Yusuf Manji mikononi mwa TAKUKURU baada ya kurejea nchini

Yusuf Manji mikononi mwa TAKUKURU baada ya kurejea nchini

maliyamungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
564
Reaction score
419
Mfanyabiashara wa Tanzania Yusuf Manji anashikiliwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchi Tanzania Takukuru akikabiliwa na tuhuma tatu, baada ya kurejea nchini Tanzania kutoka nje ya nchi .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Takukuru kamishna wa Polisi Said Hamduni, Manji anashikiliwa toka alipowasili nchini Tanzania akituhumiwa kukwepa kodi.

Kampuni zake za Intertrade Commercial LTD Service na Golden Globe International Service Limited zinatuhumiwa kwa kutolipa kodi ya VAT kati ya mwaka 2011 na 2015 wakati zikifanya biashara na Shirika la Umeme nchini Tanzania Tanesco Kupitia kampuni yake ya Golden Globe.

Kamishana Hamduni anasema kulifanyika udanganyifu wakati wa manunuzi ya kampuni ya Tigo.

Tuhuma nyingine inayomkabili ni kupitia kampuni yake ya Quality Group kuhusu mapato ya klabu ya Yanga ambayo alikuwa akiidhamini na kuiongoza kama mwenyekiti wakati huo.

Manji alitorokea nje ya nchi mwaka wa 2018 baada ya Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kumuachia huru pamoja na wenzie watatu mwezi Septemba 2017 walipokuwa wakituhumiwa kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Alituhumiwa pia kuhujumu usalama wa taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeza sare za jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania.

Manji amerejea nchini Tanzania siku chache baada ya Rais Samia Suluhu kuhimiza wafanyabiashara waliotoroka nchi kurejea na kuendelea na uwekezaji wao.

Chanzo: BBC
 
Kipindi hiki cha awamu ya sita, kuhojiwa na TAKUKURU haitishi sana kama ktk awamu ya tano ambayo watendaji walioteuliwa na mwendazake hawakuwa huru na walikuwa ktk shinikizo la kukomoana na pia awamu ya tano haikusisitiza haki kutendeka.

Hivyo tufuatilie kwa ukaribu kuona kama haki itatendeka kufuatana na matamko ya awamu ya sita.
 
Huyu mama anaanza kunipa wasiwasi
Ni kama anacopy ujinga wa jiwe.

Alikemea takukuru walikuwa wanafanya kazi zisizowahusu lakini na yeye anawatumia kwa kazi zisizowahusu..yani anapita mlemle kwa jiwe.

Kazi za kiuchunguzi wa ubadhirifu wa fedha anatakiwa kwanza apewe CAG au timu ya uchunguzi.Ripoti ya CAG/timu ya uchunguzi ndiyo inayokabidhiwa kwa takukuru kama CAG/timu wakiona dalili za rushwa.

Hawa CCM vipi?
 
Hapo kuna Rushwa gani mpaka Takukuru waanze kumhoji manji ?hii itapelekea kuzuia uwekezaji tena kwani watakosa imani na Tanzania kwa kuona vyombo hujishughurisha na uchunguzi hata usio na Rushwa
Unawasemea wawekezaji ?!!!

Umeyafumba macho kuwaona kuwaona akina Dangote ,Mwanamfalme wa Dubai ,Mwanamfalme wa Saudia na wengineo wakitiririka kama mvua katika nchi hii ya amani ?!!

#KaziIendelee
 
Kipindi hiki cha awamu ya sita, kuhojiwa na TAKUKURU haitishi sana kama ktk awamu ya tano ambayo watendaji walioteuliwa na mwendazake hawakuwa huru na walikuwa ktk shindikizo la kukomoana na pia awamu ya tano haikusisitiza haki kutendeka.

Hivyo tufuatilie kwa ukaribu kuona kama haki itatendeka kufuatana na matamko ya awamu ya sita.
Kuna vitu huelewi.

CAG mara nyingi anakagua taratibu kama zilifuatwa ama lah. Mnaweza kufuata taratibu na mkala hela na CAG asijue lakini uchunguzi utajua.

CAG anakagua kama taratibu zilizowekwa za matumizi zinafuatwa, uchunguzi kama wa TAKUKURU unahakikisha kama kweli hicho kitu kilifanyika, bei yake halisi, anataftwa muuzaji, wanajirodhisha uhalali wa lisiti iliyoletwa, wanawez kuomba bank statement ya account ya muuzaji nk.

Uchunguzi hugundua mambo mengi zaidi kuliko ukaguzi.
 
Huyu mama anaanza kunipa wasiwasi
Ni kama anacopy ujinga wa jiwe..
Alikemea takukuru walikuwa wanafanya kazi zisizowahusu lakini na yeye anawatumia kwa kazi zisizowahusu..yani anapita mlemle kwa jiwe..
Kazi za kiuchunguzi wa ubadhirifu wa fedha anatakiwa kwanza apewe CAG au timu ya uchunguzi.Ripoti ya CAG/timu ya uchunguzi ndiyo inayokabidhiwa kwa takukuru kama CAG/timu wakiona dalili za rushwa..
Hawa ccm vipi?!!!!
Unajuaje kama kadhia yake tayari haikuwa TAKUKURU?
 
Back
Top Bottom