TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

MAGUFULI ALITAKA KUMUOKOA KWA KUMUACHISHA NGADA YEYE NA WAISIHARAMU WENZAKE WAKAMTUKANA NA KUMWITA DICTATOR...CHEKI SASA NGADA ZIMEMUONDOA BAADA YA KUCHANGANYA PODA ZA MADAWA YA KULEVYA NA DAWA ZA MAHOSPITALINI ...NIKAMA MLEVI WA POMBE ANAPO KUWA NA DOZI YA DAWA ZA HOPITALINI ANASHAURIWA KUTULIA KUNYA POMBE KWANZA MAANA UKICHANGANYA MAMBO YANAKUWA SIYO ....
Jiwe kachangia kifo cha manji
 
View attachment 3029953
Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Pia soma
- Yusuf Manji apoteza sifa ya kuwa Diwani wa Mbagala Kuu kwa kushindwa kuhudhuria vikao


 
Back
Top Bottom