Yupi ni kocha bora wa kigeni kuwahi kufundisha ligi ya Bongo?

Victor stantclaus, Tambwe Leya,Raul Shungu,Rudi Guntendorf, Micho, Plujim(Yanga),/Nabi Camara,Samsorov,Edil Silva, Popadi, Sianga, Patrick Phiri,Omog, Lenchentre na Patrick Aussem( Simba)
Tom Saintfit alifundisha mpira mkubwa sana
 
Nikipima kwa vigezk vya mafanikio
James siang'a na Patric Ausesm kwa upande wa vilabu wao ni bora..!

kwa timu ya Taifa Amunike kufuzu Afcon...!

Nje ya hapo ni upenzi tu...lakin hakuna kocha aliefikia level hizo.!
 
James Siang'a alitupa ubingwa wa ligi bila kufungwa.

James Siang'a siku tunrudiana na Ismailia, tunawachapa 2 - 0 ndani ya nusu saa, mvua inaharibu sherehe.

Yule mdingi alituletea heshima sana.
Kocha aliyeipa Simba ubingwa bila kufungwa ni Patrick Phiri pekee, ila nakubali Siang'a alikuwa bonge la coach Simba, alitupeleka champions league 2003 kwa kumtoa bingwa mtetezi Zamalek akishirikiana na Talib Hilal
 
Professor Victor na Tabwe leya hawana wapinzani !
Professor Victor hana mpinzani, ndiye aliyeipa Yanga ubingwa Mara 5 mfululizo 1968 to 1973 akina Sunday Manara, Maulid Dilunga ni vipaji alivyovikuza. Mwanzilishi wa kwanza wa soka la watoto Tanzania ambalo lilizaa vipaji vya ukweli kuwahi kutokea Tanzania, Kassim Manara, Tostao, Mkweche, Jaffari, Adolph Rishard, Juma Mensah Pondamali nk. Aliwahi kurejea miaka ya 2,000 kama kocha wa Taifa Stars lakini kwa misimamo yake ya umakini aliondoka faster baada ya kuona TFF (FAT) haina weledi.
 
Kocha aliyeipa Simba ubingwa bila kufungwa ni Patrick Phiri pekee, ila nakubali Siang'a alikuwa bonge la coach Simba, alitupeleka champions league 2003 kwa kumtoa bingwa mtetezi Zamalek akishirikiana na Talib Hilal

Asante kwa kunifahamisha ndugu, file langu lilirecord tofauti.
 
Professor Victor hana mpinzani, ndiye aliyeipa Yanga ubingwa Mara 5 mfululizo 1968 to 1973 akina Sunday Manara, Maulid Dilunga ni vipaji alivyovikuza. Mwanzilishi wa kwanza wa soka la watoto Tanzania ambalo lilizaa vipaji vya ukweli kuwahi kutokea Tanzania, Kassim Manara, Tostao, Mkweche, Jaffari, Adolph Rishard, Juma Mensah Pondamali nk. Aliwahi kurejea miaka ya 2,000 kama kocha wa Taifa Stars lakini kwa misimamo yake ya umakini aliondoka faster baada ya kuona TFF (FAT) haina weledi.
Kwa kuongezea tu Professor Victor ndiye aliyeifkisha Yanga Robo fainali klabu bingwa ya Africa mwaka 1969 ikiwa ni record wakati huo, na kutolewa kwa kura (yaani kurusha shilingi) na klabu nguli kabisa wakati huo Asante Kotoko ya Ghana
 
Patrck Aussens mnyonge mnyongeni.......
Hakuna ukweli sana kwa Patrick Aussems katika hili, ni kweli ni kocha mzuri anayejua kuusoma mchezo, lakini anabebwa sana ubora wa wachezaji (uwekezaji) wa Simba. Hawezi kukuza vipaji ( Salamba, Kaheza, Rashid nk), misimu miwili ameshindwa kujenga difensi imara Simba na kutolewa na UD Songo kumedhihirisha uwezo wake ni wa kati na si wa kuifikisha Simba lengo wanalolitarajia.
 
Professor Victor hana mpinzani, ndiye aliyeipa Yanga ubingwa Mara 5 mfululizo 1968 to 1973 akina Sunday Manara, Maulid Dilunga ni vipaji alivyovikuza. Mwanzilishi wa kwanza wa soka la watoto Tanzania ambalo lilizaa vipaji vya ukweli kuwahi kutokea Tanzania, Kassim Manara, Tostao, Mkweche, Jaffari, Adolph Rishard, Juma Mensah Pondamali nk. Aliwahi kurejea miaka ya 2,000 kama kocha wa Taifa Stars lakini kwa misimamo yake ya umakini aliondoka faster baada ya kuona TFF (FAT) haina weledi.
Mkuu hii ni historia ya kweli kabisa ambayo watu wengi hasa vijana wa sasa hawaifahamu. Professor Victor Stanculescu hana mpinzani na kama angeendelea kwa muda kua hapa nchini soka letu lingekua mbali sana. Yeye alikua anatengeneza vijana. Nakumbuka Yanga walikua na vikosi kama vitatu au vinne hivi

Kulikua na Yanga Kids ambao walikua ni under 14. kulikua na Yanga B na timu ya wakubwa na reserves wake.Wachezaji wadogo walikua wanafundishwa namna ya kuuchezea mpira na control ndio maana kukawa na mafundi hasa wa mpira

Kuna timu ya Pan Africa FC ambayo ilimeguka kutoka Yanga iliundwa na wachezaji hao waliotengenezwa na Victor yaani kina Juma Pondamali, Mohamed Mkweche, Jafar Abdulrahman, Leogder Tenga, Leopord Tasso, Mohamed Yahya "Tostao", Mohamed Richard Adolf, Ali Katolila, Gordian Mapango,, Kassim Manara na wengineo

Sina hakika kama kina Hussein Ngulungu, John Faya, Abdallah Burhani na Peter Tino ambao nao walikua Pan walipitia pia mikononi mwake
 
Victor stantclaus, Tambwe Leya,Raul Shungu,Rudi Guntendorf, Micho, Plujim(Yanga),/Nabi Camara,Samsorov,Edil Silva, Popadi, Sianga, Patrick Phiri,Omog, Lenchentre na Patrick Aussem( Simba)
Huyo Edil Silva aliwafundisha 'Samba na Diagonal' Simba ilikuwa ukiwatazama unafurahi na roho yako.
 
Back
Top Bottom