Roger Milla alistaafu soka la kimataifa mwaka 1987 na kuelekea katika visiwa vya reunion akijishughulisha na biashara khasa viatu baada ya cameroon kufuzu kombe la dunia mwaka 1990 timu na viongozi wakenda ikulu kwa mh Paul biya kwa pongezi basi katika mazungumzo akaulizia kuhusu Milla wa kamwambia mzee huyo unaemtaja tayari kesha tandika daruga mh rais hakukubaliana nao akawaambia mchezaji yule aitwe na kwa msisitizo akaomba namba ya Milla na kumtwangia aje ashiriki bila khiyana ilikuwa imebaki miezi mitatu kitu kama hicho.
Mwanaume akaja kufanya yake na moja kati ya mabao yake alimfunga nyanda mwenye mbwembwe nyingi rene heiguita baada ya kutaka kumlamba chenga.