Yusuf Manji mikononi mwa TAKUKURU baada ya kurejea nchini

Huu ndio mtihani wa kwanza kwa Mama na Hamduni. Hilo la Manji litakuwa kuwapa Imani wawekezaji na ili waamini nia njema ni lazima amuachie Manji

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Hakna kitu hapa hii ni janja janja ya kuwahadaa wananchi tyuuh, kwani unadhan Manji ni mjinga kurudi tena TZ.
 
Wewe ni kajinga yani!
.
Kwa hiyo unataka na Manji nae apewe nafasi ya kupiga maana sisi tumepiga sana?
.
Huu utetezi wenu kwa Manji faida yenu hasa ni kitu gani?

Vyombo vya dola ndio vinajua mengi zaidi juu ya huyo Manji ila wewe kapuku uko hapa kumtetea wakati bibi zako kule kijijini hata hela ya panadol hawana?
 
Mama alitwambia lakini yeye na dhalimu magufuli ni KITU KIMOJA! Sukuma GANG bado wameshika usukani ili kumuenzi dhalimu hawataki Kikwete awazidi KETE!
Sasa kwani hii ni zama ya kikwete? Mambo mengine tuwage wakweli na wa wazi, nchi kuendeshwa kwa remote ni ujinga mkubwa sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Nafasi ya kupiga ipi? Kwani alivyokuwa ananunua mbaazi alikuwa anawapiga? Alivyotaka kuuziwa coco beach na KMC ndio kupiga? Acha Ujinga wewe zero brain.
 
Msije kushangaa kesho kutwa anaingia ikulu kuzungumza na mama
🤣🤣🤣🤣 hakuna tatizo kabisa,na mimi nipo huku nilipo najiibia zangu chaki na kuchapa vibinti vyenu kama marupurupu
 
Manji vs Sabaya nani anafadhali 😭😭😭
 
Umemaliza Mkuu, ELIMU YA RUSHWA INAHITAJIKA KWA KIWANGO KIKUBWA MNO...

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja tuone itakuwaje
Nalog off
 
Unajuaje kama kadhia yake tayari haikuwa TAKUKURU?
FaizaFoxy Habari ya mwaka mpya umejichimbia kinyama natumai umekuja na nondo mpya za udini karibu sana jukwaa lilipooza kukosa watu kama wewe
 
Hapo kuna Rushwa gani mpaka Takukuru waanze kumhoji manji ?hii itapelekea kuzuia uwekezaji tena kwani watakosa imani na Tanzania kwa kuona vyombo hujishughurisha na uchunguzi hata usio na Rushwa
Reposted from @udaku_magazine TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
_
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwa inamshikilia mfanyabishara Yusuf Manji kwa mahojiano kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamdun amesema kuwa Manji ambaye amerejea nchini baada ya kuondoka tangu mwaka 2018 anatuhumiwa kwa makosa matatu.

CP Hamdun amesema tuhuma hizo zinahusisha kampuni zake za Intertrade Commercial Ltd Serivice na Golden Globe International Service Limited.

Tuhuma ya kwanza ni kuisababishia serikali hasara kwa kukwepa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na udanganyifu wakati akifanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Pili, inadaiwa kuwa kupitia kampuni ya Golden Globe alifanya udanganyifu wakati wa kununua hisa za kampuni ya mawasiliano ya Tigo.

Tatu ni tuhuma ya mapato ya Yanga SC yanayohusu kampuni ya Quality Group.

Manji alikamatwa juzi katika uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili nchini.
 

Wewe ndo unatupa wasiwasi wa uwezo wako wa kuelewa.
Kwani Manji hakuwahi kuchunguzwa awali ? Mambo ya kodi au Yanga ni ya Leo.. ?
Mlizoea mtu wa kubwatuka bwatuka ovyo....
 
Kipindi hicho serekali ilikua wapi zaidi ya miaka 10?
 
Hata wewe umepotea kidogo, CAG 'hatumwi' na Rais; na report yake anawasilisha kwa bunge.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Kama mlimshindwa kipindi cha Jiwe ndiyo mumuweze leo; kwanza jiulizeni kwa nini ameamua kurudi sasa na si wakati mwingine wowote !!
Usiingie kwenye huu mtego. Manji hakurudi kwa bahati mbaya. Ni mikakati hii. Si ajabu ukienda utamkuta nyumbani kwake amejipumzisha huku mitaani watu wanatukakana kwa mambo wasiyoyajua. Manji ni mpigaji kama wapigaji wengine tu na hana usafi wowote. Hili la kutangaza kuwa ''anashikiliwa'' ni mikakati ya kumsafisha tu ili wenye uelewa wasiseme serikali inakumbatia mafisadi yaliyokuwa yamekimbia. Hivi mnafanya Manji ni mjinga na amerudi bila kwanza kuhakikisha kila kitu kitaenda vizuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…