibaya ila majirani walivyoondoka usitake kujua nini kilinipata.
Siku hiyo ikawa imepita hivyo na siku nyingine zikaja na kazi zangu ni zile zile ikiwa ni pamoja na kumpelekea mzee Kipipa chakula site na nyumbani kwake jion.
Mzee Kipipa nae akaendeleza ufiraun wake, mara ya pili ya tatu na mwishowe ikawa ni utamaduni na kilichomsaidia ni kwamba kila alipomakiza ushetani wake ilikua lazima anipe hela huku akiniambia "hizi kampe mama yako mwambie mjomba anasema asante".
Ghafla step maza aligeuka bosslay wa kijiji kwa pesa za mzee Kipipa.Hakuna kanga/tenge mpya ilitoka akashindwa kununua,alokula vizur mtaan alikua yeye,kuvaa vizur ni yeye, inshort pesa ndogondogo hazikua issue kwake.Nadhani kuna mahala ilifikia step maza akajua kinachoendelea kule kwa mzee Kipipa ila kwa vile sikua mwanae na kwa vile hela ya mzee Kipipa ilishamnogea ikafika wakati kabla ya kunituma nipeleke kapu jioni alikua ananiambia nikaoge kwanza na nilishangaa siku step maza aliponipa mafuta yake nijipake na kuniambia nisirudie gaun chafu bali nikavae gauni langu la kanisani.Mwayego nilipendeza kisha akanipa kikapu nipeleke chakula kwa mjomba mzee Kipipa.Mzee Kipipa alivyoniona akasema vile ndo napaswa kuwa kila niendapo kwake.Akafanya afabyayo na kama kawaida alipomaliza akinipa hela nimpelekee step maza tofaut ni kwamba siku hiyo hela zilikua nyingi.
Maisha yakaendelea hivyo,nikawa mnyonge siku hadi siku, sina raha na mara nyingi nilitamani kujiua.
Ujenz wa shule ya mzee Kipipa uliendelea na siku moja akaaga kuwa anarudi Dar mara moja kwenda kupumzika na kuwaona familia yake.Step maza aliipokea habar hiyo kwa huzun mithili ya mtu aliyesikia habari ya msiba lkn kwa upande wangu ilikua ni habari ya faraja tena nilitaman yule mzee agongwe na gari afe kabisa na asirud tena kijijin kwetu.Kwa upande wangu mzee Kipipa aliniaga tokea jana yake alipomaliza kunifanyia ushetani wake.Aliniambia kuwa kesho ataondoka kijijin ila akirud akasikia nimemwambia mtu yeyote kuhusu 'uchumba' wetu basi atamuua mama yangu mzazi.
Basi mzee Kipipa akasafiri huku akiaga kuwa atarud baada ya mwez mmoja lkn miez na miaka ikakatika ila hakurudi tena.
Kwa upande wangu kuondoka kwa mzee Kipipa kulipunguza mzigo mzito wa mateso lakini baada ya kipindi fulani nikaanza kutokwa na vitu vichafu sehemu za siri,homa kali na nilikua natoa harufu mbaya.
Baada ya majirani kuanza kunong'ona step maza akanipeleka hospitali.Nikatibiwa na kuambiwa niseme anayeniingilia.Nilibembelezwa,nilitishiwa lkn kila nilipoulizwa nilisema sijui na mwishowe yakaisha hayo.
Nilikua mtoto mwenye kupenda shule lakin mahudhurio yangu yalikua mabaya kutokana na majukumu ya nyumbani.Hata hivyo pamoja na kuwa Tide alikua hakosi shule lakini mim mwenye mahudhurio mabovu nilifaulu vizuri sana kwenye mitihani yetu ya mwisho ya darasa la nne na yeye kufeli kias cha kuhitajika kurudia darasa.Mim na Prince Chibonge ndio tuliokua tunaongoza kwa akili shule.
Wiki ya kwanza ya mim kuripoti shule kama mwanafunz wa darasa la tano step maza ambae alikua amelazwa hospitali kwa kupooza akaruhusiwa aendelee na matibabu nyumbani.Mpaka anarudishwa nyumnan ndugu zake wengi waliokuja kumuuguza wakawa wameondoka na hivyo ikawa amebakia mama yake ambae nae alikua ni mgonjwa.
Basi ikawa kila siku nikitaka kwenda shule naambiwa nibaki nimsaidie bibi yule kaz za nyumbani.Kina Tide na Prince Chibonge wao wanaenda shule.Wiki mwezi,miez mwaka na ndo ikawa bye bye sikurudi tena shule.
Baada ya kipindi kirefu sana baba akarud nyumban siku moja,ilikua ni furaha kubwa kwangu nikitumai ya kwamba ujio wa baba utabadili maisha yangu.
