Yupi ndiye msanii bora zaidi kwa sasa Afrika?

Kimatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
286
Reaction score
271
Soko la muziki barani Afrika limekua sana kwa sasa, haishangazi kuona wasanii mbalimbali wakipishana kwenye majukwaa makubwa duniani kote kufanya show zinazowaingizia kipato.

Kuna wasanii wengi sana wa Afrika wanaovutia kiasi hadi cha nyimbo zao kuwa kwenye playlists za watu mbalimbali mashuhuri duniani, kuwa nominated kwenye tuzo kubwa kama Grammy, BET n.k,

Kuwa kwenye charts maarufu kama billboard, kupewa collabo na wasanii wakubwa duniani, kupiga shows Ulaya, mfano kama Burnaboy, Wizkid, Davido, Simi Diamond Platnumz, Tiwa Savage,Yemi Alade, Patoranking, Rema, Mr Eazi, Harmonize na wengineo wanafanya vizuri. Ila je, nani ni zaidi ya wote na kwa kigezo kipi?
 
Burnaboy..Grammy nominated

Alikua na mwaka bora sana uliopita, ila mwaka huu nahisi kuna vichwa vingine vimejipanga kama Wizkid ambae anatarajia kuachia album yake aliyoitengeneza kwa miaka kitabu, ila Burnaboy hapoi July kuna uwezekano akaachia album nyingine "Twice as tall"
 
kwa sasa ni burna boy bt kwa mwaka huu mfalme wa utube anatisha coz jeje ndo ngoma kubwa baran africa mpaka sasa, inaongoza mauzo platform zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…