Song il gok
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 878
- 938
· Manji anaingia ubia na Yanga na kuamua kuchukua asilimia 75 ya mapato huku akiiachia klabu asilimia 25 na kubeba hasara yote. Kumbuka Mzigo wa gharama zote pamoja na hasara za timu zitabebwa na Manji, Mishahara pamoja na gharama zote za uendeshaji zitabebwa na Manji na baada ya miaka 10 timu itabaki kuwa mali ya wanachama huku akiwa amependekeza kama ni suala la kiwanja yeye hatopenda kijengwe nje ya mji kwakuwa watazamaji hawajitokezi pindi kiwanja kinapokuwa nje ya mji na kama wanachama wataridhia basi kwahiyo asilimia 25 itakayopatikana ataitumia kujenga uwanja kama wengi walivyopendekeza katika mkutano wa dharula uliofanyika Diamond Jubilee. Anachotaka Manji ni kuiendesha klabu kwa mfumo wa kibiashara kitu ambacho timu zetu zimeshindwa kufanya kwa Zaidi ya miaka 80.
· Mo’ Dewji kwa upande wake anafanya ujanja ujanja anaichukua Simba BURE kwa kudai anainunua timu kwa bilioni 20 huku akiitumia pesa hiyohyo kununua treasury bonds (hisa za serikali kisha mapato yatokanayo na faida ya kununua hisa hizo za serikali, atagawana na klabu na kuchukua asilimia 51 ya faida hiyo huku akiipatia Simba asilimia 49 wakati huo huo akiwa ameinunua timu. Ikumbukwe Hanspope kwa sasa ana hali mbaya kifedha toka sakata la sukari lichukue sura mipango yake ya kifedha imeenda kombo, Kaburu alikuwa anategemea mchongo wa kibali cha kuingiza mbolea ambacho alijipatia uwakala wa Afrika Mashariki na kati na hakuna mbolea iliyokuwa inaingia hapa nchini bila kupitia kwake, huo ujanja ujanja kwa Magufuli umekwisha nae ana hali mbaya kifedha, Aveva sio siri huyu alikuwa mfanyakazi wa Mo’ na alikuwa Mo’ Foundation.
Kwahiyo kwa hili ni wazi kuwa Mo’ amewaingiza mkenge wana Simba kiujanjaunja MILELE na hii yote inatokana na kuhujumu timu ifanye vbaya ili washabiki wasiingie uwanjani ili ikose mapato na nguvu ya ushindani ili kipindi anajitokeza na dau lake aonekane kama Mungu mtu na muokozi wa timu na kiukweli dhamira yake imefanikiwa mpaka sasa. Na ukizingatia yeye ni mwanasiasa akaongeza na nguvu ya wanasiasa wapenda dezo ili kuipigia makelele ishu ya Manji na Yanga ambayo wanachama wamebariki kwa asilimia 200 ili suala lake la kuwalaghai wanasimba lipite bila kelele.
Wote tumeona jinsi mkuu wa mkoa alivyoshikwa mabega uwanja wa taifa na kulishwa keki siku ya Simba Day wakiashiria kubariki ulaghai huo ila chakushangaza baada ya kushiba keki Makonda kaanza kushikilia bango suala la Yanga na Manji akielewa fika kuwa Mo ataumbuka endapo watanzania watagundua utapeli anaofanya Mo.
· Ikumbukwe bilioni 20 alizotoa Mo ni bei aliyojiamulia yeye bila kuweka wazi vigezo alivyotumia kufikia kwnye uamuzi wa kutoa dau hilo, Simba ni timu na inavitega uchumi. Kwahiyo kununua asilimia 51 za hisa ni kujipa umiliki wa mali zote za klabu. Ni Dhahiri kwamba bei ya hisa za timu itapanda baada ya uwekezaji hivo ni wazi kabisa hapo baadae hakuna mwanachama ambaye atakuwa na uwezo wa kununua hisa za timu, Mo atarudi tena na wazo la kumalizia sehemu za hisa hivyo basi kuwa mmiliki wa asilimia 100, wakati upande wa pili Yanga itabaki na mali zake zote yani timu na vitega uchumu vya klabu; Jangwani na nyumba ya Mafia.
#YangayetuSimbayake