Nikatafuta wasaa,nikamueleza yote ninayopitia pale na kwamba kama inawezekana anipeleke nikaishi na mama yangu.Baba akasema amekuja mara moja kumuona mama na kwamba atakaa siku tatu tu na kuondoka ila atakuja kunichukua nikakae nae huko kazin anapokaa na nitaendelea na masomo huko lakin baada ya kuondoka dingi hakugeuka nyuma.
Kumbe zile chuki zote za step maza kwangu zilichangiwa pia na kutelekezwa na dingi.Dingi wangu alikua na bado ni mzee wa totozi nyingi.Wakat step maza anaumwa dingi alikua keshaanzisha maisha na mwanamke mwingine wanaishi kama mke na mume.Hata alivyokuja alikuja tu kibinadamu lkn hakuwa amekuja kama kwa mkewe.
Yule bibi,mama yake na step maza alikaa na sisi kama miez minne hivi kisha na yeye akaondoka ikawa wanakuja wale ndugu wakuja kumuona mgonjwa leo na kuondoka kesho lakin pia step maza alishapata nguvu wakutembea mwenyewe lakin alipata changamoto ya kudondoka kama mtu mwenye kifafa.Anaweza akawa kashinda vizuri tu ghalfla akadondoka.
Ugonjwa wa step maza ulinifanya nikomae akili kabla ya umri kwani alivyoondoka yule bibi ikawa kama vile mim ndo mama wa ile familia.
Imagine mtoto wa umri wa kuwa darasa la tano nilikua bila kuelekezwa najua nikiamka nifanye nini,nipange tutakula nin kulingana na pesa niliyopewa na siku hakuna pesa nilijua nikachume nini shamban au ndan kuna nin nipike tule.
Pamoja na kuwa prince Chibonge alikua mkubwa kwangu na Tide tulilingana ila mim ndo nilikua kama dada yao mkubwa.Nilikua naweza kwenda dukan bila kuambiwa na mtu na kukopa sabuni ili ndugu zangu wafue nguo za shule au nifue nguo za step maza.
Hichi ndo kipindi atep maza alikua akinionesha upendo.Nilipokua nikimpelekea msosi alikua akiuliza kama na mim nimekumbuka kula au nahudumia wengine tu.Ndo kipindi alitoa kanga zake sandukuni akanigea,ndo kipindi alinambia mim ni baraka kwake na aliniahid ni lazima nirud shule akishapona.
Kwa vile manyanyaso yaliisha na nilikua nakula nakushiba nilinenepa na kwa vile mim ni supa tall kama baba yangu na shepu kama la mama yangu nilionekana kama msichana mkubwa kumbe toto la la tano.Mrefuu,juu mwembamba chin nimwagie kama namba 6.
Vijana wazee na waume za watu wote walikua wanafukuzana kuonja makombo ya mzee kipipa lkn wote niliwaona kama mbweha tu na kama sikuwaona kama mzee Kipipa basi ni kama mjomba na kama si kama mjomba basi ni kama baba tu.Mpaka hapo nilishajijengea picha kuwa wanaume wote hawana huruma.
Siku moja mwezi wa December ya ule nwaka niliotakiwa niwe la tano nilikua nimeenda kuhemea na wakati narudi nyumbani nikamkuta step maza akiwa amekaa nje na mgeni aliyeonekana kutoka mbali.Kufika karibu wala haikuchukua muda kumkumbuka sura chafu ya mzee Kipipa japo alikonda hadi kitamb kikamuisha.Step maza kuniona tu akasema kwa furaha"Mwanao uliokua ukimuulizia kila saa huyo hapo"
Baada ya kuambiwa vile mzee Kipipa alionekana kunishangaa sana kisha akasema"Ina maana Clepatina ndio amekua..amekua...mmm...mmmkubwa hivi?"
Step maza akacheka halafu akasema "watoto wa siku hizi kaka wanakua kama uyoga sijui wanakimbilia wapi" kisha step maza akanigeukia na kuniuliza "Klee unamkumbuka mjomba wako au umeshamsahau?"
Baada ya swali hilo
Nikamgeukia mzee Kipipa aliyekua akijichekesha chekesha pale nikamtizama kama sekunde ishirini hivi kwa sura ya kumchimba biti nililomaanisha kisha kwa sauti iliyochanganyika hasira,uchungu,kisasi na kwa kujiamini nikamkazia macho nikamwambia
"NAWEZA KUISAHAU SURA YA BABA YANGU NA NIKAWA NA AMANI LAKINI SIWEZI KUISAHAU SURA YAKO NA NIKAISHI KWA AMANI!!".
Baada ya kumtamkia maneno hayo niliendelea kumkazia macho kwa muda mrefu kisha nikageuka polepole na kutembea kuelekea jikoni na kimya kikuu kikatawala nyuma yangu.
My sis
Joannah darling bro
Half american bestie
Equation x
Watu8 Analyse To yeye Shunie Antonia Gautama cocastic babukijana Depal Glenn Unique Flower dronedrake
Dr. Mariposa