Dah umenikumbusha mbali, hiyo ilikuwa mwaka 1983, Simba ya kina Lilla, Mogella, Malota, Innocent Haule, Mkandawire baada ya kwenda Brazil mwezi mzima pre season wakiwa chini ya kocha Mbrazil Edil Silva, Simba ilirejea imeiva kweli kweli na mechi ya kwanza wakapangiwa CDA wakati huo wanajulikana kama watoto wa nyumbani, moto kweli kweli akina Mgodo, Mgeni, Nyuki, Adolph Kondo, Simfukwe, CDA walilala 2 - 0 lakini walipigiwa diagonal acha mchezo. Wakati huo Rage kiongozi wa Simba alikuwa na rap Manara cha mtoto, lakini hiyo diagonal na baadaye samba zilidumu miezi mitatu tu, Simba ikapoteza mwelekeo, na Silva akaondoka kimya kimya, mwishoni mwa msimu Yanga bingwa.