Soko la muziki barani Afrika limekua sana kwa sasa, haishangazi kuona wasanii mbalimbali wakipishana kwenye majukwaa makubwa duniani kote kufanya show zinazowaingizia kipato.
Kuna wasanii wengi sana wa Afrika wanaovutia kiasi hadi cha nyimbo zao kuwa kwenye playlists za watu mbalimbali mashuhuri duniani, kuwa nominated kwenye tuzo kubwa kama Grammy, BET n.k, kuwa kwenye charts maarufu kama billboard, kupewa collabo na wasanii wakubwa duniani, kupiga shows Ulaya, mfano kama Burnaboy, Wizkid, Davido, Simi Diamond Platnumz, Tiwa Savage,Yemi Alade, Patoranking, Rema, Mr Eazi, Harmonize na wengineo wanafanya vizuri. Ila je, nani ni zaidi ya wote na kwa kigezo kipi?