Yusuph Manji anakodi Yanga, Mo Dewji anachukua bure Simba

Yusuph Manji anakodi Yanga, Mo Dewji anachukua bure Simba

Song il gok

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
878
Reaction score
938
· Manji anaingia ubia na Yanga na kuamua kuchukua asilimia 75 ya mapato huku akiiachia klabu asilimia 25 na kubeba hasara yote. Kumbuka Mzigo wa gharama zote pamoja na hasara za timu zitabebwa na Manji, Mishahara pamoja na gharama zote za uendeshaji zitabebwa na Manji na baada ya miaka 10 timu itabaki kuwa mali ya wanachama huku akiwa amependekeza kama ni suala la kiwanja yeye hatopenda kijengwe nje ya mji kwakuwa watazamaji hawajitokezi pindi kiwanja kinapokuwa nje ya mji na kama wanachama wataridhia basi kwahiyo asilimia 25 itakayopatikana ataitumia kujenga uwanja kama wengi walivyopendekeza katika mkutano wa dharula uliofanyika Diamond Jubilee. Anachotaka Manji ni kuiendesha klabu kwa mfumo wa kibiashara kitu ambacho timu zetu zimeshindwa kufanya kwa Zaidi ya miaka 80.

· Mo’ Dewji kwa upande wake anafanya ujanja ujanja anaichukua Simba BURE kwa kudai anainunua timu kwa bilioni 20 huku akiitumia pesa hiyohyo kununua treasury bonds (hisa za serikali kisha mapato yatokanayo na faida ya kununua hisa hizo za serikali, atagawana na klabu na kuchukua asilimia 51 ya faida hiyo huku akiipatia Simba asilimia 49 wakati huo huo akiwa ameinunua timu. Ikumbukwe Hanspope kwa sasa ana hali mbaya kifedha toka sakata la sukari lichukue sura mipango yake ya kifedha imeenda kombo, Kaburu alikuwa anategemea mchongo wa kibali cha kuingiza mbolea ambacho alijipatia uwakala wa Afrika Mashariki na kati na hakuna mbolea iliyokuwa inaingia hapa nchini bila kupitia kwake, huo ujanja ujanja kwa Magufuli umekwisha nae ana hali mbaya kifedha, Aveva sio siri huyu alikuwa mfanyakazi wa Mo’ na alikuwa Mo’ Foundation.

Kwahiyo kwa hili ni wazi kuwa Mo’ amewaingiza mkenge wana Simba kiujanjaunja MILELE na hii yote inatokana na kuhujumu timu ifanye vbaya ili washabiki wasiingie uwanjani ili ikose mapato na nguvu ya ushindani ili kipindi anajitokeza na dau lake aonekane kama Mungu mtu na muokozi wa timu na kiukweli dhamira yake imefanikiwa mpaka sasa. Na ukizingatia yeye ni mwanasiasa akaongeza na nguvu ya wanasiasa wapenda dezo ili kuipigia makelele ishu ya Manji na Yanga ambayo wanachama wamebariki kwa asilimia 200 ili suala lake la kuwalaghai wanasimba lipite bila kelele.

Wote tumeona jinsi mkuu wa mkoa alivyoshikwa mabega uwanja wa taifa na kulishwa keki siku ya Simba Day wakiashiria kubariki ulaghai huo ila chakushangaza baada ya kushiba keki Makonda kaanza kushikilia bango suala la Yanga na Manji akielewa fika kuwa Mo ataumbuka endapo watanzania watagundua utapeli anaofanya Mo.

· Ikumbukwe bilioni 20 alizotoa Mo ni bei aliyojiamulia yeye bila kuweka wazi vigezo alivyotumia kufikia kwnye uamuzi wa kutoa dau hilo, Simba ni timu na inavitega uchumi. Kwahiyo kununua asilimia 51 za hisa ni kujipa umiliki wa mali zote za klabu. Ni Dhahiri kwamba bei ya hisa za timu itapanda baada ya uwekezaji hivo ni wazi kabisa hapo baadae hakuna mwanachama ambaye atakuwa na uwezo wa kununua hisa za timu, Mo atarudi tena na wazo la kumalizia sehemu za hisa hivyo basi kuwa mmiliki wa asilimia 100, wakati upande wa pili Yanga itabaki na mali zake zote yani timu na vitega uchumu vya klabu; Jangwani na nyumba ya Mafia.
Yanga 1.jpg

