Yupo Wapi Ally Kamwe kwenye Tamasha la wiki ya Mwananchi?

Yupo Wapi Ally Kamwe kwenye Tamasha la wiki ya Mwananchi?

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
631
Reaction score
2,247
Yu wapi?!
Haja onekana kabisa kwenye Tamasha.

“Yanga Walikosea kama unaweza kumtafuta Mobetto popote alipo sasa kwanini walishindwa kumtambulisha alikamwe na kama allishindwa kufika uwanjani hata wangemtaja tuu.

Soma pia: FT: Yanga 2-1 Red Arrows | Siku ya Wananchi 2024 | Mkapa Stadium

PS.

ana andika mwana michezo Nazareth Upete.
______________________
______________________

😄 Andiko lililopita niliandika kuhusu UUNGWANA wa ALLY KAMWE jana kwenye tamasha!

Wakati nikipitia Comments kuna maswali kadhaa ambayo mmeyauliza na nitajibu!

Ally Kamwe hakuwa muhimu KUTAMBULISHWA!?

Jibu ni NDIO… Ally Kamwe hakustahili Kutambulishwa (UNVEILING) kwa sababu tayari alishafanyiwa na jana ilikuwa maalum kwa ajili ya wachezaji.

Nini Kilipaswa kufanyika kwa Ally Kamwe!? Kwa jana alistahili kufanyiwa kitu kimoja tu… KUTAMBULIWA HADHARANI (ACKNOWLEDGEMENT / RECOGNITION) Yeye ndiye aliyewaita mashabiki… Kulikuwa na kila sababu ya kutambua hadharani kwa mchango wake mkubwa wa tukio lile na usimamizi mzuri wa mambo.

Niliona MC’s wakisifia hadharani kuwa wamejaza uwanja wa UHURU… Ilishindikana nini kusema ALLY KAMWE amefanya kazi nzuri kuhakikisha na kule Uhuru kunakuwa mahali rafiki!? Kusema haikuwa lazıma ni kupakaza mafuta kwenye miguu michafu.

Swali la 2. Ally Kamwe amesema KAZI ITAMTAMBULISHA!

Well, Very professional Comment! Ally katumia kanuni na muongozo namba moja wa kitaaluma ya Mahusiano ya Jamii (PUBLIC RELATIONS) kuwa PROTECT YOUR ORGANIZATION’S IMAGE AT ANY COST yaani Ilinde sura ya taasisi yako kwa gharama yoyote! Ulitarajia aseme SIJATENDEWA HAKI!?

Swali la 3. Yanga kuna mgogoro!?

Jibu linaweza kuwa NDIO au HAPANA! Inawezekana wao wenyewe walipanga mambo yaende vile!

Itakuwa ni Mgogoro kama wale walioongoza tamasha hawajamtafuta hata ‘kumplease’ kwa kilichotokea!

Kama walimsahau Mkuu wa Mkoa na Kamati tendaji why tuamini kumsahau Ally Kamwe ilikuwa ni MGOGORO!? Probably walipitiwa! JUST PERHAPS.

Generally: Ally Kamwe ni kielelezo cha mtu muungwana na mwenye adabu sana. Kutambuliwa hutokana na ngazi ya vyeo am zoezi lote la maudhui na ratiba kwa kawaida lilikuwa chini ya idara yake! Akagawa pande ila aliowapa pande hawakumkiri hadharani…!

Mwisho kabisaa… Moja ya sifa kubwa ya mashabiki wa hii timu yake hupambana sana kuilinda timu yao😁 Kunaweza kuwa na doa la dhahiri ila wakiamua kusimama kusema sio doa hutawaweza!

Hata ya jana sio kama hawajui kuwa HAIKUWA SAWA… Wanajua sana İLA wao huwa hawapo tayari kuona sega lolote likiangukia kanzu yao!

Again… CONGRATS ALLY KAMWE Kusitiri makosa yaliyojitokeza!
 
Amemkimbia
Screenshot_20240728-222638 (2).png
Screenshot_20240728-222638 (2).png
 
Back
Top Bottom