TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

View attachment 3029953
Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.
Apumzike kwa Amani mwananchi huyu. Kuna kipindi alituheshimisha.
 
Waliokabidhiwa hizo mali wajiongeze zaidi ya yeye
 
Mbona mtandaoni hakuna hiyo stori? If it is true RIP Manji.

Huu mwaka ni mbaya mno kuwahi kutokea, hapa ni June tu kuna vifo vingi sana vya watu wa kawaida na maarufu duniani mf vifo vya viongozi kama Rais wa Iran, Makamu Rais Malawi, Mkuu wa Majeshi Kenya, yani kuna mabalaa kila mahali , kuuwawa watu kwenye ukumbi Russia, mafuriko makubwa yaliyoua watu wengi Dubai, India, Kenya, TZ, Burundi nk, vifo vya mahujaji zaidi ya 1000 kwa joto huko Saudi Arabia, kuuwawa protesters Kenya watoto wa Gen Z sijui wamefika 27 , lakini kitu kibaya zaidi ni vifo vya watoto wasio na hatia hapa TZ mtoto albino asie na nguvu za kupigania uhai wake kwa madhalimu akiwemo baba yake mzazi, mtoto Asimwe na huko Gaza watoto wadogo wanauwawa sana kwa kupigwa mabomu, kunyimwa chakula, kunyimwa matibabu na dunia nzima imebariki iko kimya , pia kuna vita kali ya Gaza, Myanmar, Sudan, Congo DR, Ukraine watu wanauwawa sana huko nk.

My take :
Allah is not happy with the world for genocide in Gaza ambako ni ardhi takatifu iliyomtoa Nabii Issa bin Mariam, Nabii Mussa, nk kule watu hawana chakula, hawana pa kulala na hawana maji , wanapigwa mabomu mda wote na dunia nzima ikitazama tu. Tumuombe sana Mungu maana bado kuna miezi 6 mbele balaa kila mahali, kila kukicha!
Ni kawaida. Dunia ina watu more than 7,000,000,000. Kama kwa mwaka 1% ya hao wanafariki, that means kwa mwaka wanafariki watu 70,000,000. Hiyo ni sawa na watu 191,781 kila siku. So, probability p(x) kwamba atafariki mtu maarufu kwa mwaka ni kubwa; so it's normal.
 
Back
Top Bottom