#YangayetuSimbayake
 
Bora kununua kwa bil 20 kuliko kukodi bure..... Kila mwaka atawaambia kapata hasara na hakuna faida ya kugawana na baada ya miaka 10 atawapa yanga yenu ile ile ikiwa na kila kitu kilekile bila kupiga hatua yoyote.... Poor yanga
 
naelewa sana mawazo yenu wewe wa mchangani. Acha umbumbumbu
 
· Manji anaingia ubia na Yanga na kuamua kuchukua asilimia 75 ya mapato huku akiiachia klabu asilimia 25 na kubeba hasara yote. Kumbuka Mzigo wa gharama zote pamoja na hasara za timu zitabebwa na Manji, Mishahara pamoja na gharama zote za uendeshaji zitabebwa na Manji na baada ya miaka 10 timu itabaki kuwa mali ya wanachama huku akiwa amependekeza kama ni suala la kiwanja yeye hatopenda kijengwe nje ya mji kwakuwa watazamaji hawajitokezi pindi kiwanja kinapokuwa nje ya mji na kama wanachama wataridhia basi kwahiyo asilimia 25 itakayopatikana ataitumia kujenga uwanja kama wengi walivyopendekeza katika mkutano wa dharula uliofanyika Diamond Jubilee. Anachotaka Manji ni kuiendesha klabu kwa mfumo wa kibiashara kitu ambacho timu zetu zimeshindwa kufanya kwa Zaidi ya miaka 80.

· Mo’ Dewji kwa upande wake anafanya ujanja ujanja anaichukua Simba BURE kwa kudai anainunua timu kwa bilioni 20 huku akiitumia pesa hiyohyo kununua treasury bonds (hisa za serikali kisha mapato yatokanayo na faida ya kununua hisa hizo za serikali, atagawana na klabu na kuchukua asilimia 51 ya faida hiyo huku akiipatia Simba asilimia 49 wakati huo huo akiwa ameinunua timu. Ikumbukwe Hanspope kwa sasa ana hali mbaya kifedha toka sakata la sukari lichukue sura mipango yake ya kifedha imeenda kombo, Kaburu alikuwa anategemea mchongo wa kibali cha kuingiza mbolea ambacho alijipatia uwakala wa Afrika Mashariki na kati na hakuna mbolea iliyokuwa inaingia hapa nchini bila kupitia kwake, huo ujanja ujanja kwa Magufuli umekwisha nae ana hali mbaya kifedha, Aveva sio siri huyu alikuwa mfanyakazi wa Mo’ na alikuwa Mo’ Foundation. Kwahiyo kwa hili ni wazi kuwa Mo’ amewaingiza mkenge wana Simba kiujanjaunja MILELE na hii yote inatokana na kuhujumu timu ifanye vbaya ili washabiki wasiingie uwanjani ili ikose mapato na nguvu ya ushindani ili kipindi anajitokeza na dau lake aonekane kama Mungu mtu na muokozi wa timu na kiukweli dhamira yake imefanikiwa mpaka sasa. Na ukizingatia yeye ni mwanasiasa akaongeza na nguvu ya wanasiasa wapenda dezo ili kuipigia makelele ishu ya Manji na Yanga ambayo wanachama wamebariki kwa asilimia 200 ili suala lake la kuwalaghai wanasimba lipite bila kelele. Wote tumeona jinsi mkuu wa mkoa alivyoshikwa mabega uwanja wa taifa na kulishwa keki siku ya Simba Day wakiashiria kubariki ulaghai huo ila chakushangaza baada ya kushiba keki Makonda kaanza kushikilia bango suala la Yanga na Manji akielewa fika kuwa Mo ataumbuka endapo watanzania watagundua utapeli anaofanya Mo.

· Ikumbukwe bilioni 20 alizotoa Mo ni bei aliyojiamulia yeye bila kuweka wazi vigezo alivyotumia kufikia kwnye uamuzi wa kutoa dau hilo, Simba ni timu na inavitega uchumi. Kwahiyo kununua asilimia 51 za hisa ni kujipa umiliki wa mali zote za klabu. Ni Dhahiri kwamba bei ya hisa za timu itapanda baada ya uwekezaji hivo ni wazi kabisa hapo baadae hakuna mwanachama ambaye atakuwa na uwezo wa kununua hisa za timu, Mo atarudi tena na wazo la kumalizia sehemu za hisa hivyo basi kuwa mmiliki wa asilimia 100, wakati upande wa pili Yanga itabaki na mali zake zote yani timu na vitega uchumu vya klabu; Jangwani na nyumba ya Mafia.

#YangayetuSimbayake
Fact mkuu. Ni muda ufike sasa tuendeshe clubs zetu za mpira kisasa zaidi na kwa faida.
 
