Yupo wapi siku hizi?

Yupo wapi siku hizi?

Yes kama mfuatiliaji wamuziki hili ndo jina alilotumia kwenye ile star search ya coca cola nahisi..
Ndipo lilipopatikana kundi la WAKILISHA
Witness--WAKI
Langa-- LI
Sarah-- SHAA
Kundi lilipovunjika Sarah akaondoka na SHAA yake.. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Walitengeneza hit song kama Hoi na Kiswanglish
Jina la Shaa alipewa na marehem mangwea walipofanya hii collabo mwanzo jina alikua anatumia lake halali la Sarah kaisi ndio mangwea akamuita shaa na likapita mpaka leo
 
Binafsi ningependa kufahamu wako wapi

1. Eluka. Aliimba 'Nikizipata'.
2. ML Chris na 'Antonia from Cuba (kuba)'. Walikuwa wanafanya The Weekenda nadhani, Clouds FM back in the day kila Ijumaa from 4 to 6 jioni. Loved that show.
3. Dj Yusuf. Aliimba 'mbele kwa mbele'
4. Dani Msimamo. Aliimba 'Wapo wanaotaka, moja ya ngoma kali sana za rap Bongo. Nadhani aliwalenga Clouds.
5. Dunga wa Mandugu Digital.
DJ yusuph yupo marekani
 
'Da Jo' from Kigamboni.... the female emcee who made me start internalising bongo hip hop. I loved muuuch ile flow yake ya kurap.

'Da Jo' yupo wapi nowadays? Anafanya nini?

One of my most favourite female emcees wa bongo hip hop by then.

-Kaveli-
Da Jo tumekukubali, na bado nadhani kuna swali [emoji23][emoji23] lilikua bonge la Ngoma hili
 
'Da Jo' from Kigamboni.... the female emcee who made me start internalising bongo hip hop. I loved muuuch ile flow yake ya kurap.

'Da Jo' yupo wapi nowadays? Anafanya nini?

One of my most favourite female emcees wa bongo hip hop by then.

-Kaveli-
Ah we da jo tumekukubali...
Na bado nadhani kuna swaliii... [emoji23] [emoji23]

Kuna ile, "we si ndo uloleta nyodo, unataka soo"
 
Hapana baada ya sarah kujitoa wakilishaa
Langa na witness wakabadili jina wakajiita WAKILI
Ndipo Sarah kiutani akaona ajiite "Shaa" zile herufi za mwisho za kundi...
Sio marehem ngwair aliyempa jina
Jina la Shaa alipewa na marehem mangwea walipofanya hii collabo mwanzo jina alikua anatumia lake halali la Sarah kaisi ndio mangwea akamuita shaa na likapita mpaka leo
 
Hapana baada ya sarah kujitoa wakilishaa
Langa na witness wakabadili jina wakajiita WAKILI
Ndipo Sarah kiutani akaona ajiite "Shaa" zile herufi za mwisho za kundi...
Sio marehem ngwair aliyempa jina
Bro ukicheki hyo video ambayo ndio ngoma ya kwanza ya shaa after kutoka wakilisha bdo alikua akitumia Sarah kaisi.. na ktk verse ya ngwea ndio akatamka shaa na ndio likapita. Aliwahi kuielezea pia kipindi cha msiba wa Ngwea bado naitafuta link ntaiweka pia hapa
 
'Da Jo' ndo emcee pekee aliyesahaulika mazima. Hakunaga mwananzengo yeyote mwenye info yoyote kuhusu huyo mdada. Nilishamuulizia sana humu mara nyingi pasipo kupata any tips. Na tracks zake nazitafuta sanaaaa bila mafanikio.

Da Joo... wherever you are, much luv to ya.

-Kaveli-
 
Frola nducha huwa na msikia kwenye redio ya Umoja wa Mataifa
 
Miaka ileeee.... unamsikiiza Da Jo akipasuka kwa spika, mara unamsikiiza Zay B yupo gado, mara gafla umamsikia Sista P anakuja. Mara paap unamsikiiza Sir Nature Kiroboto na rap katuni zake akimlilia Sinta. Kabla hujabadili radio station, gafla unamsikiiza Crazy GK naye anaauliza 'atakufaje' baada ya kumzika 'sister sister'.

Hujakaa sawa, unamsikia Jay Moe anaelezea 'majukumu' na 'ulimwengu ndiyo mama' baada ya kuwa amechoshwa na 'maisha ya boarding'.

Mara gafla unamsikia Mentali prof Jay anapamba Jina Lake na kueleza jinsi alivyoopoa demu mkali kwa zali. Mara paap, unamsikia Mwana FA anakwambia ye na mabinti damdam. Gafla kwa mbaaaali unaisikia 'sista duu kama unataka kuja home'.

Aaarggh... Those days when swahili rap was real music.

-Kaveli-
 
kwa mujibu wa Bi Star wa kaole Nyamayao yupo nchini china akifanya kutafsiri sinema/ tamthilia zao kwa kuweka maneno ya kiswahili.

Haya niloongea nae live tukiwa safarini toka dar kwenda morogoro.

Kibakuli kwa sasa ni camera man. Nasikia jamaa ni video shooter mzuri tu. Anafanya pia editting...
 
Tabia wa kidedea ni marehemu nadhani

Yuko wapi Frank Mtao wa channel 10 mara ya mwisho nilisikia yupo China

Na Kuna jamaa aliyekuwa anafanya hihhop base ya eatv kabla ya Saigon
 
zamani ukikumbuka unaweza ukamwaga hata chozi yani hivi wako wapi sumbi na bocha,abiola, bupe na aunt seche wa kaole, yu wapi dada alieimba maprosooo

Dada Othiambo, unamkumbuka Da Jo?

-Kaveli-
 
Big doggy Pose

Watoto wa juzi hawawezi wajua hawa.

Wao wanamjua harmonize na lavalava tu

Enzi hizo BDP wanatesa na ngoma ya "make wa MTU ni sumu na majobless au ile ya wanaokwenda jela Ft inspector harun ,harmonize alikuwa Ntwara anacheza mdako na kibababa lava lava alikuwa kwao mitaa ya uswazi dar hapo alivalishwa nepi

Hahahaha
Umechanganya Madawa mkuu..Ma-jobless ni BDP(Bigdogg Pose) waliokuwa wanafanya recording zao na Amit Bajaj Mentor.
Wapo kinondoni shamba kwa msokota nywele
Walioimba "Mke wa mtu Sumu" na "wanaokwenda jela" wanaitwa LWP (Life with Purpose) walikuwa wana record na Pfunk nadhani wapo TMK
 
Back
Top Bottom