Yupi ni kocha bora wa kigeni kuwahi kufundisha ligi ya Bongo?

Yupi ni kocha bora wa kigeni kuwahi kufundisha ligi ya Bongo?

Kama wana Yanga wamemsahau Prof Dusan Condic basi atakuwa hawana shukrani.

Huyu mchawi wa kiserbia ndiyo aliyekuja kuwapa Yanga ubingwa baada ya kuukosa Miaka mingi mfululizo.

Lakini huyu jamaa ndiye aliyekuja kuufuta uteja wa Yanga kwa Simba uliodumu kwa miaka 12 mfululizo.

Kumbukeni kikosi cha Yanga cha kina
Obren cirkovic
Ivo Mapunda
Shadrack Nsajigwa
Godfrey Bonny
Rashid Gumbo
Wisdom ndlovu
James chilaponda
Credo mwaipopo
Fred Mbuna
Shamte Ally
Nabir cannavaro
Boniface Ambani
George Owino
John Baraza
Edwin Bukenya
Athuman Idd chuji
Gaudence mwaikimba
Ndiyo nilikuwa kikosi Bora kabisa cha Yanga cha karne ya 21.

Tuweke kumbukumbu sawa sawa Zahera hajafikia hata mafanikio ya Sam Timbe au Hans Van del pluijm.

Kukawa na Maurice Sunguti, umenikumbusha shamba la bibi miaka ya 2008, huyo baraza huyo alimshikisha beki wa Mji Mpwapwa ndani ya kumi na nane enzi hizo, beki alienda kukaba akiwa katanua mikono jamaa akambetulia mpira ilikua ndani ya Jamhuri Moro
 
papa zahera alituingiza sana mkenge yanga! kapewa nafasi ya ukocha yeye kajiongezea majukumu, msemaji wa klabu yeye, mdhamini wa club yeye, muhamasishaji yeye! aliyekuwa analia kwa ajili ya klabu yeye (hapa alitushinda mpaka mashabiki kulia kwa sababu ya yanga

sasa kwa nini asiwe yeye kocha bora
 
James Siang'a aliifanya Simba S. C kutisha kipindi chake.

Tambwe Leya kupitia vijana wadogo wa Yanga aliifanya timu ya kutisha.
 
Back
Top Bottom