Bora kununua kwa bil 20 kuliko kukodi bure..... Kila mwaka atawaambia kapata hasara na hakuna faida ya kugawana na baada ya miaka 10 atawapa yanga yenu ile ile ikiwa na kila kitu kilekile bila kupiga hatua yoyote.... Poor yanga
Unataka hatua gani labda we mbumbumbu?kwani huoni jinsi tunavyowala kila siku?tunachotaka mashabiki ni raha au hujui hilo?angalia nje makocha wanavyofukuzwa kwa kuwanyima raha mashabiki,tunachotaka ni vikombe na burudani hayo mengine chukueni nyie na mooooo
 
Fact mkuu. Ni muda ufike sasa tuendeshe clubs zetu za mpira kisasa zaidi na kwa faida.
Ni kweli mkuu.Na katika hili ukweli upo bayana. Kati ya hawa wawekezaji wawili inaonekana kabisa yupi ana mipango ya maendeleo.
 
Unataka hatua gani labda we mbumbumbu?kwani huoni jinsi tunavyowala kila siku?tunachotaka mashabiki ni raha au hujui hilo?angalia nje makocha wanavyofukuzwa kwa kuwanyima raha mashabiki,tunachotaka ni vikombe na burudani hayo mengine chukueni nyie na mooooo
Asante mkuu nasmapesa endelea kuwatibu hao vyura. Ujinga wao unaonekana ni wa kurithi au wamejaaliwa na waganga wa kienyeji
 
Mo tapeli tu
Na Manji nae walewale....

Waswahili njaa nazi hazina adabu

mtu anakuja kuposa binti yako unamlilia 'amchukue bure'
The Boss Kati ya watu hawa wawili nani anaonekana kuchukua bure bure?! Mtu alijitoa miaka 15 imepita leo anarudi kutafuta nini. Au na wewe ni wale wateja wa Snura mkuu?!
 
Wote 'matapeli'
Mkuu unaonekana umejaa hasira. Bilioni 20 ndio 51% ya Simba?! So akitaka kukaa miaka 40 bado atawapa 20B na atakua amepata ngapi yeye. Nani atachangia hio nyingine mkuu.Kuna mwanasimba ataweza kununua hisa za 19B?! Au ndo watajazwa mamluki. Ngoja kina "akilimali" wa chura snura nao watibuliwe maslahi yao utajua tuu
 
Wanachama wa Simba na Yanga wote wana Tatizo moja la msingi. Tatizo Hilo ni "MAARIFA NA WELEDI" juu ya soko la soka.

Suala la kununua au kukodi klabu sio Tatizo. Tatizo ni kwa kiasi gani unaweza kufanya "mapatano" ya kuuza au kukodi kitu ambacho hujui thamani yake. Chifu Mangungo wa Msovero alifanya hivyo, serikali imefanya hivyo, ni ajabu na aibu kwa wanachama wa Simba na Yanga kurudia makosa yale yale.

Mbali ya majengo na rasilimali zenye kuonekana Simba na Yanga wana rasilimali kubwa isiyoonekana ambayo kitaalamu inaitwa "GOODWILL". Je, ni nani kati yetu ajuae thamani ya vilabu hivi viwili. Tunahitaji kwa hakika na bila shaka kujua thamani halisi ya vilabu hivi ili mchakato ima wa kukodisha au kuuza hisa ufanyike.

Yanga na Simba ni migodi inayotembea, tuitendee haki. Wapo watu waliozifanya klabu hizi kuwa hapo zilizopo, ni aibu na fedheha kubwa kwetu kudharau michango ya wazee wetu hao na kuzitoa klabu hizi bure. Kama sio kutetemeka basi watatikisika huko "MAKABURINI".
 
Mkuu Ngwananzengo ulianza vizuri lakini kwa hapa "Mbali ya majengo na rasilimali zenye kuonekana Simba na Yanga wana rasilimali kubwa isiyoonekana ambayo kitaalamu inaitwa "GOODWILL". umekurupuka.Hamna kitu kama hicho kiuchumi.
 
Mimi uchambuzi wangu sio wa KIUCHUMI. Mimi uchambuzi wangu umeegemea katika masuala ya fedha na uhasibu. Kama kiuchumi hakuna "goodwill" Ni sawa lakini kumbuka masuala ya makampuni hasa hisa na masoko yanategemea sana "goodwill". Pengine kama huifahamu vizuri naomba nikuelimishe.

"Goodwill "Ni taswira ambayo kampuni au taasisi imejijengea katika jamii. Simba kwa misimu 4 mfululizo haina matokeo mazuri ndani ya uwanja. Azam wanatimu nzuri na matokeo mazuri ndani ya uwanja. Azam akienda kucheza na Mbeya city au Toto Afrika hawezi kupata idadi ya watu ambao Simba itapata. Hii ndio "goodwill", Kwa maana hiyo taswira ya Simba tayari imeshajigenga ndani ya nafsi na mioyo ya watu wengi ima wawe wana Simba au si wana Simba.
 
Hivi "MO" si alianzisha Singida united ilipotelewa wap?na african lyon ia iko wap?

#Yanga ya kimataifa#
 
Back
Top Bottom